Mwakyembe amtaja waziwazi Rostam Aziz!

Nyambala badala ya wewe kupindishia pia ungeendelea kutujuza ni nani aliyesema kuwa kuna vitu wameficha? Ni nani ambaye aliomba mjadala wa Richmond urudi upya ili watoboe siri?

Mimi sijasema kwamba Mwakyembe ni mchafu, ninachoquestion ni hicho kitu wanachokisema ni ushujaa wa kusema. Kwanza hataki kutoka CCM, pili kuna vitu alivificha. Soma hii article kama nilivyoitoa kwenye mwananchi.

Watanzania hatujaambiwa ukweli wote kuhusu Richmond/Dowans Send to a friend Tuesday, 25 January 2011 19:51 0diggsdigg

George Maziku

NAANDIKA makala haya kwa lengo la kusimamia ukweli na kuweka kumbukumbu sawa, nataka kurekebisha tabia tuliyojijengea Watanzania ya kuwalaumu na kuwashutumu watu kwa kutumia taarifa nusu-nusu, taarifa zisizo na ukweli kamili, taarifa za kuungaunga tu, na wakati mwingine tunawaacha wahusika halisi bila kuwabebesha msalaba wao.

Wakati wote wa sakata hili la Richmond na Dowans, Watanzania tumekuwa tukiwashambulia watu wawili tu, Lowassa na Rostam, tukiwatuhumu na kuwahukumu kuwa wao ndio vinara wa sakata hili, kwamba wao ndio wahusika wakuu wa kashfa hii ya kihistoria katika nchi yetu, kwamba wao ndio wamiliki wa makampuni haya ambayo sasa yanayoligharimu mabilioni taifa letu.

Waliosababisha tuamini hivyo ni wanasiasa na wanahabari ambao wakati wote wamekuwa wakitushawishi Watanzania tuamini kuwa Lowassa na Rostam ndio "wezi" wetu, kwamba hawa ndio waliosuka njama za kukwapua mabilioni yetu kupitia mradi wa dharura wa kufua umeme.

Kwa mfano, iliyokuwa Kamati ya Bunge ya kuchunguza mkataba kati ya serikali na Richmond iliyoongozwa na mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, maarufu kama kamati ya Mwakyembe, iliyotoa ripoti ikiwatuhumu wanasiasa hawa wawili kuwa nyuma ya kashifa hii.

Kwa upande wetu wanahabari kwa muda mrefu tumekuwa tukiandika taarifa kwa kuzirudia rudia tukiwahukumu moja kwa moja Lowassa na Rostam kama wamiliki wa Richmond na Dowans, na kwa maana hiyo wamekula njama za kutuibia.

Binafsi msimamo wangu umekuwa wazi kabisa tangu mwanzo, kwamba Watanzania hatujaambiwa ukweli wote kuhusu suala hili, tumefichwa habari muhimu na nzito kuliko hizi tunazozisikia, tumelishwa taarifa zitokanazo na chuki binafsi za kisiasa na pengine kibiashara.

Kwa mfano, Kamati ya Mwakyembe ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa mbunge huyo wa Kyela ambaye sasa ni Naibu waziri wa ujenzi, haikusema ukweli wote, ilituficha ukweli halisi wa sakata hilo, kwa ufupi kamati ile iliamua kwa makusudi kumlinda mtu aliyestahili kubeba lawama zote, mtu aliyestahili kusulubiwa.

Kamati ya Mwakyembe haikusema ukweli kuhusu nafasi ya rais Jakaya Kikwete katika mchakato mzima wa kuipatia mkataba wa kufua umeme wa dharura kampuni ya kitapeli ya Richmond, na hata katika uamuzi wa baadaye wa kuhamisha kinyemela mkataba huo kwenda kwa Dowans.

Yapo maelezo na nyaraka zinazothibitisha kuwa rais Kikwete alikuwa msimamizi mkuu wa mchakato ulioipatia Richmond zabuni ile, alikuwa akitoa maagizo na maelekezo mbalimbali kwa aliyekuwa waziri mkuu wake, Lowassa na alikuwa mwamuzi wa mwisho wa uamuzi wowote uliofikiwa wakati huo.

Kwa msingi huo, kuwatwisha zigo la lawama aliyekuwa waziri mkuu Lowassa, mawaziri wa zamani wa nishati na madini Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi bila maelezo ya kina na yenye mashiko na ushahidi madhubuti, ni uonevu na upotoshaji wa ukweli halisi wa sakata hilo.

Ni kweli Lowassa, Karamagi na Dk Msabaha walihusika kutokana na nyadhifa zao serikalini, lakini hawakuwa waamuzi wa mwisho wa suala hili, walikuwa wakitekeleza maagizo ya juu, kulikuwa na mtu mzito kuliko wao aliyekuwa na maamuzi ya mwisho, huyu ndiye anayestahili kulaumiwa na kuhukumiwa kwa yote yaliyotokea baadaye.

Lakini kwa sababu ambazo haziko wazi, Kamati ya Mwakyembe haikuhoji kabisa nafasi ya rais Kikwete katika sakata hili, waliamua kumlinda Rais, hata aliyekuwa Spika wa Bunge wakati ule, Samuel Sitta hakujihangaisha kuutafuta ukweli uliofichwa na Kamati ya Mwakyembe, hata kambi ya upinzani bungeni haikuhoji suala hilo, na hata wananchi hatujahoji hilo.

Kwa upande wa Rostam, yeye amekiri kuileta nchini kampuni ya Dowans iliyonunua mkataba wa Richmond, lakini yeye amesema alifanya hivyo baada ya kuombwa "kuwaokoa" wakubwa waliokuwa "wamebanwa mbavu" baada ya kubumbuluka kwa "dili" lao la Richmond.

Sasa kwa nini yeye abebeshwe lawama zote? Kwanini ahukumiwe kwa kosa lisilo lake? Rostam hakuiba, yeye kosa lake ni kuwasaidia wezi kuficha mali ya wizi, tumhukumu kwa hilo, lakini si kwa kosa la wizi, tuwatafute wezi wetu na tuwahukumu kwa madhambi yao. Source: Mwananchi

Kwa mantiki hii viongozi wote waliohusika na kuileta Richmonds na dada yake Dowans ni lazima wawajibike bila upendeleo.Haingii akilini tukawawajibisha wachache na kuwaacha wengine.Haki ni lazima itendwe kwa wote waliohusika na ufisadi huu.
 
Mnamwandama Rostam Azziz kwa sababu ni Mu-Islaam.

Shame on you Wakristo mkiongozwa na Mwakyembe, Samuel Sitta, Slaa, Mbowe, Lema, na genge zima la Wakristo. Mwataka wengine wale wapi?

Sometimes I feel I don't deserve kuwepo kwenye forum moja na watu kama wewe Sikonge!!! Siijui elimu yako lakini kwa kuwa unajua kutumia computer, ni dhahiri kwamba ulienda shule (ingawa sina uhakika na kuelimika kwako).

Hivi unawezaje kuchukulia mambo mazito yanayoikabili nchi yetu kimzaha mzaha hivi? Naungana na mdau mmoja aliyewahi kusema kwamba ingekuwa vema tungejulikana kwa majina yetu halisi, pengine pumba kama hizi zisingekuwepo.

Mtaniwia radhi lakini ukweli ni kwamba inasikitisha na kukasirisha kuwa na watu wenye mawazo kama ya Sikonge na hawaoni aibu kuchangia watu wazima wanapoongea. Na kibaya zaidi wanajiita Great Thinkers!!!!

Nakulilia Tanzania.
 
Mnamwandama Rostam Azziz kwa sababu ni Mu-Islaam.

Shame on you Wakristo mkiongozwa na Mwakyembe, Samuel Sitta, Slaa, Mbowe, Lema, na genge zima la Wakristo. Mwataka wengine wale wapi?

Sasa ukisikia kufilisika kifikra ndiko huku yani hutaki fisadi atajwe kwa jina kwa kuwa ni muislamu,hapa hakuna anayejadili dini ya mtu kunachojadiliwa ni ufisadi tu na jinsi unavyonyong'onyesha uchumi wa nchi.Mbona ametajwa EL na Mzee wa kikofia chekundu Nimrod Mkono hakuna aliyesema udini.Kama hauna cha kuchangia kaa kimya.
 
Mnamwandama Rostam Azziz kwa sababu ni Mu-Islaam.

Shame on you Wakristo mkiongozwa na Mwakyembe, Samuel Sitta, Slaa, Mbowe, Lema, na genge zima la Wakristo. Mwataka wengine wale wapi?

.
Tunaemwandama hapa ni mwizi ila kama uislamu unajinajibisha kama mwizi acha tuuandame maana mwizi sii rafiki yetu hata kidogo.
.
 
Mnamwandama Rostam Azziz kwa sababu ni Mu-Islaam.

Shame on you Wakristo mkiongozwa na Mwakyembe, Samuel Sitta, Slaa, Mbowe, Lema, na genge zima la Wakristo. Mwataka wengine wale wapi?

Nina wasiwasi na shule uliyosoma ww!! Maana naona hata uwezo wa kufikiri huna. Tatizo la mtanzania yule mwenye dhiki sana ndiyo anaunga mkono utumbo wa akina (Rostam Aziz) a.k.a IRAN. Kwa taarifa yenu huyu jamaa hana uchungu na hii nchi kwa sababu anajijua si mtanzania. Hata mkimtoa baruuu tayari kwao IRAN ni billionea. Ameshajichumia kwa wadanganyika kwa raha zake.
 
Hahahaaa, SOMA VIZURI UJUMBE WANGU.

Kama kweli una akili na Great Thinker utaelewa kilichopo ndani. Go Deep Mazee......

I know you can do better than that.

Kachero na Kiby na nyinyi someni vizuri ujumbe. Vinginevyo, rudini darasa la sita.
Sometimes I feel I don't deserve kuwepo kwenye forum moja na watu kama wewe Sikonge!!! Siijui elimu yako lakini kwa kuwa unajua kutumia computer, ni dhahiri kwamba ulienda shule (ingawa sina uhakika na kuelimika kwako).

Hivi unawezaje kuchukulia mambo mazito yanayoikabili nchi yetu kimzaha mzaha hivi? Naungana na mdau mmoja aliyewahi kusema kwamba ingekuwa vema tungejulikana kwa majina yetu halisi, pengine pumba kama hizi zisingekuwepo.

Mtaniwia radhi lakini ukweli ni kwamba inasikitisha na kukasirisha kuwa na watu wenye mawazo kama ya Sikonge na hawaoni aibu kuchangia watu wazima wanapoongea. Na kibaya zaidi wanajiita Great Thinkers!!!!

Nakulilia Tanzania.
 
go go Mwakyembe ondoa huyo bagachori arudi kwao Irani analeta wachekeshaji anawaita wawekezaji, wanaingia ubia wanakula Bia wanalewa chakali wanasahau kilichowaleta, tumekuwa macho sasa Tanzania suo shamba la Bibi ni Shamba la Mbwa Mwitu ukileta ubabe tunakutoa utumbo , msituchezee kabisa
 
Suala la Dowans lilijitokeza juzi jumatatu wakati kamati ya wabunge wa CCM iliyoketi Dar es Salaam, nimefurahishwa na hii nukuu jinsi alivyozungumza Mwakyembe: "Mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu: anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi"

Source: Mwana Halisi Janaury 26-Feb 1, 2011 Ukurasa wa pili paragrafu ya 22

Halipwi fisadi yeyote mpaka kieleweke. Wakati umefika sasa wa kuwasimamisha mafisadi waliokubuhu kwa uwezo wetu wote ili wasiendelee kuifanya nchi yetu kama shamba la bibi.

Kwa taarifa yako, mie sina dhiki. Soma tena na tena uelewe na si kuchukulia tu kwa nje.

Ndiyo nyie akina Ronaldo mnatongoza wanawake, mkifika home mnakuta kumbe madume.

Fikiri zaidi na zaidi mwanawane kabla hujarukia mambo, kama kweli zina-charge.
Nina wasiwasi na shule uliyosoma ww!! Maana naona hata uwezo wa kufikiri huna. Tatizo la mtanzania yule mwenye dhiki sana ndiyo anaunga mkono utumbo wa akina (Rostam Aziz) a.k.a IRAN. Kwa taarifa yenu huyu jamaa hana uchungu na hii nchi kwa sababu anajijua si mtanzania. Hata mkimtoa baruuu tayari kwao IRAN ni billionea. Ameshajichumia kwa wadanganyika kwa raha zake.
 
Unataka Mwakyembe asema nini zaidi ya haya?

"Lakini Mhe. Dk. Msabaha (Mb), baada ya mahojiano chini ya kiapo, akaniuma sikio Kamati Teule kuwa katika suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu au, kwa maneno yake mwenyewe, “Bangusilo” kwa lugha ya Kizaramo. Maelezo hayo ya ziada nje ya kiapo ya Mheshimiwa Waziri yaliyotoa ujumbe kuwa “si yeye ila mkuu wake wa kazi”, yalioana na maelezo aliyoyatoa Balozi Kazaura nje ya kiapo tarehe 30 Novemba, 2007. Mara baada ya kumaliza mahojiano kwa kiapo na Kamati Teule, Balozi akatoa maelezo ya ziada kuwa Richmond ilikuwa mradi wa “Bwana Mkubwa” na “mshiriki wake mkubwa kibiashara”, akimaanisha Mhe. Waziri Mkuu na Mhe. Rostam Aziz (Mb).

[FONT=Trebuchet MS, sans-serif]Kamati Teule ilikuwa imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7 waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.[/FONT]

...

Miruko ngoja nikuulize?

  1. Hivi hiyo Kamati ilifanya jitihada gani kutambua huyo Bwana Mkubwa aliyetajwa ni nani?
  2. Pia ilifanya jitihada gani kuhakikisha kuwa inawabana Msabaha na Kazaura kutoa ufafanuzi kuwa Bwana Mkubwa wanayemuongelea ni Mkubwa wao kikazi na siyo Bwana Mkubwa wao wa madili?
  3. Je hiyo Kamati ilifanya jitihada gani kuhakikisha kuwa wanampata huyo Bwana Mkubwa, wanamhoji na kutoa ripoti kama walivyoagizwa na Bunge kuchunguza suala zima na siyo kubakiza?
  4. Na kama walishindwa kumhoji huyo Bwana Mkubwa na kuhakikisha kama kweli alihusika, ilikuwaje wafikie hitimisho kwamba kuna watu inabidi wachukuliwe hatua za kinidhamu (na hapa ni kwamba kama huyo Bwana Mkubwa ni Mkuu wa Kazi na ndiye mwenye mradi inawezekanaje awatie adabu watu waliokuwa wanatii amri yake?)
  5. Je huoni kwa maswali yangu nina haki kabisa ya kumshuku Mwakyembe?
 
Ujasiri ni kuongelea kwenye Kamati Kuu ya CCM? Hiyo taarifa anayo toka alipoketi kama Mwenyekiti wa Kamati ile! Alikuwa anaijua kabla ya hukumu kutolewa! Akapewa na uwaziri kama zawadi! Akaukubali na anaendelea nao! Sasa hivi Rostam akijiuzulu uchaguzi katika jimbo lake utarudiwa fedha ya kodi itatumika bado ametusaidia? Mbona hakusema kabla ya uchaguzi wananchi wajue? Au anasaidia chama kwanza then watanganyika?

Na Mwakyembe anajua, Raisi hajui? Siku zote hajamwambia? Kama amemwambia na Raisi amekaa kimya ametusaidiaje? Kama hajamwambia kwa nini?

Lazima tujiulize sana katika hili jambo na kupata majibu sahihi! Tukikurupuka tutabaki washabiki kama ilivyokuwa kipindi cha kujiuzulu kwa EL!

Nyie watanzania wa Igunga sijui kama mambo ya magazeti yanayoandika juu ya ufisadi wa Rostam mnasoma, Badala ya kusema Mwakyembe au Sitta au Kikwete basi muulizeni Rostam moja kwa moja. Mi naona hata kama Mwakyembe akisema haya kabla ya uchaguzi lakini watanzania wa igunga kama hamwoni Rostam kuwa ni Fisadi hapo ni pagumu lazima tuamue sisi wenyewe kumweka chini ya vurugu Rostam. Namna gani ????????????????????????????????????????????????????
 
Mnamwandama Rostam Azziz kwa sababu ni Mu-Islaam.

Shame on you Wakristo mkiongozwa na Mwakyembe, Samuel Sitta, Slaa, Mbowe, Lema, na genge zima la Wakristo. Mwataka wengine wale wapi?

Hyuy labda kama anatumia password ya Sikonge but the Sikonge i know sio huyu
 
Sikonge aisee weee una akili sana...................Heri ya mwaka mpya Mkuu
 
Nyie watanzania wa Igunga sijui kama mambo ya magazeti yanayoandika juu ya ufisadi wa Rostam mnasoma, Badala ya kusema Mwakyembe au Sitta au Kikwete basi muulizeni Rostam moja kwa moja. Mi naona hata kama Mwakyembe akisema haya kabla ya uchaguzi lakini watanzania wa igunga kama hamwoni Rostam kuwa ni Fisadi hapo ni pagumu lazima tuamue sisi wenyewe kumweka chini ya vurugu Rostam. Namna gani ????????????????????????????????????????????????????

Siasa za kibongo bora kuingia mtaani tu
 
Ni mie kabisa wala sijabadilika. Nisome vizuri utanipata. Sema leo naingia kwa kutumia UNGO na kutua na sipitii milango ya siku zote.
Hyuy labda kama anatumia password ya Sikonge but the Sikonge i know sio huyu
 
Sikonge, nina wasi wasi, ni wewe uliyeandika hayo. maana nakufahamu muda mrefu sana.
 
Hahahaa, Ogah. Asante kwa kunitakia heri na mie nikutakie pia hiyo heri ya Mwaka mpya 2011.

Nafurahi umeingia tu na kunipata kwenye mawimbi nayotumia leo. Nafurahi na Hasira za watu hapa ambazo hazimnyimi Rostam usingizi. Kwa hili inabidi nikubaliane na Waberoya kuwa "inabidi kulipasua jipu bila kuangalia mgonjwa analia vipi......"
Sikonge aisee weee una akili sana...................Heri ya mwaka mpya Mkuu
 
Back
Top Bottom