Mwakyembe amtaja waziwazi Rostam Aziz!

Ujasiri ni kuongelea kwenye Kamati Kuu ya CCM? Hiyo taarifa anayo toka alipoketi kama Mwenyekiti wa Kamati ile! Alikuwa anaijua kabla ya hukumu kutolewa! Akapewa na uwaziri kama zawadi! Akaukubali na anaendelea nao! Sasa hivi Rostam akijiuzulu uchaguzi katika jimbo lake utarudiwa fedha ya kodi itatumika bado ametusaidia? Mbona hakusema kabla ya uchaguzi wananchi wajue? Au anasaidia chama kwanza then watanganyika?

Na Mwakyembe anajua, Raisi hajui? Siku zote hajamwambia? Kama amemwambia na Raisi amekaa kimya ametusaidiaje? Kama hajamwambia kwa nini?

Lazima tujiulize sana katika hili jambo na kupata majibu sahihi! Tukikurupuka tutabaki washabiki kama ilivyokuwa kipindi cha kujiuzulu kwa EL!

Bora yeye kuliko wewe uliempiga mtu RISASI pale Pub Alberto Moshi na kutumia taaluma yako ya kuwa mwanansheria na kufahamiana na wanasheria mkamaliza kesi kihuni, yule uliempiga risasi ni kaka yangu toka nitoke, najua wewe ni diwani wa pasua moshi Mungu atatulipia haki yetu kama familia
 
Twendeni bara barani jamani ....Tunisia washamaliza kazi....lebanoni mziki unaendelea na sasa ngoma inakesha Egypt.
 
Vigogo wapasua jipu la Dowans

Na Waandishi wetu 26th January 2011

headline_bullet.jpg
Wamtaja mmiliki wake kavu kavu
headline_bullet.jpg
Ombi la kukaza hukumu latua mahakamani

