Mbeba Maono
Senior Member
- Jun 24, 2008
- 108
- 7
kwani tatizo nini? ni kwasababu kule pemba ndo kuna mafuta sasa wapemba ndo wamiliki mafuta yale peke yao? mbona hata bara kuna mafuta kule pwani ya kusini wamegundua na jana tu wameona dalili kubwa sana ya mafuta kwenye bonde la ziwa Rukwa? kama vipi, waacheni wapemba walale mbele na mafuta yao, na sisi wabara tutalala mbele na vyetu tulivyopewa na Mungu. tatizo kubwa ambalo ni moja ya hata kimegeo kinachomega muungano ni mafuta ya pemba. Je, kama mafuta yasingekuwapo pemba na yakawepo bara tu, kungekuwa na misukosuko yote hiyo?, basi muungano wetu ni wa siku za faida tu, siku zisizo na faida ni ugomvi. tunachowang'ang'ania sana wazanzibar ni nini? kwani sisi wabara hatuna nini? tunakosa nini, tunafaidika nini na wao kama sio wao kufaidika na sisi zaidi? you think we need them more than they need us? No, I don't think so. let them take their way and go. watuache watanganyika vyovyote watakavyo tuita, na sisi tutachimba mafuta vilevile. period.