Mwakyembe amtaja waziwazi Rostam Aziz!

Likes of Mwakyembe wanapambana katika capacity zao, SWALI KUBWA TUJIULIZE " JE SISI WANANCHI HASA WADANGANYIKA TUMEFANYA NINI KATIKA HILI?". Kazi yetu ni kununua magazeti kusoma na kukaa kimya, ati ngoja tuone nn kitatokea. Tumeona wenzetu Tunisia, na sasa Misri nn kinachotakiwa kufanya.
 
yaani inauma sana na nasikia tayari wanakamilisaha aiport near the boader. TUSAHAU ICOME YA WATALII sie tuna bwabwaja tuuuuuu (especially viongozi hawaoni mbele hata mita mia)
Kwa mtazamo wako tunyamaze tu ili mafisadi wafanye watakavyo?Tutaendelea kubwabwaja mpaka watuelewe.
 
Suala la Dowans lilijitokeza juzi jumatatu wakati kamati ya wabunge wa CCM iliyoketi Dar es Salaam, nimefurahishwa na hii nukuu jinsi alivyozungumza Mwakyembe: "Mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu: anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi"

Source: Mwana Halisi Janaury 26-Feb 1, 2011 Ukurasa wa pili paragrafu ya 22
PHP:
sasa sebene limefikia chorus
Hapa patamu, wakati wenyewe wanapigana sisi tunapanga njia ya kwenda magogoni!!!
 
hana lolote Mwakyembe...mi sijamuona kama kuna la maana analoongea kama anakerwa na haya why sasa anaendelea kuwa miongoni mwao huko CCM...

Unaweza usielewe, huo ni ujasiri usio kawaida katika nchi hii inayoendeshwa ki-mafia huku wanasiasa na watendaji wengi wakijali zaidi mustakabali na maslahi yao kwa kushika miguu ya ma-don.
 
Maandamano yamtake Rais Kikwete awajibike yeye na Serikali yake yote sio kuwajibisha watu kwani madudu haya yakitokea yeye alikuwa wapi asiyaone na kama aliyaona na kuyajua alichukua hatua gani.Kwa kukaa kwake kimya inaonyesha kuwa anayajua madudu haya na ni mshiriki wa karibu kuwaibia watanzania hivyo awajibike yeye kwanza na serikali yake yote.

Hii ndio inayotakiwa. Kikwete & Co needs to pack and go! Ameshindwa kazi.
 
Wakuu,

Nanona moto umewaka Egypt pia!!! Tunisia wamefungua njia...

Vipi sisi si tuchukue hatua, haya mambo hayatapita bila kujitoa!!!
 
hana lolote Mwakyembe...mi sijamuona kama kuna la maana analoongea kama anakerwa na haya why sasa anaendelea kuwa miongoni mwao huko CCM...

Kalamu daftari sio kila changes uzifanye ukiwa nje. Unaweza ukawa humohumo lakini ukaleta changes. Mfano kama mkeo anakojoa kitandani, kumtibu na kumrekebisha ndani kwa ndani, saa nyingine si busara kutoka nje ukasema mke wangu kikojozi. Sasa mbona vyama vyote kuna uozo wake ndani?

Kwa hiyo anayepingana na wengine ndani ya Chadema atoke chadema aje Nccr, na hukohuko ikiwa hivyo aende tlp? sasa ataishia wapi. Siku zote ukimuudhi mtu ni wajibu wa yule uliyemuudhi kuonesha hasira zake hata kama ni kukuadhibu, hivyo CCM WAMUADHIBU Mwakyembe sababu anawaudhi , sio yeye ajiadhibu, yeye hana familia? hataki kusomesha watoto?

Wewe acha aseme akiwahapo hapo ili waone aibu maana akiwa nje yao watasema muongo. Acha aoneshe maovu ili walioko nje kama unavyofikiri wewe wapate pa kuanzia.
 