[FONT=ArialMT, sans-serif]Ile sinema ya Dowans imeingia sura mpya, safari hii wabunge wameamua kumlipua mwenzao kuwa ndiye mmiliki wa kampuni hiyo ambayo imezua mtafaruku mkubwa nchini baada ya kushinda kesi ya kutaka ilipwe fidia ya Sh. bilioni 94 na Tanesco.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati ya wabunge CCM kilichomalizika juzi, zinasema kuwa walau wabunge watatu ndani ya kikao hicho, walimnyooshea moja kwa moja kidole, Mbunge mwenzao kuwa ndiye mmiliki wa Dowans.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dowans Tanzania Limited ilirithi mkataba tata wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ambao kampuni ‘hewa' ya Richmond Development Corporation iliingia na Tanesco Juni 23, mwaka 2006, kufua umeme wa dharura wa megawati 100 kwa kutumia gesi asilia.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dowans ilifungua kesi dhidi ya Tanesco katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) ambayo hukumu yake iliiamuru Tanesco kulipa faini ya Sh. bilioni 94 kwa kukatisha mkataba huo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa kutoka ndani ya kikao cha wabunge hao kilichofanyika juzi usiku jijini Dar es Salaam, ilisema wabunge hao walimtaja mwenzao baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, kuwasilisha taarifa ya Tanesco dhidi ya hukumu ya ICC.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, wanasheria waliosoma hukumu ya kesi hiyo wamedhihirisha wazi kuwa, mmiliki halali wa Dowans ni mbunge huyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa zinaeleza kuwa, hukumu hiyo yenye kurasa 211 tayari imenyofolewa kurasa nne, ambayo imeelezwa kwamba iwapo itawekwa hadharani, ushahidi wake unadhihirisha wazi kuwa ni mmiliki wake na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyeileta kampuni ya Richmond.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chanzo chetu ndani ya CCM kimeeleza kwamba, wabunge waliosimama kumlipua mwenzao, walikuwa na nakala ya hukumu ya ICC na kuweka bayana ushahidi wa mmoja wa waliokuwa mashahidi wa Tanesco katika mahakama hiyo ambaye ni Meneja wa Net Group Solutions kwamba alilazimishwa kusaini makubaliano ya kuhamisha mkataba wa Richmond kwa Dowans.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa chanzo hicho, meneja huyo aliieleza ICC kwamba majadiliano ya kuhamisha mkataba wa Richmond kwenda Dowans yalifanyika nje ya Tanesco kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chanzo hicho kilinukuu sehemu ya ushahidi wa Meneja wa Net Group Solutions katika hukumu ya ICC ikisema kwamba, asiposaini chochote kinaweza kumtokea, shinikizo alililodai alipewa na mbunge huyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, aliungana na wabunge wenzake kupinga malipo ya Dowans na kueleza kuwa, kampuni yake ya uwakili itajitolea kusimamia kesi kwa niaba ya serikali kuhakikisha Dowans hailipwi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Baada ya wabunge hao kuchachamaa, Kamati ya wabunge wote wa CCM walipitisha azimio kuitaka serikali isilipe kampuni ya Dowans, jambo ambalo liliridhiwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, katika kikao hicho, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amepewa jukumu la kuwa msemaji wa serikali kuhusu suala la Dowans ili kuepusha mpasuko ndani ya chama na serikalini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika hatua nyingine, Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Samuel Sitta, amesema leo atawasilisha malalamiko yake kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) dhidi ya baadhi ya magazeti aliyodai yanatumika kumchafua.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Sishangai kuchafuliwa na kampuni ya … kwa sababu mmiliki wake ndiye mmiliki wa Dowans, mimi kusimamia maslahi ya umma dhidi ya Dowans lazima nimkere mmiliki wa magazeti hayo kwa sababu ndiye atakayenufaika na malipo ya bilioni 94 ambayo baadhi yetu tunaona sio haki," alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, alisema msimamo wake upo wazi ndio maana amekuwa akiandamwa na baadhi vyombo vya habari na waandishi wanaotumika kumchafua.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, mbunge huyo jana hakuwepo katika semina ya Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano iliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]WAKILI KUKAZA HUKUMU [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo huo, wakili mmoja wa kujitegemea, amedaiwa kuwasilisha maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka kukazwa kwa hukumu ya ICC dhidi ya Tanesco.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakali huyo anadaiwa kuwasilisha maombi hayo, jana kwa niaba ya Dowans ambayo inapambana kulipwa kititia cha Sh. bilioni 94.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwanasheria huyo jana alifika mahakamani hapo na kuwasilisha maombi yake, ingawa haijafahamika kama alipewa namba ya kesi.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Ni kweli (jina linasitiriwa)… leo (jana) amewasilisha maombi yake, lakini siwezi kukupa taarifa zaidi kwani mimi sio msemaji wake na hajipangiwa jaji," kilisema chanzo hicho.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa hukumu ya ICC juu ya kesi ya Dowans dhidi ya Tanesco iliyowasilishwa mahakamani hapo ilikuwa ni viambatanisho tu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa mkataba wa Dowans na Tanesco na sheria ya kimataifa ya mikataba, ili hukumu ya ICC iwe na nguvu kisheria ni lazima isajiliwe mahakama kuu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Imeandikwa na Restuta James, Romana Mallya na Hellen Mwango.[/FONT]
 
Inabidi twende Rwanda tukamkodishe H.E Kagame atusaidie kuwajibisha mafisadi wote. Yule haangalii mtu machoni. Kwa style ya viongozi wetu Tz ni kulindana tu. Hata iweje. Tofauti na hapa tukubali Dr. Slaa aongoze nchi kwa kipindi kimoja tu amalizane kwanza na wala nchi tu. Tumechoka.
 
Inabidi twende Rwanda tukamkodishe H.E Kagame atusaidie kuwajibisha mafisadi wote. Yule haangalii mtu machoni. Kwa style ya viongozi wetu Tz ni kulindana tu. Hata iweje. Tofauti na hapa tukubali Dr. Slaa aongoze nchi kwa kipindi kimoja tu amalizane kwanza na wala nchi tu. Tumechoka.
Unajua kwamba Kagame hana tofauti. Kwanza wapinzani wake wote wakati wa uchaguzi walikua wametokea kundi moja sema kwa sababu ya uchaguzi ilibidi ionekane kwamba ana upinzani lakini wapi? So sijui kama Kagame atafaa.
 
Wabongo bana, sometimes tunakritisaizi unconstructively kabisaa. Haya ni mambo yametokea juzi tu 2008 tayari historia imeanza kupindishwa.

1. Hivi aliyetuambia kwamba kampuni ya Richmond ilikuwa ikitumia same address na ile ya Caspian ni nani?

2. Aliyetuambia kwamba walimwita Rostam kwa mahojiano akatoa udhuru tena si mara moja ni nani?

I am not saying Mwakyembe ni mtimilifu or whateva of that sort lakini at least katika CCM kwa standards za ki-CCM ameonyesha ujasiri na si mara moja kwenye suala hili. Na hii ya kusema kazi yake ni kutaja tu, nadhani ni kuwakwepeshea makusudi wenye majukumu yanayofuata baada ya hapo. TAKUKURU, DPP na mahakama.

Nyambala badala ya wewe kupindishia pia ungeendelea kutujuza ni nani aliyesema kuwa kuna vitu wameficha? Ni nani ambaye aliomba mjadala wa Richmond urudi upya ili watoboe siri?

Mimi sijasema kwamba Mwakyembe ni mchafu, ninachoquestion ni hicho kitu wanachokisema ni ushujaa wa kusema. Kwanza hataki kutoka CCM, pili kuna vitu alivificha. Soma hii article kama nilivyoitoa kwenye mwananchi.


Watanzania hatujaambiwa ukweli wote kuhusu Richmond/Dowans Send to a friend Tuesday, 25 January 2011 19:51 0diggsdigg

George Maziku

NAANDIKA makala haya kwa lengo la kusimamia ukweli na kuweka kumbukumbu sawa, nataka kurekebisha tabia tuliyojijengea Watanzania ya kuwalaumu na kuwashutumu watu kwa kutumia taarifa nusu-nusu, taarifa zisizo na ukweli kamili, taarifa za kuungaunga tu, na wakati mwingine tunawaacha wahusika halisi bila kuwabebesha msalaba wao.

Wakati wote wa sakata hili la Richmond na Dowans, Watanzania tumekuwa tukiwashambulia watu wawili tu, Lowassa na Rostam, tukiwatuhumu na kuwahukumu kuwa wao ndio vinara wa sakata hili, kwamba wao ndio wahusika wakuu wa kashfa hii ya kihistoria katika nchi yetu, kwamba wao ndio wamiliki wa makampuni haya ambayo sasa yanayoligharimu mabilioni taifa letu.

Waliosababisha tuamini hivyo ni wanasiasa na wanahabari ambao wakati wote wamekuwa wakitushawishi Watanzania tuamini kuwa Lowassa na Rostam ndio "wezi" wetu, kwamba hawa ndio waliosuka njama za kukwapua mabilioni yetu kupitia mradi wa dharura wa kufua umeme.

Kwa mfano, iliyokuwa Kamati ya Bunge ya kuchunguza mkataba kati ya serikali na Richmond iliyoongozwa na mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, maarufu kama kamati ya Mwakyembe, iliyotoa ripoti ikiwatuhumu wanasiasa hawa wawili kuwa nyuma ya kashifa hii.

Kwa upande wetu wanahabari kwa muda mrefu tumekuwa tukiandika taarifa kwa kuzirudia rudia tukiwahukumu moja kwa moja Lowassa na Rostam kama wamiliki wa Richmond na Dowans, na kwa maana hiyo wamekula njama za kutuibia.

Binafsi msimamo wangu umekuwa wazi kabisa tangu mwanzo, kwamba Watanzania hatujaambiwa ukweli wote kuhusu suala hili, tumefichwa habari muhimu na nzito kuliko hizi tunazozisikia, tumelishwa taarifa zitokanazo na chuki binafsi za kisiasa na pengine kibiashara.

Kwa mfano, Kamati ya Mwakyembe ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa mbunge huyo wa Kyela ambaye sasa ni Naibu waziri wa ujenzi, haikusema ukweli wote, ilituficha ukweli halisi wa sakata hilo, kwa ufupi kamati ile iliamua kwa makusudi kumlinda mtu aliyestahili kubeba lawama zote, mtu aliyestahili kusulubiwa.

Kamati ya Mwakyembe haikusema ukweli kuhusu nafasi ya rais Jakaya Kikwete katika mchakato mzima wa kuipatia mkataba wa kufua umeme wa dharura kampuni ya kitapeli ya Richmond, na hata katika uamuzi wa baadaye wa kuhamisha kinyemela mkataba huo kwenda kwa Dowans.

Yapo maelezo na nyaraka zinazothibitisha kuwa rais Kikwete alikuwa msimamizi mkuu wa mchakato ulioipatia Richmond zabuni ile, alikuwa akitoa maagizo na maelekezo mbalimbali kwa aliyekuwa waziri mkuu wake, Lowassa na alikuwa mwamuzi wa mwisho wa uamuzi wowote uliofikiwa wakati huo.

Kwa msingi huo, kuwatwisha zigo la lawama aliyekuwa waziri mkuu Lowassa, mawaziri wa zamani wa nishati na madini Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi bila maelezo ya kina na yenye mashiko na ushahidi madhubuti, ni uonevu na upotoshaji wa ukweli halisi wa sakata hilo.

Ni kweli Lowassa, Karamagi na Dk Msabaha walihusika kutokana na nyadhifa zao serikalini, lakini hawakuwa waamuzi wa mwisho wa suala hili, walikuwa wakitekeleza maagizo ya juu, kulikuwa na mtu mzito kuliko wao aliyekuwa na maamuzi ya mwisho, huyu ndiye anayestahili kulaumiwa na kuhukumiwa kwa yote yaliyotokea baadaye.

Lakini kwa sababu ambazo haziko wazi, Kamati ya Mwakyembe haikuhoji kabisa nafasi ya rais Kikwete katika sakata hili, waliamua kumlinda Rais, hata aliyekuwa Spika wa Bunge wakati ule, Samuel Sitta hakujihangaisha kuutafuta ukweli uliofichwa na Kamati ya Mwakyembe, hata kambi ya upinzani bungeni haikuhoji suala hilo, na hata wananchi hatujahoji hilo.

Kwa upande wa Rostam, yeye amekiri kuileta nchini kampuni ya Dowans iliyonunua mkataba wa Richmond, lakini yeye amesema alifanya hivyo baada ya kuombwa "kuwaokoa" wakubwa waliokuwa "wamebanwa mbavu" baada ya kubumbuluka kwa "dili" lao la Richmond.

Sasa kwa nini yeye abebeshwe lawama zote? Kwanini ahukumiwe kwa kosa lisilo lake? Rostam hakuiba, yeye kosa lake ni kuwasaidia wezi kuficha mali ya wizi, tumhukumu kwa hilo, lakini si kwa kosa la wizi, tuwatafute wezi wetu na tuwahukumu kwa madhambi yao. Source: Mwananchi
 
Bora yeye kuliko wewe uliempiga mtu RISASI pale Pub Alberto Moshi na kutumia taaluma yako ya kuwa mwanansheria na kufahamiana na wanasheria mkamaliza kesi kihuni, yule uliempiga risasi ni kaka yangu toka nitoke, najua wewe ni diwani wa pasua moshi Mungu atatulipia haki yetu kama familia
Hayo maneno unaweza kuyasimamia siku zijazo au ni ya leo tu.
 
