Mtuhumiwa ma mauaji ya Mwangosi afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali

Just curious, katika hii kesi polisi wanapeleleza nini ambacho hakijakamilika?

Inasikitisha sana Polisi mdogo huyo kutolewa kafara, ili kupunguza hasira ya Watanzania kwa uongozi wa Jeshi la Polisi, Kiutawala hamna askari mbaya, awe amevuta bangi, amebaka au ameua, ila kuna Kamanda mbovu asiyejua uwajibu wake wa kiutawala, uamrishaji (Rules of Engagement) hivyo kushindwa kusimamia nidhamu na utawala wa Askari walio chini yake. Hapa tusipigwe changa la macho lazima Makamanda wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Polisi Wawajibike?
 
huyo katolewa kama mbuzi wa kafara?? Kafa kwa manufaa ya wengine??
 
Mimi nadhani sas JF tubadilike na tusiwe watu wa kulalamika tu bila kuichukuwa action, bahati nzuri hapa tuna Members wa fani zote, tuna maengineer, Walimu, Wanasheria, Wabunge, Wanaharakati na wanahabari n:k

Ni aibu kama Watanzania tutakubali kufanywa mazuzu kwa viwango hivi, hii haikubaliki hata kidogo na kujaza comment zisizokuwa na solution ni wasting of time, naomba sasa twende mbele zaidi. Huu si wakati wa uhodari wa kubonyeza keyboard huku tunadhalauliwa kwa kiasi hiki na hawa hopeless na Failure Polisi halafu tunakaa kimya tu.

Tunataka kuona wote walioshiriki mauwaji haya akiwemo RPC wote waface Justice, nawapa reference mkumbuke Zombe akushiriki wala hakuwepo kwenye tukio la mauwaji lakini alitiwa pingu kwa sababu yeye ndio alitowa amri ya Mauwaji, swala la Zombe kushinda kesi ni hadithi nyingine ya uzembe wa makusudi kutokuwa na madpp wenye viwango.
 
Matola

HUU NI USANII YEYE ALITUMWA NA WATAWALA, HAPO WANATUPOTEZEA, KWANI WALIOTUMWA KUMUA IMRANI KOMBE SIPOWAPO MTAANI, CHENGA ZIKIENDELEA, MARA SI MIMI NILIYE TOA MSAMAHA WA KUACHIWA KWAO, SIYE WATANZANIA KWELI NI MAZEZETA, HIYO NI PICHA NYINGINE KAMA ILE YA KOVA NA KICHAA WA MKENYA ALIYE MUUMIZA DKT. ULIMBOKA.

Last edited by a moderator:
Inasikitisha sana Polisi mdogo huyo kutolewa kafara, ili kupunguza hasira ya Watanzania kwa uongozi wa Jeshi la Polisi, Kiutawala hamna askari mbaya, awe amevuta bangi, amebaka au ameua, ila kuna Kamanda mbovu asiyejua uwajibu wake wa kiutawala, uamrishaji (Rules of Engagement) hivyo kushindwa kusimamia nidhamu na utawala wa Askari walio chini yake. Hapa tusipigwe changa la macho lazima Makamanda wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Polisi Wawajibike?
Ur very wrong, sasa ndio wanapalilia hasira zetu na hili ndio tutalishikia bango mpaka wataomba ardhi ipasuke, hatukubaliani kabisa na kesi hii batili.
 
Inaoekana unataka kuchanganya mambo, kwa mtazamo wangu RPC ni mshitakiwa 2 ila yule askari aliyevunjwa mguu ndiye shahidi namba 1 ,wanasheria tuwekeni sawa .naomba kuwakilisha
Shahidi wa kwanza ingependeza awe RPC wa Iringa!

Ingependeza sana!
 
Hao wauaji wako Saba..bila kumsahau huyo askari kanzu ambaye wengi ni kama mnam-ignore. Yeye Kashika Bastola..huenda huyo dogo pacificus aliua kwa presha kwamba usipo-pull trigger nakupiga risasi.. AU labda ilikuwa Pacificus akikosa target yeye apige..Woooooote hao wanapaswa kufikishwa mbele ya sheria

ndio sababu nikasema walitakiwa kushitakiwa askari sita wanaoonekana kwenye picha wakimshambulia Mwangosi, nimemsamehe mmoja kwakuwa nimeona alikuwa akifanya jitihada za kumnusuru Mwangosi, ambaye atapaswa kuwa shahidi namba moja.
Lakini pia nimesema RPC Kamuhanda alipaswa kushitakiwa kwakuwa alikuwepo eneo la tukio wakati unyama huo unafanyika na alifahamishwa na waandishi wa habari ili amnusuru Mwangosi lakini hakufanya hivyo, inawezekana yeye ndiye alitoa amri ya kuua.
 
Mi nahisi huu ni usanii mwinginewa serikali legelege, naamini kabisa hii imefunguliwa ili watuzuge kuliongelia tena hili swala then kesi itapotea kimyaa. Kwani yule bwana aliyestakiwa kwa kumtesa Dk Uli kesi yake imeishia wapi? Kuna mtu anaiongelea tena? Hii ndio imekuwa njia ya serikali kupotezea issue kama hizi wanajua kwa kupeleka hii kesi mahakamani tayari wameshawafunga watz midomo
 
Sikubaliani kabisa na kesi hii ni batili, Wanaharakati wote wanapaswa kuipinga hii kesi maana ni kuwafanya Watanzania ni wapumbavu kuliko maelezo.

Daudi-Mwangosi.jpg

Mbele ya RPC huyo kijana amemlenga Mwangosi waziwazi huku wengine wakimsulubu marehemu. Wengine tuliopitia mafunzo ya kijeshi,nashangaa kwanini kamanda Kamuhanda hajakamatwa mpaka sasa kwasababu kama anadai hakutoa amri ya kuua,basi alikua na uwezo wa kuepusha tukio lile. Ashitakiwe kwa mauaji,uzembe na kutowajibika.
 
Askari anayetuhumiwa kumuua Daudi Mwangosi leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya mkoa wa Iringa na kusomewa mashitakata yake. Huku akiwa chini ya ulinzi mkali ambao ulifanya wanahabari waliofika mahakamani kujitahid kupata picha kwa ugumu.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya Daines lymo mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mtuhumiwa Pacificus Cleophase Simon (23

Source:
francisgodwin.blogspot.com/
 
September 12, 2012

BREAKING NEWssssssssMTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWAMAHAKAMANI LEO IRINGA

Baadhi ya wanahabari wakitoka mahakamani

Askari anayetuhumiwa kumuua Daudi Mwangosi leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya mkoa wa Iringa na kusomewa mashitakata yake. Huku akiwa chini ya ulinzi mkali ambao ulifanya wanahabari waliofika mahakamani kujitahid kupata picha kwa ugumu.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya Daines lymo mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mtuhumiwa Pacificus Cleophase Simon (23

HABARI KAMILI ITAKUJIA HIVI PUNDE

Huyu askari ni mtanzania ? Anastahili adhabu kali sana. Auae kwa upanga yampasa kuuwawa kwa upanga.
 
Uyu dogo ana 23 years naweza jua alianza aliajiriwa lini kujiunga na jeshi la polisi
Kuna hesabu nataka fanya apa......
 
Asante kwa taarifa. Tunaomba haki itendeke ili kurudisha imani ya wananchi kwa vyombo vya dola.
 
Mbele ya RPC huyo kijana amemlenga Mwangosi waziwazi huku wengine wakimsulubu marehemu. Wengine tuliopitia mafunzo ya kijeshi,nashangaa kwanini kamanda Kamuhanda hajakamatwa mpaka sasa kwasababu kama anadai hakutoa amri ya kuua,basi alikua na uwezo wa kuepusha tukio lile. Ashitakiwe kwa mauaji,uzembe na kutowajibika.
Kisheria huwa tunatowa na reference na reference nzuri ni kesi ya Zombe, Kamanda Zombe hakuwepo sehemu ya tukio la mauwaji lakini alikamatwa na kujumuishwa kwenye shtaka la mauwaji kwa sababu yeye alitoa amri ya mauwaji.

Sasa inashangaza huyu RPC Kamuhanda yeye pia alitowa amri ya mauwaji na alikuwepo eneo la mauwaji kushuhudia agizo lake linatekelezwa kisha ndio akatokomea, je ni kwa nini huyu asiwe mshitakiwa namba moja kwenye kesi hii ya mauwaji?
Hii haikubaliki na hatuwezi kuruhusu ujinga huu uendelee ndani ya Taifa letu.
 
Back
Top Bottom