Wana JF
Ninavyoona mimi Hoja za mwakyembe hazina mashiko hata kidogo, kama sikumnukuu vibaya amesema kuwa ilikuwa shamhuna afikirie dhana ya collective responsibility na asipinge kauli ya PM Mizengo Pinda ,OKAY. Sasa hapa ninapata kigugumizi..... collective responsibility ipi aliyoikusudia Harison Mwakyembe kwa sababu kama ni utendaji wa Baraza la Mawaziri Shamhuna hahusiki na baraza la mawaziri la T/bara au pengine kuna mantiki mengine yaliyiojificha. ......... Sijui, lakini nafikiri kama Mwakyembe hataki kuelewa mipaka ya kiutendaji kati ya SMZ/ SMT/bunge/ baraza la wawakilishi hio ni kasoro kubwa akiwa yeye ni mwanasherisa wa kuheshimika.

La pili, Kwa mtazamo wa haraka hoja hii ya znz ninchi, wilaya au handeni, biharamulo, haipewi nguvu si tu ndani ya bunge au kwenye vyombo vya habari. Inaonekena wazi wazi kuwa Spika anamlinda PM pinda asijibu hoja yoyote ile inayohusiana na sakata hii. Kwa nini? Hapana jawabu ya mkato lakini ni mkakati tu wa SMT(Serikali ya Muungano) kukandamiza uhuru wa mawazo kwa wabunge wetu kule bungeni. Je hili Mwanasheria Mwakiyembe ameliona na kulikemea ?????

Ukifuatilia ktk media za bara, utaona kuwa vyombo vyote vya habari haviko objective and neutral katika kuielezea sakata hii ya znz ikielekea kuwa ni wilaya ya handeni / babati. Wahariri wanaendeleza ajenda ya kutulaumu sisi wazanzibari eti hatutaki muungano na hawataki kuandika makala za kiuchambuzi ambazo zingeeleza mambo mengine ambayo yako nje ya boksi na hayapewi nafasi.

Lililobaki, ni sisi wananchi kuja na activism ya hali ya juu na tuoneshe wazi kuwa hatutaki muungano kabisa na sio tu ufanyiwe marekebishao. Wanasiasa wamejitahidi na wanaendelea kujitahidi kuunda jukwaa la kueleza maoni yao na inapasa tuwaunge mkono kwa juhudi zao.
 
Wewe kila kitu "Shamhuna hiki" "Shamhuna hivi" "Shamhuna vile". Au wewe ndiyo Shamhuna mwenyewe?? Unaboa sana aisee!
 
Wewe kila kitu "Shamhuna hiki" "Shamhuna hivi" "Shamhuna vile". Au wewe ndiyo Shamhuna mwenyewe?? Unaboa sana aisee!
Unatakiwa ujibu hoja Ila fahamu katika hili Mwakiembe na Shamhuna ndio wahusika wakuu ,otherwise u may skip.
 
Umekuwa Mwiba sasa.

Huko kukimbiwa mbona hamshindi Olympic basi? Kwi kwi kwi....
 
Wewe unaonekana umefukuka maana unaposema Zanzibar wakipata maji bure na umeme bure ,hayo hayakutoka Tanganyika ,tokea zama Zanzibar maji ni bure ,umeme ukilipwa ,mashule bure madaftari kabakaba,balaa la kulipia mashule na kuadimika vifaa anavyohitaji mwanafunzi limezuka kwa utawala wa Tanganyika kujivalisha ndani ya Tanzania na kuikaba koo Zanzibar kupitia udhibiti wa njia za uchumi na serikali ya Zanzibar kushindwa kutimiza malengo yake nakuhakikishia hata umeme ungelifikia kuwa bure ,lakini leo maji yanaanza kulipiwa ,mashule ndio hivyo usiseme umeme bwanamkubwa mara kazima switch,Zanzibar imegandamizwa na haiwezi hata kufurukuta kwa jamaa waTanganyika roho zilivyowabadilika ,kuna jamaa huko bara wanafikiri Zanzibar ni sawa na Ulaya, this is too macha.
Fedha ikiletwa Tanzania inabidi igawiwe 50 / 50 ,,zimeungana nchi mbili na hapo pia napo pana kero ,vipi utaipa Zanzibar fedha kama unaigawia Wilaya ,hapo ndipo Mawaziri wa Tanzania wanaposhindwa kuwajibika ndani ya Serikali ya Muungano uzalendo unawajaa na kumega sehemu kubwa ya msaada kwa ajili ya kwa Tanganyika ,hivyo sivyo kabisa angalau msaada ungewekwa 2/3 tukafahamiana ,na ndio Muungano lakini mnabinya na mwisho au misaada mingine hata Zanzibar haioni ndani inagawiwa juu kwa juu.