Suala la Dowans lilijitokeza juzi jumatatu wakati kamati ya wabunge wa CCM iliyoketi Dar es Salaam, nimefurahishwa na hii nukuu jinsi alivyozungumza Mwakyembe: "Mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu: anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi"

Source: Mwana Halisi Janaury 26-Feb 1, 2011 Ukurasa wa pili paragrafu ya 22

Hivi kwenye mapendekezo ya Kamati ya Richmond walishauri ROSTAM achukuliwe hatua gani? Je ROSTAM AZIZ alitajwa kama mmoja wa wahusika kwenye ile kashfa au ndio wale ambao majina yao yalifichwa kwa makusudi na kamati ya Mwakyembe ili kulinda heshima ya serikali?
 
Suala la Dowans lilijitokeza juzi jumatatu wakati kamati ya wabunge wa CCM iliyoketi Dar es Salaam, nimefurahishwa na hii nukuu jinsi alivyozungumza Mwakyembe: "Mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu: anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi"

Source: Mwana Halisi Janaury 26-Feb 1, 2011 Ukurasa wa pili paragrafu ya 22

Imetulia!

Tegemeo pekee sasa ni Wapiganaji wa ndani ya CCM Mwakyembe na Six . . .

I can clearly see in worst cases wanaweza wakaachia na ngazi kama CCM wakijifanya Kichwa ngumu!

Get Up Stand Up Kamanda!
 
hana lolote Mwakyembe...mi sijamuona kama kuna la maana analoongea kama anakerwa na haya why sasa anaendelea kuwa miongoni mwao huko CCM...
Sasa angekuwa nje wangepataje ujumbe huo, maana wengine wakiambiwa Serikali italipa DOWANS hawaulizi bali wanamshangilia mwenyekiti etc .
 
Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati ya wabunge CCM kilichomalizika juzi, zinasema kuwa walau wabunge watatu ndani ya kikao hicho, walimnyooshea moja kwa moja kidole, Mbunge mwenzao kuwa ndiye mmiliki wa Dowans.
[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, wanasheria waliosoma hukumu ya kesi hiyo wamedhihirisha wazi kuwa, mmiliki halali wa Dowans ni mbunge huyo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa zinaeleza kuwa, hukumu hiyo yenye kurasa 211 tayari imenyofolewa kurasa nne, ambayo imeelezwa kwamba iwapo itawekwa hadharani, ushahidi wake unadhihirisha wazi kuwa ni mmiliki wake na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyeileta kampuni ya Richmond.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa chanzo hicho, meneja huyo(wa Net Group Solutions) aliieleza ICC kwamba majadiliano ya kuhamisha mkataba wa Richmond kwenda Dowans yalifanyika nje ya Tanesco kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Chanzo hicho kilinukuu sehemu ya ushahidi wa Meneja wa Net Group Solutions katika hukumu ya ICC ikisema kwamba, asiposaini chochote kinaweza kumtokea, shinikizo alililodai alipewa na mbunge huyo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika hatua nyingine, Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Samuel Sitta, amesema leo atawasilisha malalamiko yake kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) dhidi ya baadhi ya magazeti aliyodai yanatumika kumchafua.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Sishangai kuchafuliwa na kampuni ya … kwa sababu mmiliki wake ndiye mmiliki wa Dowans, [/FONT]

Maneno makubwa hayooooooooooooo!!!!!!!!!!!! jamani, usiposaini lolote linaweza kukutokea sio mimi ni yule mbunge, na ni nani amenyofoa hizo kurasa nne, huyo ndiye wa kufa naye je ni Mwanasheria mkuu, Ngeleja au Pinda?
 
Anaendelea kuwepo.......je kazi yake itakuwa kuyutajia wezi tu?

Kulaumu ni rahisi, kila mtu anaweza. Lakini, tusisahau kuwa utamaduni wa kuwa wazi (openness) ndio unaanza ku-evolve Tz. Tumedumu katika hali ya woga na kulindana kama ndugu au wajamaa kwa muda mrefu. Wakati wa nyuma makosa yalikuwepo lakini si makubwa sana na yalivumilika na kustahili kulindana. Hata hivyo uongozi wa juu wa nchi ulikuwa na mikono safi na ulikuwa ukichukua hatua za kuwajibisha viongozi mafisadi. Hivyo alichofanya Mh Mwakyembe ilikuwa kutoa ukweli huku akionesha staha kwa viongozi.

Lakini pia tusisahahu kuwa Dr Mwakyembe si rais wa nchi, hivyo kwa kutoa ukweli alioutoa alimsaidia rais kuchukua hatua. Dr Mwakyembe alimbakishia Rais heshima na madaraka ya kutenda. Hata ungekuwa wewe hali hiyo ingekutawala.

Kwa hivi sasa tushukuru changes are taking place, watu wanaanza kusimama kidete kusema ukweli na believe me Tz has changed for ever. Anayejiandaa kuwa rais katika miaka ijayo asitegemee mteremko kama akina che Mkapa na udikteta wake, au kina Dr Kikwete na Dowans zao.

Dr Mwakyemebe na Mh S. Sitta wanahitaji pongezi na si lazima wajitoe kwenye madaraka au chama chao cha CCM baada ya kutofautiana na serikali na Chama. Mchakato bado unaendelea, saa ya kubakia au kujitoa CCM itafika - watafanya maamuzi magumu.
 
siku zote RA anatuhumiwa kumiliki DOWANS.... mbona hajatokea na vielelezo vinavyoonyesha wamiliki halali wa DOWANS ili awe amejisafisha.... vinginevyo hii kampuni ya DOWANS Tanzania ni ya kwake..... hakuna ubishi hapa
 
Hapo Kalamu umesema kweli kabisa.
Mwakyembe alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa Richmond, angetuletea hilo alilosema sasa moja kwa moja badala ya kuzunguka mbuyu tusingekuwa tumefika hapa. Wao wenyewe walisema kuna vitu wameficha ili kuisaidia serikali sasa Rostam ni serikali?

Unataka Mwakyembe asema nini zaidi ya haya?

"Lakini Mhe. Dk. Msabaha (Mb), baada ya mahojiano chini ya kiapo, akaniuma sikio Kamati Teule kuwa katika suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu au, kwa maneno yake mwenyewe, “Bangusilo” kwa lugha ya Kizaramo. Maelezo hayo ya ziada nje ya kiapo ya Mheshimiwa Waziri yaliyotoa ujumbe kuwa “si yeye ila mkuu wake wa kazi”, yalioana na maelezo aliyoyatoa Balozi Kazaura nje ya kiapo tarehe 30 Novemba, 2007. Mara baada ya kumaliza mahojiano kwa kiapo na Kamati Teule, Balozi akatoa maelezo ya ziada kuwa Richmond ilikuwa mradi wa “Bwana Mkubwa” na “mshiriki wake mkubwa kibiashara”, akimaanisha Mhe. Waziri Mkuu na Mhe. Rostam Aziz (Mb).

[FONT=Trebuchet MS, sans-serif]Kamati Teule ilikuwa imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7 waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.[/FONT]


...
 
siku zote RA anatuhumiwa kumiliki DOWANS.... mbona hajatokea na vielelezo vinavyoonyesha wamiliki halali wa DOWANS ili awe amejisafisha.... vinginevyo hii kampuni ya DOWANS Tanzania ni ya kwake..... hakuna ubishi hapa
kuna vitu huwa anavijibu haraka sana lakini si RichMond na Dowans
 
Tusikomee kuongea peke yake tuchukue hatua. Inabidi yaandaliwe maandamano ya kumtaka Rais awawajibishe wale wote waliohusika kwenye sakata la Dowans/Richmond akishindwa aachie ngazi

Maandamano yamtake Rais Kikwete awajibike yeye na Serikali yake yote sio kuwajibisha watu kwani madudu haya yakitokea yeye alikuwa wapi asiyaone na kama aliyaona na kuyajua alichukua hatua gani.Kwa kukaa kwake kimya inaonyesha kuwa anayajua madudu haya na ni mshiriki wa karibu kuwaibia watanzania hivyo awajibike yeye kwanza na serikali yake yote.
 
Back
Top Bottom