Suala la Dowans lilijitokeza juzi jumatatu wakati kamati ya wabunge wa CCM iliyoketi Dar es Salaam, nimefurahishwa na hii nukuu jinsi alivyozungumza Mwakyembe: "Mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu: anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi"

Source: Mwana Halisi Janaury 26-Feb 1, 2011 Ukurasa wa pili paragrafu ya 22

Kumbe source ni mwana halisi , iko hivi : MWANAHALISI = KUBENEA=CHADEMA, jibu tosha !
 
Ok. Baada ya kumtaja RA kuwa ndiye KINARA, nini kiliendelea??? kuna mwenye taarifa zozote??
 
Kumbe source ni mwana halisi , iko hivi : MWANAHALISI = KUBENEA=CHADEMA, jibu tosha !

sasa na wewe umekuwaje? kwa hiyo Mwakyembe hakuyasema? Sioni reasonable linkagea kati ya mada na mwanahalisi - kubenea - na chadema issue ni nauliza kubenea kazusha hakuyasema? Watu wengine bana.........walizaliwa wabishi tuuuuuuu hata kwenye facts, ahaaaaghhhh. KUmbe ni kweli Criminals are Born.
 
Kumbe source ni mwana halisi , iko hivi : MWANAHALISI = KUBENEA=CHADEMA, jibu tosha !

Ndio walewale, watu wakiongelea ukweli kazi ni kulalalmika yunaonewa
na myakuja kwa gear ya udini, ukabila, ukanda, rangi ili mraidi uwe tofauti

hapa kuna tatizo na wewe ujaribu kuangalia hili tatizo kiupana, hizo bilionis za kuwalipa Dowans zingesaidia sana maendeleo ya nchi hii
 
Ujasiri ni kuongelea kwenye Kamati Kuu ya CCM? Hiyo taarifa anayo toka alipoketi kama Mwenyekiti wa Kamati ile! Alikuwa anaijua kabla ya hukumu kutolewa! Akapewa na uwaziri kama zawadi! Akaukubali na anaendelea nao! Sasa hivi Rostam akijiuzulu uchaguzi katika jimbo lake utarudiwa fedha ya kodi itatumika bado ametusaidia? Mbona hakusema kabla ya uchaguzi wananchi wajue? Au anasaidia chama kwanza then watanganyika?

Na Mwakyembe anajua, Raisi hajui? Siku zote hajamwambia? Kama amemwambia na Raisi amekaa kimya ametusaidiaje? Kama hajamwambia kwa nini?

Lazima tujiulize sana katika hili jambo na kupata majibu sahihi! Tukikurupuka tutabaki washabiki kama ilivyokuwa kipindi cha kujiuzulu kwa EL!

Hao akina Sitta na Mwakyembe hata wakiongea kuhusu usanii wa Richmond/Dowans ndani ya Kamati Kuu ya CCM ni poa tu, nawapa big-up. Vipi kuh wajumbe wasioongea au wanaoitetea hiyo kampuni hewa ya kisanii?
Wengi hata humo kwenye vikao wanaujua ukweli ila hawana UJASIRI wa kuongea. Bravo Sitta & Mwakyembe.

Si lazima muwe mtu wa kusema 'ndiyo mzee' ndipo ukubali kuwa Waziri. Hawa wanatuonyesha kuwa unaweza kukubali kuwa Waziri na ukabaki na misimamo na maadili yako, hasa ya kutetea Taifa.

Pia si lazima kuhama chama chao. Wao ni wapambanaji, wanapambana wakiwa popote pale walipo hata ndani ya chama chao kinachoelekea kumezwa na mafisadi.
 
Is this news, mwakyembe tunajua bifu yake inatokana na nini? na yeye anataka kajirichmond kake na tanesco period! boring
 
Mnamwandama Rostam Azziz kwa sababu ni Mu-Islaam.

Shame on you Wakristo mkiongozwa na Mwakyembe, Samuel Sitta, Slaa, Mbowe, Lema, na genge zima la Wakristo. Mwataka wengine wale wapi?
 
Back
Top Bottom