Zao la karafuu wameliua watanganyika? Utalii wameua watanganyika? Yaani mlitegemea biashara ya kuingiza chupi bure na kuzipeleka Tanganyika ndiyo kungewanasua katika dhiki!

Kama alivyouliza mwenye busara kuliko mimi, tugawane fedha 50/50 na tugharamie matumizi 50/50! Mbona mnaangalia mapato tu? Tena misaada! Mawazo tegemezi kama hayo ndiyo yatakayowabakiza hapo mlipo. kila wakati mnasubiri ankal wa Muscat awatumie makombo.

Jiangalieni kwanza kabla ya kukimbilia kumlaumu jirani.
 
Zao la karafuu wameliua watanganyika? Utalii wameua watanganyika? Yaani mlitegemea biashara ya kuingiza chupi bure na kuzipeleka Tanganyika ndiyo kungewanasua katika dhiki!

Kama alivyouliza mwenye busara kuliko mimi, tugawane fedha 50/50 na tugharamie matumizi 50/50! Mbona mnaangalia mapato tu? Tena misaada! Mawazo tegemezi kama hayo ndiyo yatakayowabakiza hapo mlipo. kila wakati mnasubiri ankal wa Muscat awatumie makombo.Jiangalieni kwanza kabla ya kukimbilia kumlaumu jirani.
Naona busara inakushinda,na ukienda huko tutapoteza muelekeo ,kusema wanategemea ankal kuwaletea mitumba kutoka maskati,sio baya ila sasa naamini kuna watu huko Tanganyika wanaona Zanzibar kuna waarabu watupu, watu wa dizaini zenu inaonyesha hata wabunge wanaowakilisha Zanzibar hamuwajui, nilikwisha sema hapa kuwa Tanganyika kuna waarabu wengi kuliko Zanzibar ya leo. Weka kando hilo inaonyesha ni mfinyu wa historia. Itafute Zanzibar Empire katika vitabu vya tarehe za zamani.
Wewe unafahamu hao mankali ndio wameteka hizo mbuga za wanyama na wanawinda kwa nafasi zao ,hivi unaelewa kwamba Bizinez senta kwa ukanda wa Afrika ya mashariki itajengwa hapo Bagamoyo na watakaojenga ni hao hao maankal.hivi unafahamu kuwa hawa maankal wamenunua bandari za kimarekani huko kwa joji kichaka.
Ni kitu gani kinachowafanya kuung'ang'ania Muungano na kusema mnaulinda huku si kulinda bali ni kuikalia Nchi ya Zanzibar kimabavu.
Mnaona haya kitu gani kuitaja Tanganyika yaani mnashindwa kumpa sapoti hata Mtikila mnashindwa kuwaunga mkono wale G55 ni aibu kwa wazalendo waTanganyika kama Wazenji waTauwana ni wao kwa wao nyie hayawahusu nde wala sikio ,lakini ilivyo sasa kama mauaji ya 2001 yalioendeshwa na benyamin Serikali ya Tanganyika ilijiyovisha koti la Muungano inahusika moja kwa moja ,mauaji ya kina Hanga na wenziwe Serikali ya Tanganyika ilijiyovisha koti la Muungano inahusika moja kwa moja.
Hadi hii leo sababu za msingi za kusema mnaulinda Muungano hazipo na mahakama ya katiba mnaiogopa ,wamezuka wazushi wengine eti tuitishe mdahalo ,wengine wanasheria wakuu kila mti mnaokamata unateleza naona mnakufa vifo vya tumbili na kima.
 
Mwakyembe aombe radhi - Wapinzani

2008-08-16 13:36:31
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Kambi ya Upinzani Zanzibar imemtaka mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, kuomba radhi viongozi wa Zanzibar aliowaita watovu wa nidhamu.

Naibu Waziri Kiongozi Bw. Ally Juma Shamuhuna na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bw. Idd Pandu Hassan, walipinga kauli ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, aliyesema Zanzibar si nchi ila ni sehemu ya Muungano.

Wakizungumza na Nipashe mjini Zanzibar jana, Makamu mwenyekiti NCCR Mageuzi, Bw. Khamis Ambar, alisema;`` Dk. Mwakyembe hajawatendea haki viongozi wa Zanzibar kwa kuwaita watovu wa nidhamu wakati hao ni watu wazima na walikuwa wakitekeleza majukumu yao kama viongozi wa serikali ndani ya Baraza la Wawakilishi.``

Alisema mawaziri walilazimika kujibu hoja ya Waziri Mkuu kuwa Zanzibar si nchi, baada ya wajumbe wa baraza hilo kutaka serikali itoe tamko ili wananchi wajue msimamo wake kwenye suala hilo.

``Kwa kweli Dk. Mwakyembe amelipotosha Bunge kwa maslahi yake, ni vyema akaiomba radhi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,`` alisema Bw. Ambar.

Alisema viongozi hao wasingeweza kukaa kimya wakati wajumbe wa Baraza hilo waliokuwa wakichangia bajeti za serikali walitaka kujua msimamo wa serikali kufuatia kauli ya Waziri Mkuu.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Bw. Salum Bimani alisema Waziri Mkuu Pinda hayuko juu ya Mamlaka ya Katiba ya Zanzibar.

Alisema mawaziri wa Zanzibar wanawajibika kwa Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi na sio kama alivyosema Dk. Mwakyembe.

Alitoa mfano kwamba Baraza la Mawaziri lilipovunjwa kutokana na kashfa ya Richmond, Baraza la Mawaziri Zanzibar halikuguswa kwa vile halihusiki na Mamlaka ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano.

``Kauli za vitisho hazifai katika dunia ya leo. Mwakyembe asipotoshe suala hili. Baraza la Mawaziri Zanzibar linasimamia mamlaka na majukumu ya Zanzibar,`` alisema Bw. Bimani.

Bw. Bimani alieleza kushangazwa na Spika Bw. Samuel Sitta kuwaachia baadhi ya wabunge kujadili suala la hadhi ya Zanzibar lakini akiwadhibiti wapinzani.
-------------------------------------------------
Natumai hoja yangu ya kuwa yeye Mwakiyembe ndio inafaa aadhibiwe imekubalika. Wana JF msiwe mnapinga kila kitu wanachoandika wengine,nimetupiwa mijineno kibao na baadhi yetu ambao ,waliniona nimekosea kwa kumgeuzia kibao Mwakiyembe ,ila tujaribu kuipa sheria mkondo wake ,Mwakiyembe alikosea tena vibaya sana, hoja ilikwisha zuiwa na Spika Sitta ,ni ushujaa gani uliompa Mwakiyembe kuruka kiunzi cha Spika ?
-----------------------------------------------------
KATIBA MPYA NI KITU CHA LAZIMA,kwa Muungano na yasio kuwa ya Muungano. Je Majeshi ya upinzani yataweza kuelekezwa huko ili ipatikane Katiba Mpya katika mfumo wa Vyama vingi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya UPDP, Bw. Haji Othman Haji, alisema kutatua suala hilo ni kuanzishwa haraka Mahakama ya Katiba ya Muungano.

Matatizo yanayojitokeza ndani ya Muungano yalisababishwa na orodha ya mambo ya Muungano (Articles of Union) kwa siku moja wakati ni jambo lililohitaji muda wa kutosha.

Naye Joseph Mwendapole anaripoti kwamba Mhadhiri mkongwe wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu, amesema suluhu ya malumbano ya ama Zanzibar ni nchi au la ni kutungwa kwa Katiba mpya.

Akizungumza na Nipashe jana, Profesa Baregu alishauri uitishwe mjadala wa kitaifa utakaohusisha wananchi wote na ambao utazungumzia namna ya kuandika katiba mpya.

``Kwa muda mrefu watu wanalalamikia muundo wa Muungano sasa ni muda mwafaka mjadala huu uje na watu waulizwe wanataka serikali tatu au mbili ili kumaliza manung\'uniko ya muda mrefu,`` alisema.

Profesa Baregu aliongeza kuwa suala la Katiba mpya haliepukiki kwani ndio suluhisho pekee la kumaliza malumbano ya muda mrefu.
 
Kwani hamkujua tangu awali kama huyu mwakyembe ni mtu wa kukurupuka? angalia hii, anasema kwamba, waziri mkuu akisema jambo kwa kile alichokiita " ministerial collective responsibility" ni kwamba atakachosema waziri mkuu hata kikiwa kibaya basi mawaziri wote mnatakiwa mkikubali. akatolea mfano zaidi ya kwamba, ndio maana alipojiuzuru lowassa, mawaziri wote walijiuzulu. kisha akataka mawaziri wa zanzibar waliopingana na Pinda, wamekiuka maadili ya kazi. Mimi na jiuliza, kwani, alipojiuzulu lowassa, na balaza la mawaziri la zanzibar lilijiuzuru? kwani waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano ndiye anayesimamia baraza la mawaziri wa zanzibar? huyu mwakyembe anasema shamuhuna amekwenda kinyume kwa hoja ipi? yeye haoni anazidi kuonyesha madudu yake?

