Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,499
- 113,610
Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa. Leo niko Mbeya, hiki kibaridi cha Mbeya, kwa sisi tulio zoea mablangeti yale, hata ujifunike vipi, na blangeti zito kiasi gani, kibaridi bado kiko pale pale, kinapenya, unakisikia!, mpaka saa hizi uzingizi umegoma!, hivyo the best company na companion ni kushuka jf.
Huu mjadala wa IGA ya DPW na Bandari zetu, unatusaidia kwa mengi, sasa kuna watu wanaanza kuhoji serikali ya Tanganyika, wanataka serikali 3.
Hoja nyingine mjadala huu wa IGA ulizotusaidia ni hizi
Wazo kama hili nililileta humu kitambo, Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
Huku kuhoji hoji muungano kunakoibuliwa sasa na baadhi ya watu, nako sasa kunageuka ni kero ya muungano!, kwa maoni yangu, dawa ya pekee na tiba ya kweli ya kiuhakika na ya kudumu kutibu kero zote za Muungano, ni kwenda kwenye serikali moja!. Swali ni Je Tanzania sasa umefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?
Mimi ni mtu wa mastori mastori, kama wewe ni mtu wa short and clear, ishia hapa na ku jump kule kwenye conclusion, wale wa mastori tuendelee
Mastori ya Pasco
Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana ili iweje!
Kama nilivyosema kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, hakuna mkanganyiko wowote wa kimataifa kuhusu Tanzania.
Lakini Kitaifa kuna mkanganyiko wa katiba kati ya katiba ya JMT na katiba ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, ya mwaka 1977, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inaiita Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT!. Kitendo cha katiba ya Zanzibar kuuita Zanzibar ni nchi, kinawakanganya Watanzania kudhani kuwa nchi ya Tanganyika ndio pekee iliyokufa ila nchi ya Zanzibar ipo haikufa
Naomba niwahakikishie Tanzania ni nchi moja ya JMT, ile nchi inayotajwa na katiba ya Zanzibar kuwa ni nchi ya Zanzibar, sii kweli kuwa Zanzibar ni nchi, bali ni jina tuu, hayo mabadiliko ya katiba ya Zanzibar kujiita nchi, kimuungano ni mabadiko batili, ila, kwa vile mabadiliko hayo ni kwaajili ya Zanzibar tuu, na hayatambuliwi na katiba ya JMT, serikali ya JMT, imeamua kuyapuuza!, lakini kufuatia hizi kelele, tutapuuza mpaka lini?. Si ni bora twende kwenye serikali moja, haya yote yaishe?.
Conclusion
Kwa vile Rais Samia, anakwenda kutupatia katiba mpya, hili pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuzimaliza kero zote za muungano, ni kwenda kwenye serikali moja. Nimalizie na hili swali, je, Tanzania sasa mmefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?
Wasalaam,
Paskali.

- IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
- IGA ya DPW imetusaidia mambo mengi. Kwanza kuonyeshea tuna wanasheria wa aina gani, pili kuidogosha fani ya sheria na sasa kila mtu ni Mwanasheria?
- Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
Wazo kama hili nililileta humu kitambo, Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
Huku kuhoji hoji muungano kunakoibuliwa sasa na baadhi ya watu, nako sasa kunageuka ni kero ya muungano!, kwa maoni yangu, dawa ya pekee na tiba ya kweli ya kiuhakika na ya kudumu kutibu kero zote za Muungano, ni kwenda kwenye serikali moja!. Swali ni Je Tanzania sasa umefika wakati wa kutimiza ndoto ya Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, ya uzalendo wa kweli wa JMT, wa kwenda kwenye serikali moja?
Mimi ni mtu wa mastori mastori, kama wewe ni mtu wa short and clear, ishia hapa na ku jump kule kwenye conclusion, wale wa mastori tuendelee
Mastori ya Pasco
Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana ili iweje!
Mkanganyiko wa Katiba.Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale ya Mwanza ya 1976!.
Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!. Jee ndoto hii ya Mwalimu Nyerere, kwa Tanzania kuwa nchi moja ya JMT yenye serikali moja na rais mmoja, itakuja kutimia?.
Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutokana na hoja za mwana jf huyu kuhoji ilipo serikali ya Tanganyika.
Mkuu MKWEAMINAZI, kwanza kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako hili, kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.Mwaka 1964 nchi ya Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania.
Pili nikurekebishe hii opening statement yako ya "Mwaka 1964 nchi ya Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", it should be "Mwaka 1964 nchi iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, iliungana na nchi iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuzaa nchi ya Tanzania", kwasababu nchi hizi zote mbili sasa hazipo!.
Hii ni kweli, na ndicho kilichopo!. Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu muungano now, than any other times, kwasababu ni Mama Samia, ndiye aliyetoa ruhusa watu waachwe huru kujadili muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikilizaNilitarajia muungano ule ungezifuta nchi zote mbili yaani nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika ili kuwe na nchi moja tu ya Tanzania.
Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika, wala nchi ya Zanzibar, kilichopo ni nchi moja tuu ya Tanzania!. Zanzibar sio nchi!.Kinachoshangaza kwa muungano huu ni uwepo wa nchi ya Zanzibar na kutoweka kwa nchi ya Tanganyika.
Nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.Je kwanini nchi ya Tanganyika itoweke na nchi ya Zanzibar iwepo?
Zanzibar hii iliyopo sio nchi, ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani!.
Sii kweli nchi ya Tanzania iko kwenye ardhi ya iliyokuwa Tanganyika, nchi ya Tanzania ni eneo lote la iliyokuwa Tanganyika na eneo lote la iliyokuwa Zanzibar!.Kwanini nchi ya tanzania iwe kwenye ardhi ya nchi ya Tanganyika bila kuijumlisha ardhi ya nchi ya Zanzibar wakati udongo wa Tanganyika na Zanzibar ulichanganywa?
Na ni kufuatia kitendo kile cha kuchanganya udongo, ndio kuizi fuse nchi zote mbili kuwa nchi moja, hivyo muungano wetu ni muungano wa milele!, hauwezi kuvunjwa kwa namna yoyote, kwasababu ili kuuvunja huu muungano wetu adhimu, ni lazima kuuchukua ule udongo ulio changanywa na kuutenganishe, kitu ambacho haiwezekani!.
Ndio maana hata ule unaitwa ni mkataba wa muungano, The Articles of the Union between Tanganyika and Zanzibar, ule sio mkataba, ni makubaliano ya kuungana milele!, Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?
Hapana, Tanganyika ilibadili jina na kuwa Tanzania Bara, ila jina la Zanzibar lilibaki kwasababu ya utawala wake wa ndani tuu lakini Zanzibar sio nchi!.Au huu muungano ulikuwa wa kubadili jina la Tanganyika na kuwa tanzania maana jina la zanzibar lipo?
Usiendelee kuuliza tena, nchi ya Tanganyika haipo!, na nchi ya Zanzibar pia haipo, kilichopo ni nchi moja ya Tanzania!.Nauliza tena, Nchi ya tanganyika ipo wapi?
Elimu ya Uraia Kuhusu Muungano wetu adhimu!.
Duniani kuna miungano ya aina mbili Kuu,
1. Miungano ya union, nchi mbili au zaidi zinaungana kuunda nchi moja. Zile nchi zote zinakufa na inazaliwa nchi moja mpya.
2. Miungano ya federation, ni nchi mbili au zaidi zinaungana na kuunda nchi moja, ila zile nchi zote zinakuwa na serikali ya muungano, Federal Government na State Government, kila nchi ina utawala wake wa ndani.
Muungano wetu ni very unique, kwasababu ni muungano pekee duniani ambao on one side ni muungano wa union kwa nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT, at the same time ni muungano wa federation wenye serikali mbili.
Muungano wetu kimataifa ni muungano wa union, Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, yenye serikali moja ya JMT, chini ya rais mmoja wa JMT, ambaye ni head of state, head of the government and CinC.
Lakini Kitaifa, nchi ya Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, yenye katiba mbili, katiba ya JMT, na katiba ya Zanzibar, yenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya Zanzibar, SMZ, yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar