Acha kumpigia mbuzi gitaa....Angalia jinsi ya kumsaidia Mwalimu Hamisi kwanza ili asivunjike moyo wa kusomesha Watazania wenzetu. Serikali yetu ni sikio la kufa, halisikii dawa!
I propose "Saidia shule ya msingi Saninga Fund"
Umewahi mno soma post inayokufata 'Oysterbay' je wewe umekuja na idea gani ya kusaidia? ninachosema mimi wakina Hamisi wako wengi sana Tz hii
Shahada(degree)= 310,000; stashahada(dip.)=280,000; Cheti(certificate)= 120,000= Yawezekana ndio mshahara wa mwl Hamisi kama hajapandishwa daraja!!
Pia hii mishahara ni Gross sallary (haijakatwa kodi)!
Wewe waweza? Naamini huwezi! Sasa tumlaumu nani matokeo ya mitihani yanapokuwa mabaya?
Unafikiri tatizo ni chama tu kweli? unafikiri chama kingine kinaweza kuwafanya walimu wakae huko?
Naweza kuchangia baiskeli ya huyu mwalimu ila sijui itamfikiaje? My Pledge
Tumain asante kwa moyo wa kujitolea.....jinsi ya kumfikia labda chanzo cha hii habari (ulipoitoa ) aweza kuwa msaada zaidi.
Ila zaidi ya baiskeli kama wengine walivoshauri labda tuone jinsi gani twaweza kumsaidi a mwalimu huyu (japo wakina Hamisi ni wengi Tz) lakini kwa kuanzia lets see how we cana help him out
aaaah pity!!!!
Chanzo ni gazeti la mwananchi (TZ) na mimi niko nje ya nchi...tushauriane namna ya bora pengine mod anaweza kutusaidia
Mwalimu huyo, ambaye anafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, anasema, "Asikudanganye mtu, mazingira ya kazi ni magumu sana, ukweli nimeelemewa na mzigo wa vipindi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba bila ya kupata msaada wowote hata kutoka katika shule jirani,"anasimulia."
"Afadhali sana sasa nimetulia, lakini ungekuja hapa kati ya Januari 2009 na Septemba 2009, ungenionea huruma jinsi nilivyokuwa napata shida ya kuwafundisha watoto hawa
Hebu pigeni hesabu mshahara wake kwanza ni kiasi gani ukitilia maanani kuwa hata overtime hana!.... Halafu ukifikiria watu wa EPA, RADAR, na wahuni wengine chamani na serikalini unashindwa pata jibu.....Na ukiangalia kwa makini hao ndiyo wanaokula jasho la mtu kama huyu!Ukitaka maji yaliyo salama ni lazima ununue dumu moja kwa Sh 700 hadi Sh1,000 kutoka katika kisiwa kingine kilicho mbali.
Ukifikiria kuwa ni miaka karibu hamsini (50) baada ya uhuru unashindwa pata jibu kichwani, je mwalimu kama huyu, au watoto kama hawa uhuru umewasaidia vipi?... na bado mwalimu ukienda kufuata mshahara, lazima ufunge shule hadi urudi ndipo ufungue shule. Pengine hutumia hata wiki mbili."
Anzisha hapa hapa kwa haraka haraka,
SAIDI MWALIMU HAMISI, SAIDI SANINGA SHULE YA MSINGI!
Kwa kuanzia tunaweza kupata mchango wa haraka haraka wa kumnunulia mwalimu Hamisi baiskeli. Maana nimesoma kwamba huwa anatembea kwa miguu umbali wa kutwa nzima kufuata huduma za afya na mshahara!
Baiskeli ni shilingi ngapi jamani?