Mwalimu Hamisi ana moyo sana?

Halafu inatia hasira, lakini mwisho unakuja kuappreciate kuwa Mungu alikupendelea sana kupata bahati ya kufikia hapa ulipo hence kneel down and thank him please then lets find a way to help him guys
 
Acha kumpigia mbuzi gitaa....Angalia jinsi ya kumsaidia Mwalimu Hamisi kwanza ili asivunjike moyo wa kusomesha Watazania wenzetu. Serikali yetu ni sikio la kufa, halisikii dawa!

Umewahi mno soma post inayokufata 'Oysterbay' je wewe umekuja na idea gani ya kusaidia? ninachosema mimi wakina Hamisi wako wengi sana Tz hii
 
Umewahi mno soma post inayokufata 'Oysterbay' je wewe umekuja na idea gani ya kusaidia? ninachosema mimi wakina Hamisi wako wengi sana Tz hii

Nimekupata mkuu! Mimi nimependekeza JF iandae utaratibu wa kumsaidia Mwalimu Hamisi ili asivunjike moyo! Michango kidogo tu inaweza kumtatulia matatizo yake na kumtia nguvu kuendelea na moyo huo. Kumnunulia baiskeli ni mojawapo ya vitu vya kuanza navyo!
 
Hongera bwana Hamisi,hiyo kwako ni kama karama,kisikukatishe tamaa kitu chochote we sulubika kwakwenda mbele kama masia,malipo yapo mbinguni,hao ni wadogo zako,watoto zako na kadhalika,usiiache karama yako ipotee hivihivi!!
 
Shahada(degree)= 310,000; stashahada(dip.)=280,000; Cheti(certificate)= 120,000= Yawezekana ndio mshahara wa mwl Hamisi kama hajapandishwa daraja!!
Pia hii mishahara ni Gross sallary (haijakatwa kodi)!
Wewe waweza? Naamini huwezi! Sasa tumlaumu nani matokeo ya mitihani yanapokuwa mabaya?

hatuangalii chanzo cha tatizo tupo juu juu kama mwewe........am angry at myself!!!!

@sikonge nadhani wazo la kufundisha mwalimu kuvua ni zuri kulikoni kumpa samaki. lakini sasa hilo suluhisho linakidhi vipi tatizo la malimu na shule iliyotorokwa na waalimu??
mwisho wa siku hao watoto wetu hapa watakuwa wameipata hata hiyo elimu ya msingi kweli???
kweli Tanzania zaidi ya niijuavyo
 
This is terrible. Hii shule inatakiwa kuwa ya mfano. Walimu wanaokubali kuwa huko ndiyo wapandishwe vyeo kuwa maafisa elimu kila baada ya miaka 3-5 ya kazi. Nadhani itawapa walimu moyo wa kwenda huko. Ni pendekezo mojawapo ya jinsi ya kuongeza walimu katika shule za pembezoni.
 
Naweza kuchangia baiskeli ya huyu mwalimu ila sijui itamfikiaje? My Pledge
 
Wanasema ualimu ni kazi ya wito asiye nao aoende anakotaka! Halafu bado utasikia tumewapa ushindi wa kishindo-waendelee na ukiritimba. Mwe! Mbona maruweruwe na kizunguzungu kwa pamoja kuhusu sisi wa-Tanzania. Hatuna connection kabisa vichwani?

Kuna wakati Mh. waziri Simba alisema mfumo wa mawasiliano kichwani mwake umepata mushkeli; ikabidi atimkie sauzi kuuweka sawa. Pamoja na kwamba ulikuwa msamiati mpya kwangu, nadhani inabidi kama jamii tujichunguze vizuri. Vingineyo, akina Mwl. Hamisi wataendelea si kusota tu bali hata kukejeliwa na kusanifiwa kwa ajili yetu.
 
Hii ndio sera ya chama cha mapinduzi.Yaani hata enzi za mwl hakukuwa na hali kama hii shule nzima etiina mwl mmoja .
 
Hii ndio sera ya chama cha mapinduzi.Yaani hata enzi za mwl hakukuwa na hali kama hii shule nzima etiina mwl mmoja .

Unafikiri tatizo ni chama tu kweli? unafikiri chama kingine kinaweza kuwafanya walimu wakae huko?
 
Unafikiri tatizo ni chama tu kweli? unafikiri chama kingine kinaweza kuwafanya walimu wakae huko?