Tena huyu mwakyembe anajulikana sana kwa tabia yake ya kuendekeza udini. ni mbaguzi sana, hata rafiki yake wa karibu aliyemsaidia kupata ubunge amegombana naye kwa tabia yake hiyo, japokuwa wanakaa karibu huko Kunduchi, lakini hata salamu hakuna.

Nimehakikisha hilo, juzi akichangia hoja hii ya Mahakama ya kadhi, eti anatolea mfano wa znz akiacha kenya, kama vile hajui. anadhani anaongea na watoto wa chekechea.
 
1.
Unapozungumza kuwa mkweli mwanzo mpaka mwisho. Ivo umesahau yule Mnyamwezi wa Tabora ndie alikuwa Deputy Chief Minister wa mwanzo?

Mkuu heshima yako kwanza, in the future jaribu kuelewa hoja kwanza kabla hujakurupuka, hoja yangu ni kwamba kwenye katiba yetu ya Jamhuri cheo cha Deputy Prime Minister hakipo, hii ni fact sio opinion yangu,

However: Toka tupate uhuru kumekuwa na tabia kutoka kwa baadhi ya viongozi wetu wakuu kujaribu kuwabembeleza wapambe wao kwa kulazimisha kuwepo hiyo nafasi temporaly, kwa mfano:-

1. kiongozi wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Mwalimu, alipoona Salim amekataliwa kuwa rais, akamtengenezea hiki cheo ili kumfariji kwa the expense of us wananchi.

2. Wa pili alikuwa Malecela, akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza Wa Rais, alipoona Mrema anakuwa threat kwenye mbio za kugomeba urais wa 1995, akamtengenezea hii nafasi ili kumshawishi apunguze mbio za urais.

3. Na this time naye Muungwana, baada ya kuona Shamuhuna amekosa umakamu wa rais, naye akamtengenezea hako ka-nafasi kumfariji.

Ahsante Mkuu.
 
Yaani mkuki kwa nguluwe au sio ,pale Shamhuna alisema hakuna selikali ya Mseto wala choloko ,akina Mwakiyembe walipiga makofi,sasa inakuwaje leo aombe lazi.tamko rasmi kutoka serikalini SMZ mmelisikia ni majibu kutoka CCM kisiwa ndui Zanzibar(Wahafidhina wakiitaka timu ya Butiama iombe razi
)

Matatizo ya sasa ya kisiasa Zanzibar hayawezi kutatuliwa kwa kujaribu ku-vent frustrations zenu on viongozi kama Mwakyembe, ni kufukuza hewa,
toeni ushauri wa namna ya kuumaliza mgogoro wenu wa muafaka huko Visiwani, ni nyinyi wenye matatizo in the first place,

kauli za Shamuhuna ni za kushauriwa na washauri wabovu kuwa ajaribu kum-bully Muungwana, ili ampe nafasi ya kugombea urais wa huko wakati muungwana ameshaamua kwenda na Bilali, kwa sababu anahitaji a strong hand ya ku-deal na siasa za huko, Shamuhuna mpambe wa Rostam hana huo ubavu, na besides hana ukaribu sana na muungwana kuliko Khatibu na Ameir,

na hicho cheo kulikuwa ni one term only maana Mtandao sasa hauhitaji tena watu kama Shamuhuna, ili kushinda term ya pili, kwa hiyo he is doomed sasa anaweza kupiga kelele as much as he wants, ndio maana kina Husein Mwinyi, walihamishiwa huko, ni ili waje wazibe nafasi za kina Shamuhuna.

Ahsante Mkuu.
 
Zipo tetesi kuwa UWT wapo njiani kupunguza ving'ora kwa Mhe. Waziri huyo ambae ndio anaongoza kwa Tz nzima kuliza Ving'ora na misafara mrefu kuliko hata hao mabosi wake...
 
UDINI NA UELEWA MDOGO UNAWASUMBUA MWIBA, NGEKEWA NA MIZIZI
Ukifuatilia kwa karibu hoja za akina Mwiba, Ngekewa na Mizizi unagundua bangi inayowasumbua - UDINI na uelewa mdogo. Mizizi ndo kashindwa kabisa kuficha kiini cha hasira zake dhidi ya Dk. Mwakyembe-UDINI! Kakasirika kwa nini Dk. Mwakyembe alilimwagia maji Bungeni suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ambayo itaendeshwa kwa kodi yetu wote, Waislamu na wasio Waislamu. Wote watatu wanafanana kwa uelewa usioridhisha wa hoja yenyewe; wametoka nje ya mjadala!
Hivyo nawaomba wasome hansard ya Bunge katika mtandao, wajue alisema nini Dk. Mwakyembe!
Sisi wengine tumemwelewa! Dk. Mwakyembe anasema hakuna mgogoro wa kikatiba ila utovu wa nidhamu wa Mawaziri wa Zanzibar, kitu ambacho ni kweli. Toka lini Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar akawa level moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kiprotokali ni mtu wa sita katika mlolongo wa itifaki: Rais wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi, halafu ndo unamkuta Shamhuna na U-naibu Waziri Kiongozi! Hata kama tuna Serikali mbili, haziko ngazi moja, ndo sababu ya hiyo itifaki! Ki-CCM, Shamhuna hayuko hata kwenye orodha! Pinda ni mjumbe wa NEC na Kamati Kuu ya CCM! Waziri Mkuu anasema jambo, halafu Shamhuna anamjibu, tena kwa fujo na kusema "enzi za kutishana zimepita!" Halafu Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, mnashindwa kuona hoja ya msomi Mwakyembe! Hana adabu huyu ati!
Jana nilimsikia msomi mwingine Dk. Mvungi akisema Mwakyembe ana hoja ya msingi. Vipo vyombo chungu nzima vya kushughulikia mambo ya Muungano k.m. ofisi ya Makamu wa Rais, hivi Shamhuna hakuviona mpaka aropoke kumshambulia kiongozi wake wa CCM na wa Serikali? Ipo hoja aliyoiongelea Dk. Mwakyembe ya kuwa mawaziri wanafungwa na kanuni ya katiba ya kuwajibika kwa pamoja kama serikali. Hili ni suala la kitaalamu ambalo sisi wengine akina Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, tunyamaze tu!
 
Bora umewatolea uvivu mjomba. Hawa Waislamu wa Visiwani bwana vichwa ngumu kweli. Haya ndiyo matatizo ya elimu za madrasah na jadi ya kuhusudu Wamanga.
 
Naona busara inakushinda,na ukienda huko tutapoteza muelekeo ,kusema wanategemea ankal kuwaletea mitumba kutoka maskati,sio baya ila sasa naamini kuna watu huko Tanganyika wanaona Zanzibar kuna waarabu watupu, watu wa dizaini zenu inaonyesha hata wabunge wanaowakilisha Zanzibar hamuwajui, nilikwisha sema hapa kuwa Tanganyika kuna waarabu wengi kuliko Zanzibar ya leo. Weka kando hilo inaonyesha ni mfinyu wa historia. Itafute Zanzibar Empire katika vitabu vya tarehe za zamani.

Hicho kitu busara sijawahi kuwa nacho lakini nijuavyo mimi ni kuwa hapajawahi kuwa na Zanzibar Empire. Ingawa Zanzibar imekaliwa kwa zaidi ya miaka 20,000 lakini umaarufu wake kihistoria umetokana na kuwasili kwawashirazi mwaka 875 chini ya Abi Ben Sultan Hassan. Hawa walichanganyikana na wazawa waliowakuta na kutoa waswahili. Zanzibar kama ilivyokuwa Kilwa ( kwa muda mrefu ulikuwa maarufu kuliko Zanzibar), Malindi, Mogadishu, Sofala n.k. zilikuwa city states ambazo zilikuwa zikishindana katika biashara. Hakuna hata moja yao iliyowahi kutawala sehemu ya bara. Katika biashara zao walitegemea ushirika wa makabila kama wanyamwezi kuweza kufanikiwa. Alipoingia mreno katika karne ya 15 aliweza kuitawala miji hiyo kwa karibu miaka 200 ambapo waswahili kwa kushirikiana na waarabu wa Oman waliweza kuwafukuza kote isipokuwa msumbiji. Zanzibar ilipata umaarufu zaidi mwaka 1832 wakati Sultan Seyyid Said wa Oman alipoifanya Zanzibar kuwa makao makuu wa himaya yake. Tarehe 27 Agosti 1896 waarabu wa Zanzibar walifurukuta kidogo ndipo merikebu ya uingereza ilipoipiga mizinga kasri ya Beit al Hukum. Dakika 38 baadae mashujaa hao wazanzibari wakanyanyua mikono na kuifanya kuwa ndiyo vita fupi iliyowahi kutokea duniani. Linganisha na wenzao wa bara wakina Mkwawa na wenzie. Desemba 1963 waingereza walirudisha utawala kwa sultan na si kwa waswahili. Waswahili walifanya mapinduzi 1964 kuung'oa utawala wa huyo Sultan. Sultan alipewa hifadhi na Nyerere hadi hapo alipoweza kukimbilia kwengine.

Muda wote kabla ya hayo mapinduzi watawala wa zanzibar walikuwa ni waarabu wakitetewa na waingereza. Hata mgawanyiko kati ya unguja na pemba unamsingi huo wa ubaguzi wa rangi, mweusi dhidi ya mwarabu. Moja ya mbinu chafu za kumkataa Salim Ahmed Salim kugombea urais wa Tanzania zilitumia dhana ya kuwa yeye ni mwarabu. Na haya yalisemwa na nyie sio sisi! Yote haya ni ya kwenu na si ya kwetu sisi machogo. Naam, hatuna busara lakini tunawajua ndugu zetu! Inawezekana kabisa kuwa tanganyika kuna waarabu wengi kuliko huko Zanzibar. Cha muhimu ni kuangalia ni theluthi gani ya population ni hao unaowaita waarabu. Hao waarabu hawajawahi kutawala sehemu yeyote ya maana ya Tanganyika ukiondoa pengine hizo city states ambazo zilikuwa zikijitawala kwa muda mrefu wa uhai wake.
 
UDINI NA UELEWA MDOGO UNAWASUMBUA MWIBA, NGEKEWA NA MIZIZI
Ukifuatilia kwa karibu hoja za akina Mwiba, Ngekewa na Mizizi unagundua bangi inayowasumbua - UDINI na uelewa mdogo. Mizizi ndo kashindwa kabisa kuficha kiini cha hasira zake dhidi ya Dk. Mwakyembe-UDINI! Kakasirika kwa nini Dk. Mwakyembe alilimwagia maji Bungeni suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ambayo itaendeshwa kwa kodi yetu wote, Waislamu na wasio Waislamu. Wote watatu wanafanana kwa uelewa usioridhisha wa hoja yenyewe; wametoka nje ya mjadala!
Hivyo nawaomba wasome hansard ya Bunge katika mtandao, wajue alisema nini Dk. Mwakyembe!
Sisi wengine tumemwelewa! Dk. Mwakyembe anasema hakuna mgogoro wa kikatiba ila utovu wa nidhamu wa Mawaziri wa Zanzibar, kitu ambacho ni kweli. Toka lini Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar akawa level moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kiprotokali ni mtu wa sita katika mlolongo wa itifaki: Rais wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi, halafu ndo unamkuta Shamhuna na U-naibu Waziri Kiongozi! Hata kama tuna Serikali mbili, haziko ngazi moja, ndo sababu ya hiyo itifaki! Ki-CCM, Shamhuna hayuko hata kwenye orodha! Pinda ni mjumbe wa NEC na Kamati Kuu ya CCM! Waziri Mkuu anasema jambo, halafu Shamhuna anamjibu, tena kwa fujo na kusema "enzi za kutishana zimepita!" Halafu Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, mnashindwa kuona hoja ya msomi Mwakyembe! Hana adabu huyu ati!
Jana nilimsikia msomi mwingine Dk. Mvungi akisema Mwakyembe ana hoja ya msingi. Vipo vyombo chungu nzima vya kushughulikia mambo ya Muungano k.m. ofisi ya Makamu wa Rais, hivi Shamhuna hakuviona mpaka aropoke kumshambulia kiongozi wake wa CCM na wa Serikali? Ipo hoja aliyoiongelea Dk. Mwakyembe ya kuwa mawaziri wanafungwa na kanuni ya katiba ya kuwajibika kwa pamoja kama serikali. Hili ni suala la kitaalamu ambalo sisi wengine akina Mwiba, Ngekewa na bwana udini Mizizi, tunyamaze tu!

mimi nafikiri joto la watanzania limepanda sana na hakuna mwingine yeyote yule aliyelipandisha zaidi ya CCM

kwanza wao ndiyo kwa ujinga wao na tamaa ya kupata kura kwa kila mtanzania ndiyo walitumbukiza swala la Kadhi kwenye Ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2005

Ingawa Msambya anataka kutuaminisha kwamba Mangula,Mkapa,na Malecela ndiyo walioiandika ilani hiyo lakini ukweli wa mambo wao hawahusiki isipokuwa vikao vyote vya CCM kuanzia kamati Kuu hadi Mkutano Mkuu wa 2005

tena kikwete aliwahi kusema la Kadhi si la CCM bali Mrema!!? Jamaa ana vituko huyu!

Pili kwa CCM kuona kwamba hoja kubwa ya CUf inayowapatia mtaji kwa wazanzibar ni hoja ya kupata madaraka zaidi ya kiutawala kwa zanzibar,na kina Shame- huna (Shameless?) nao wameirukia. hiyo ni hofu ya CCM kushindwa mwaka 2010
 
Mnaona haya kitu gani kuitaja Tanganyika yaani mnashindwa kumpa sapoti hata Mtikila mnashindwa kuwaunga mkono wale G55 ni aibu kwa wazalendo waTanganyika kama Wazenji waTauwana ni wao kwa wao nyie hayawahusu nde wala sikio ,lakini ilivyo sasa kama mauaji ya 2001 yalioendeshwa na benyamin Serikali ya Tanganyika ilijiyovisha koti la Muungano inahusika moja kwa moja ,mauaji ya kina Hanga na wenziwe Serikali ya Tanganyika ilijiyovisha koti la Muungano inahusika moja kwa moja.

Kwetu sisi Tanganyika ilikufa mwaka 1964 na hatuna haja ya kuifufua ili tujione tumekamilika.

Mimi sasa napata wasiwasi kama wewe kweli ni mtu wa Zanzibar. Unadhani nani aliyemuokoa Mohamed Babu yasimpate yaliyowakuta wakina Hanga, Mdungi na wengine kama sio Nyerere? Waarabu na wahindi wangapi waliopata hifadhi huko unakokuita Tanganyika kukwepa kuozwa kwa nguvu kwa waswahili? Kuanzia Sultan wenu hadi wakina babu, tumekuwa tukiwakingia kifua ili msiwanyonge leo unadiriki kututupia shutuma hizo zisizo na msingi? Unadhani bila kuwepo hiyo Tanganyika waunguja wangeacha kuwachapa bakora wapemba? Wakati mkivalishwa suruali kwa nguvu na kupigiwa king'ora kila jioni kimbilio lenu si lilikuwa huko Tanganyika? Unadhani hao wapemba waliojaa Namanga, Ilala na kwengineko walitoka wapi? Kama kweli mnapendana kwa nini hawakubakia unguja?

Kwa taarifa yako hao wanaoupigania huu Muungano ni kutokana na undugu ambao upo baina yetu na kuheshimu ndoto za wazazi wetu. Wengi wa kizazi cha sasa wanaona kuvunjika kwa huo muungano itakuwa ni kama pakacha kuvuja! Ni wachache tutakaotoa machozi hilo likitokea. Na mshukuru kuwa tupo bado.
 
Spika Sitta ni mzushi mwengine ,hivi ni nani aliemuambia kuwa Mzee wa Mikasi ni mwakilishi wa Zanzibar ,jamani naona MiCCM imekuja juu lakini ,mtakufa kifo Nyani au kima.
Kijana Lazaro huna kina hata kimoja unachokijua,usibabaishe na kutaka kuuuficha ukweli ,Mwakiyembe amekosea na amekwenda mbali sana kusema hadharani chuki zake binafsi kwa viongozi wanaoitetea Zanzibar kuwa ni Nchi eti waadhibiwe ati hawana adabu ,eti wamedharau.
Mwakiyembe amechonga fitna ndani ya CCM na ndio mpaka leo CCM hawaelewani,na kama Mwakiyembe na kamati yake kama sio majungu na chuki nini kimefanyika hadi leo.
Mtamtetea sana na nyie mnaomtetea hamumtakii heri huyu jamaa kila mkizidi kumtetea ndio mnamuingiza ndani ya shimo ambalo hataweza kutoka.
Ikiwa Serikali ya Zanzibar itaamua kumshitaki Mwakiyembe kwa kuwaita mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na Waziri Shamhuna hawana adabu basi atakuwa matatani ,hao wenzake anaowaona marafiki watamgeukia na hapo ndipo atakapoifahamu chungu ya CCM.
Hivi Ndugu Lazaro kati ya Shamhuna na Mwakiyembe nani alitoa ujeuri na kukosa adabu na kuvuka mipaka ya uzungumzaji.
Napenda kama utakariri aliyosema Shamhuna na aliyosema Mwakiyembe halafu tupime kwa kipimo utakacho wewe.
Hapa usilete mambo ya itifaki kwani hiyo itifaki ni moja ya mambo yasiyokubaliwa na WaZanzibari ,hilo ni katika mipango yenu ya kuimeza Zanzibar.
Makamo wa kwanza haiwakilishi Zanzibar kama inavyosema Hati ya Muungano ila Sitta spika anaesimamia hoja za Chama chake anataka kulilazimisha, haijulikani wazo hilo amelitoa wapi.
Halafu Ndugu Lazaro siku hizi usilete mambo ya Katiba kwani imeshagundulika hiyo Katiba unayoitegemea imetungwa na CCM kwa manufaa yao ,haifai tena tunaweza kusema imekwisha expire tokea kuundwa kwa mfumo wa Vyama vingi ,sasa hao wasomi unaowataja kama watakwambia ukweli basi watakubaliana kuwa Katiba iliyopo haifai hata kunakiliwa katika hoja za siku hizi kwani mambo yamebadilika siku hizi ni kasi na ari mpya sasa utaleta Katiba iliyotungwa kuendeleza Ujamaa ,hayo ni mambo mbali mbali kabisa.
Wameambiwa na kila mtu wabadilishe KATIBA wanasema wakati haujafika, maana CCM haijaondoka madarakani ,ndio maana yake.
Hao MaDr. hawana msimamo ni watu wa kutumiwa tu na wanajali maslahi yao binafsi kwa kuwa wanaposema hivyo watu kama akina Lazaro mnawaona MaDr. wamesema ukweli na mnawapenyezea vijisenti au kuwafagilia, wakati watu hao wanshindwa kuwatetea WaTanzania kwa kuogopa kumhoji Raisi ,kwa kuogopa Kumhoji waziri Mkuu au waziri yeyote yule ,si mnamuona Sitta siku hizi anazima masuali ya papo kwa papo ,wanataka kuiga mambo wakati hawayawezi. Na nyinyi kina Lazaro mnaona hawa ndio viongozi wa kuwategemea.
 
Kama mnajua kuna ukweli, kwanini Sitta,anazuia Pinda asiyajibu masuala la wabunge wa ZNZ kuhusu suala hili. kama kuna ukweli kwanini mnakataa kuuweka Hadharani mkataba wa Muungano.
Mwisho, mjinga Sitta,hebu tukuulize,wewe ni Spika,ni waziri mkuu na ni mwenyekiti wa Bunge, maana unafanya kazi zote hizo. Halafu bado unaendela kusema UONGO ndani ya bunge na kama wakuadhibiwa basi ni huyu Sitta. Ati makamo wa Rais huyu Shein ndio muwakilishi wa ZNZ ndani ya Muungano, hivi tueleze hivyo ndio MKATABA wa MUUNGANO unavyosema au ndio Katiba viraka inavyosema.

Ati Sitta anasema , wabunge wa ZNZ wasidai serikali ya Tanganyika waachiwe Watanganyika wenyewe , Well kama ni hivyo unaamini katika haki ya mtu kuamua kwanini, mnakerwa na Wazanzibari kudai wanachotaka. Lakini hujasema kweli, Watanganyika hamdai serikali yenu na hamtaki kuidai,kwasababu ipo, mmeigeuza jina tuu ,ipo inaitawala ZNZ kwa mabavu, lakini , Pinda amepinda kweli,maana Hapa mpaka kieleweke. Mmelikoroga kwa kibri na jeuri sasa mtalipa ghali sana.

Wewe Sitta unatumia nafasi hiyo kwani ni kama umekuwa Blackmailed ,Sitta ni mbinafsi na hashemu wengine ,Sitta unajulikana kwa kuwanyima wabunge haki ya kuzungumza kwa kuona au kujiona tu kuwa wewe ndie unaefahamu kila kitu , Kama mtakumbuka na Sitta atajisahaulisha alivyomtukana Naibu Spika eti hawezi kusimamia mambo nyeti mpaka awepo yeye mwenye Bunge? ! Kisa nini? Kupenda sifa na kumdhalilisha mwenzake mbele ya umma na sasa anawazuia wabunge wasiulize, halafu bado anaendelea kuliita Bunge eti ni chombo cha kidemokrasia!
Sitta anajifanya kuwa dikteta ndani ya Bunge na anajipendeza sababu na nia ya kufanya hivyo inajulikana kuwa analinda ufisadi anaoufanya.Sitta unajulikana kwa kuchota fedha za bunge,Sitta umeshutumiwa kwa kutmia fedha za Bunge vibaya na matibabu ya uwongo yenye kuonyesha minambari mikubwa mikubwa ya fedha unazotafuna.
Mapungufu makubwa katika matumizi ya fedha yaliyofanywa na Spika SITTA. Sitta aliwanyamazisha wajumbe wa kamati hiyo, ambapo aliwatishia kutowapatia posho na safari za nje kama wangeyafumua mapungufu yake hadharani! ,sitta alitoa rushwa!!
Sitta alipokuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha cha Uwekezaji nchini (TIC) alitumia nafasi hiyo kuingia ubia na wafanyabiashara wengi wa Kigeni.na ana hisa katika kampuni za kichina zinazodili na magogo .
Sitta amekalia tangi la petrol hivyo mikakati na vikwazo anajua siku wakubwa wakiudhika basi hana kazi nae atatumbukizwa kwenye shimo la ufisadi kwani kwa shutuma alizonazo kama ni za kweli au si za kweli atakwenda na maji.
 
MWIBA,

Haya mapya au ni yale yale....!?

Duh........Mkuu una jazba sana embu punguza munkari na ueleze kwa kituo tupate/nipate elewa.
 
Back
Top Bottom