Ndugu yangu Mwiba, wakati mwingine huwa unanichekesha sana unapoamua kumwaga pumba kavu kavu.
Kosa jingine la Mwakiyembe kama bado mna matatizo ya kufahamu, ni lini alizungumza Shamhuna ? Ni lini Spika Sitta alisimamisha mambo hayo kuzungumzwa Bungeni ? Ni Lini Mwakiyembe alizungumza ,Je haoni kama alimdharau Spika kwa kuleta ushambenga wake wakati ulikwisha kupigwa stop ? Au ndio anapeleka ujumbe kuwa kuna vikao vya siri vinalifuatia suala hilo chini kwa chini maana Mwakiyembe ni CCM na Pinda mwenyewe alipoona maji makubwa alikwisha sema analirudisha kwa CCM ,hivyo akina Mwakiyembe wanaonyesha misuli yao ndani ya Chama ,hawa ni watu wa kigeugeu utawaona wanasema mpaka kipovu kinawatoka lakini hawana maana hata ya senti tano ,hawa ndio wanaotulizwa na mafisadi bungeni usione hoja siku hizi hazizungumzwi na badala yake wamerukia suala la Zanzibar si Nchi ,hivi hamshangai na kuwahoji akina Mwakiyembe yako wapi makali yao ya kuwabana mafisadi na Chama chake kinawawajibisha mafisadi ,yupo Lowasa na wengine asimamie waondoshwe kwenye Chama kwani wamekitia aibu na yeye si ndie aliekusanya ushahidi na mengine akayaficha atumie ushahidi huo kuwawajibisha waliohusika.Anaogopa kukosa adabu au sio?Nahisi mwiba ulikuwa wataka leta ajenda ingine kupitia hii.
Sioni kosa la Mwakyembe apo.
Isipokuwa ni yule mzenji kupewa kaazabu kumrudisha kwenye utimama na ajijue kuwa chochote asemacho anaongea kama nani na kina impact gani kwa jamii.
Ngoja uyo Shamhuna apate habari halafu usikie vitu vyake,mimi sipo na akina Shamhuna wala Mwakiyembe ,maana wote hao ni ndugu ila nashangaa kwa upande wangu kwa nini CCM Wahafidhina wamelivalia njuga suala hili nilitegemea CUF ndio wawe mstari wa mbele lakini kinyume chake,ndio saa ingine naona timu ya Butiama na Timu ya Wafidhina Kisiwa ndui bado zinapimana nguvu.Nahisi mwiba ulikuwa wataka leta ajenda ingine kupitia hii.
Sioni kosa la Mwakyembe apo.
Isipokuwa ni yule mzenji kupewa kaazabu kumrudisha kwenye utimama na ajijue kuwa chochote asemacho anaongea kama nani na kina impact gani kwa jamii.
Naona wachangiaji wengi wamejikita katika kuujadili Muungano kwa bias kwenye upande hasa wa kiuchumi na kisiasa.Nahoji hivi,ni kweli kuwa hakuna vitu vingine kama kijamii au/na kiusalama ambapo muungano huu una manufaa?Au ni kuwa the cons overweigh the pros.Sijaisoma thread yote,hivyo kama haya niliyoandka ni duplicate ya yaliyokwisha andikwa basi mtaniwia radhi.
SOVEREIGNTY AS RIGHT AND POWER
Sovereignty does not signify merely a certain degree or quantity of power, as if the extent to which a state is sovereign can be measured simply by calculating its relative military and economic power. Sovereignty signifies simultaneously a right to act and a power to act. There are cases where the power of a state to act is so confined and limited LIKE THE ISSUE OF FIFA AND OIC ZANZIBAR DONT HAVE THAT ONE ...that its sovereign right to act is rendered largely meaningless. Equally, there are times when the actual power of a state is so great that, although its sovereign right to use this power has not been formally acknowledged by others, it is tacitly recognized. These are extreme cases, however. Normally sovereignty means the possession of a right and power, and disputes about sovereignty are disputes about right and power.
Sovereignty manifests itself in different forms, and this largely accounts for the varying definitions that are given of it. Seen from one angle, the right and power of sovereignty is exercised over territory, and is akin to the right and power of possession or ownership of a potion of the Earth's surface. This ownership of territory includes in turn a right and power over all that exists, whether static or mobile, human or non-human, within the territory concerned, and extends to so-called territorial waters and airspace. Great Britain's claim to sovereignty over the Falkland Islands (Islas Malvinas) is a claim of ownership of this kind. Argentina denies Great Britain's right, claiming a prior right of her own. Argentina has attempted to give her right substance by challenging Great Britain's power in the Falklands War, but without success.
This is ridiculous. Zanzibar is semi autonomous, Tanzania is soverein and Tanganyika is non existent or impotent. I feel sick when i hear people ask this kind of question which has obvious answer.
Ana kesi ya kujibu mbele ya WaTanganyika iweje waTanganyika ? na Sio WaTanzania hivi unaelewa ya kwamba Tanganyika imezirai na Zanzibar bado inatuta ? Unaweza kukariri mstari ambao wewe unauona kuwa ni kweli tupu,halafu tuone kama Mwakyembe hakuvunja Katiba kwa kuzuia haki na kutaka Shamhuna asulubiwe ,maana ndivyo ilivyozoeleka ndani ya CCM ukisema ukweli unaitwa mhaini,unaitwa mpinzani unaonekana si mwenzetu ,unaekewa kikao na wafuata upepo wote wanakuzamisha kwa kuwa tu umepinga kauli,jamani mambo ya Ndio Mkuu yamepitwa na wakati wakuu wenyewe sasa hawajui hata dira ya Tanzania ilipoekea wanahitaji msaada wa hali ya juu na sio kila wanakotuongoza tuseme ndio huko huko mbele kwa mbele ,huu ni wakati wa kuekana sawa awe Raisi,Waziri Mkuu,au Waziri yeyote au kiongozi yeyote yule Jeshi au Polisi si wakati wa kunyamaziana na anapopingwa mtu wengine wakaruka na kusema unakosa adabu ,huna nidhamu ,kila mtu tapewa heshima yake na kuheshimiwa lakini linapokuja suala la kujadiliana hapo hapatakiwi usawa nani Mkuu nani mtawala nani mtawaliwa panatakiwa hoja kujadiliwa kupingwa kukosolewa isiwe akipingwa mtu aseme fulani inafaa adhibitiwe,inafaa achuliwe hatua ,inafaa aadhibiwe, ukisikia mtu anasema hivyo basi huyo ni adui wa haki tena ni mtu ambae inaonyesha ubaya wake upo ndani kwa ndani.
Shamhuna hana uhusiano na serikali ya Muungano wala CCM kama sikosei,ni kiongozi katika serikali ya Zanzibar ,hivyo alikuwa anawajibika kusema lolote iwe amesema alivyosema Pinda ni sahihi au alivyosema Pinda si sahihi ,natumai anayo haki hiyo ,sasa kilichowatonesha akina Mwakiyembe ni kwa nini Shamhuna amesema au ameipinga kauli ya Pinda hata kama kauli hiyo ilikwishatolewa maelezo lakini ifahamike ni wapi ilipotolewa maelezo ni Bungeni kwenye chombo cha Muungano na Shamhuna nae ametolea maelezo kwenye Baraza la wawakilishi Chombo chao huko Zanzibar ,kosa lipo wapi ? Bahati mbaya Shamhuna amesimamia Uzalendo wa Taifa lake na Katiba ya Zanzibar ambayo inatamka wazi Zanzibar ni nchi ,na yeye yupo sahihi zaidi kuliko Pinda kwani hakuna sehemu katika Katiba ya Muungano palipoandikwa Zanzibar si Nchi.
Jaribuni mnaposoma na kutoa hoja msiwe na jazba aidha kama wewe ni CCM hapo nitakuwa sina la kukufanya ,vilevile ukiwa ni Mtanganyika pia nitakuwa nakuangalia tu.Ila Kama unajihesabu ni Mtanzania basi itabidi uwe katika njia inayotakiwa kuwepo ,japo upo na Chama usijaribu kukilinda chama kinapokosea ni lazima ukiulize,ukihoji ili kupata maelezo na kama yanahitajika kupingwa basi usisite kupinga ,kuliko kuogopa kuambiwa unadharau au huna adabu ni aibu kwa DR>Mwakiyembe kusema maneno alisema ya fulani adhibitiwe au sijui atiwe adabu na wengine mnarukia na kumuona ni shujaa sijui kwa kigezo kipi.
Nani kakwambia kuwa Zanzibar ni Semi-Autonomous. Nenda katafute uzuri ni nini Semi Autonomous, na ivishe Zanzibar hapo -Jee inastahili kuitwa hivyo?
Na ni bora ulivyojitokeza ili upate msasa kidogo,tatizo mlilonalo Tanganyika mashuleni hamsomeshwi somo la historia ya Zanzibar na hata mkosomeshwa inakuwa kama mnapigwa burushi tu na meno yanaendelea kuoza.Habari wana jamiiforums. Nami ningependa kutoa maoni yangu kidogo kuhusu issue ya zanzibar. Mimi kwa upande wangu naona kuna vitu vya kuwekwa sawa. Kwanza kipindi kile cha kuunganisha hakuna mwananchi yeyote aliyeshirikishwa katika kuunganisha nchi hizi hivyo kuna watu especially Zanzibar ambao hawakuridhika na hiyo dhana na kwa mazingira yalivyouwa walikuwa hawaweza kusema kama wafanyavyo sasa. So cha kwanza uwekwe mchakato kama watu wanataka muungano ama la.
Pili ubinafsi ukiangalia kwa undani sana utaona ni kwa jinsi gani zanizibar inainyonya tanganyika maana tanganyika yenyewe ina kila kitu lakini imekaa kimya. Kuna mangapi ambayo wazanzibari walikuwa wanapata lakini watanganyika hawapati umeme, maji etc tena bure hapo kabla! Je huku bara watu wamewahi kupata umeme au maji bure? Acha huduma.
Tatu wanaona kuwa nguvu nyingi iko bara hivyo ili kuizuia hiyo watambulike wenyewe. Mfano mdogo hawa jamaa wa mpira ZFA na TFF nafikiri kila mtu alisikia ZFA inatakwa gawio lake la kutoka FIFA. Hiyo ni baada ya kujaribu kujiunga wakakataliwa kuwa wao si nchi haiwezekani nchi moja iwe na vyama viwili. Wanataka nusu kwa nusu. Je basis yao ni wapi? Maana haiwezekani zanzibar na tanganyika ziwe sawa.
Hivyo mimi kwa upande wangu kama kawaida ya wabara huwa hawarush kwenye maamuzi hivyo tuite kura ya maoni nani anataka muungano na kama unatakiwa then uwe wa aina gani ili kuondoa hivi vijineno vya hapa na pale.
Nawakilisha
Naona mmeshikilia sovereignty hivi hakuna neno la kiswahili ? Au mnaliepuka maana huenda tafsiri yake ikawagonganisha vichwa.Pakacha,
Baada ya kuungana na Tanganyika Zanzibar ilipoteza sovereignty yake. Ndio maana kiti chake katika UN kiliangukia chini ya Tanzania. Ndio maana ilipojiunga na OIC kinyemelea ililazimika kujiondoa baada ya jambo hilo kufahamika hadharani. Tatizo liko wapi?