Nadhani ni political will.Mbona kwenye shule binafsi kuna walimu wa kumwaga?Je ni kweli kuwa Tanzania hakuna walimu wa kutosha? Hivi tukiamua seriously kuwatengenza mazingira mazuri,shule za serikali zaitakuwa hazina walimu?mbona wenzetu Uganda hili tatizo sio kubwa kama la kwetu?tena kwao govt schools ndio zinafanya vizuri?
 
Naweza kuchangia baiskeli ya huyu mwalimu ila sijui itamfikiaje? My Pledge

Tumain asante kwa moyo wa kujitolea.....jinsi ya kumfikia labda chanzo cha hii habari (ulipoitoa ) aweza kuwa msaada zaidi.
Ila zaidi ya baiskeli kama wengine walivoshauri labda tuone jinsi gani twaweza kumsaidi a mwalimu huyu (japo wakina Hamisi ni wengi Tz) lakini kwa kuanzia lets see how we cana help him out
aaaah pity!!!!
 
Tumain asante kwa moyo wa kujitolea.....jinsi ya kumfikia labda chanzo cha hii habari (ulipoitoa ) aweza kuwa msaada zaidi.
Ila zaidi ya baiskeli kama wengine walivoshauri labda tuone jinsi gani twaweza kumsaidi a mwalimu huyu (japo wakina Hamisi ni wengi Tz) lakini kwa kuanzia lets see how we cana help him out
aaaah pity!!!!

Chanzo ni gazeti la mwananchi (TZ) na mimi niko nje ya nchi...tushauriane namna ya bora pengine mod anaweza kutusaidia
 
Mwalimu huyo, ambaye anafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, anasema, "Asikudanganye mtu, mazingira ya kazi ni magumu sana, ukweli nimeelemewa na mzigo wa vipindi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba bila ya kupata msaada wowote hata kutoka katika shule jirani,"anasimulia."

Jamaa wa watu anatia huruma, ukifikiria kuwa kuna manunda dodoma ambayo mwaka mzima bungeni ni kutia mbonji (kulala), unatamani kwenda na kuwatia viboko tu!
"Afadhali sana sasa nimetulia, lakini ungekuja hapa kati ya Januari 2009 na Septemba 2009, ungenionea huruma jinsi nilivyokuwa napata shida ya kuwafundisha watoto hawa

Nashindwa kuelewa hiyo january-sept 2009 ilikuwaje kama yeye mwenyewe anasema hivi!

Ukitaka maji yaliyo salama ni lazima ununue dumu moja kwa Sh 700 hadi Sh1,000 kutoka katika kisiwa kingine kilicho mbali.
Hebu pigeni hesabu mshahara wake kwanza ni kiasi gani ukitilia maanani kuwa hata overtime hana!.... Halafu ukifikiria watu wa EPA, RADAR, na wahuni wengine chamani na serikalini unashindwa pata jibu.....Na ukiangalia kwa makini hao ndiyo wanaokula jasho la mtu kama huyu!
... na bado mwalimu ukienda kufuata mshahara, lazima ufunge shule hadi urudi ndipo ufungue shule. Pengine hutumia hata wiki mbili."
Ukifikiria kuwa ni miaka karibu hamsini (50) baada ya uhuru unashindwa pata jibu kichwani, je mwalimu kama huyu, au watoto kama hawa uhuru umewasaidia vipi?
 
Anzisha hapa hapa kwa haraka haraka,

SAIDI MWALIMU HAMISI, SAIDI SANINGA SHULE YA MSINGI!

Kwa kuanzia tunaweza kupata mchango wa haraka haraka wa kumnunulia mwalimu Hamisi baiskeli. Maana nimesoma kwamba huwa anatembea kwa miguu umbali wa kutwa nzima kufuata huduma za afya na mshahara!

Baiskeli ni shilingi ngapi jamani?

Tukiwa wepesi wa kuguswa na matatizo ya wengine kwa kiwango hiki inafurahisha sana, lakini serikari isibweteke. Kwa hiyo tukiamua kununua hiyo baiskeli kwa kuanzia, naamini haichukui wiki michango itakuwa tayari walau kumpa moyo mwl huyo shujaa na wengine waige mfano wake ili kizazi cha masikini wale kikombolewe kielimu.......... nina majonzi!!!

.................................................
Amani yetu inatumiwa vibaya
 
Na tusiishie hapo tu, yaani kunua baiskeli, tunaweza pia kutuma timu ya waangalizi wa JF ili kuona na kuchambua zaidi nini kifanyike kilicho chini ya uwezo wetu tufanyemaana kutoa ni moyo jamani . Yote yanawezekana kama tutajitolea.... Ahsante

..........................................
Amani yetu inatumiwa vibaya.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom