Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,705
- 36,157
Mwanangu alirudi nyumbani siku moja huku akiongea kusema "Ile shule siitaki , usiponihamisha siendi tena"
Imagine mtoto wa darasa la kwanza Mwalimu anamwadhibu kwa kumpigisha ukutani.
Hilo nikamtuma wife akaongee na mwalimu aliyefanya huo ujinga likaisha. That was January.
Maisha ya shule huyu mwanangu yanaendelea vizuri.
Majuzi kachapwa kwa kutokufanya zoezi na utoro huku mwanangu hana trend ya utoro. Ilikuwa mistake tu ya utoto aliandika zoezi karatasi ya nyuma badala ya mbele. Akiona uwazi kwenye daftari kwa nyuma huwa anatumia huo uwazi. Sasa mwalimu hakuona zoezi la jana na kuhesabu tu kuwa mtoto hajafanya kazi ya Jana.
Nimeongea na mwanangu kuwa asiandike nyuma sasa hata kama ameacha karatasi isiyo na maandishi.
Sasa hata ingekuwa ni kweli mtoto hajafika shule au alifika lakini hajaandika ni sahihi umchape?
Enzi hizi bado walimu wanaendelea kuchapa watoto?
Walimu mpaka kesho hawajui kuwa mabosi zao sio maafisa elimu, madiwani na ma DED bali wanafunzi.
Je, kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kumchapa boss wake?
Kama watoto ni wasumbufu hiyo haiwapi uhalali wa kuwachapa watoto ni aina ya maboss waliowachagua , wawahudumie vivyo hivyo.
Shule za serikali zinaongoza kwa kuzalisha watoto vilaza kwakuwa walimu hawajagundua kuwa wanafunzi ndio maboss wao.
Wanafunzi na walimu ni kama maadui.