Mtazamo wa CHADEMA juu ya Lema kujiingiza gerezani

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Mimi ni mwanachadema tangu 2005 na ninakipenda sana chama chetu makini CHADEMA. Kama wadau na wenye chama tunachukuliaje jambo alilofanya Mh. Lema kwa kukataa dhamana na kukubali kuingia gerezani?
 
Hii lazima itakula kwa polisi mkuu. Alichokifanya Lema hapa ni kuanika madudu ya polisi ya kubambikizia watu kesi na kutoa vitisho.
Kumbuka si watu wengi walikuwa na update za Zuberi na polisi wenzake Arusha, sasa tunajuwa kwa maelfu kama sio mamilioni kwamba polisi Arusha wameacha kukamata wezi badala yake wanatunga kesi na kukamata wanasiasa! Mwendo mdundo!
 
Mh amechoka na purukushani za siku na hawa jamaa wa usalama, hawa jamaa wanatakiwa waelewe kuwa huyu ni kiongozi wa watu na wanatakiwa kumheshimu kama hawo wengine wa ccm,shida ni chama alichopo tu, polisi wamejenga uhasama na chadema lakini kama watashindwa kusoma alama za nyakati watajikuta wakiwapigia saluti............! nawashauri wabadilike.
 
Mimi binafsi nadhani kama atakuwa kwenye mawazo yangu ndo mda muafaka wa kufanya utafiti makini kwa wale ambao wamebambikizwa kesi na wengine mda mrefu hawaja pata hukumu za kesi zao na kutoa hadharani kama waziri mambo ya ndani kivuli.
 
Hata Kama ni mimi ningekataa dhamana,kila siku kesi kisa nimetembea na miguu kuelekea ofisini kwangu?Alichofanya Lema ni sahihi kuuonyesha umma juu ya unyanyasaji huu mbovu kwa jeshi la polisi dhidi ya wananchi wake. Kesho watu wengi watalifahamu hili magazeti yatakapoandika juu ya hili na lazima watu(raia)watataka kujua chanzo ni nini.

Ninawalaani polisi kwa kukionea chama cha demokrasia na maendeleo Chadema hasa kwa kuwafungulia kesi nyingi Wabunge wake,na hichi wanachokipanda wategemee kukivuna pia.
 
Bora jamaa ameamua kupumzika lupango, maana serikali/polisi wamekuwa wakimsonga daily hata kushindwa kuwatumikia wananchi wake. Maana inatakiwa ajifiche na asiende ofisini.

Akitembea kwa miguu ni kufanya maandamano yasiyo na kibali, wananchi wakifika ofisini kwake ni mkutano usio halali.

Hata kama angekubali dhamana, kitendo cha kutoka hapo mahakamani angapatiwa kosa lingine. Bora alivyojipumzikia huko atapunguza ongezeko la kubambikiziwa makosa/mashitaka. MAFISADI WANAPETA TU NCHI HII.
 
Ni kitendo cha kishujaa ambacho kila mwenye uchungu na nchi hii anapaswa kufanya iwapo mazingira ya kufanya hivyo yatajitokeza kwake. Kufanya kwaajili ya kutetea haki itendeke.
 
Mm nampongeza maana amefanya jambo la kijasiri, wamezidi kumfuata fuata sana kuanzia mahakamani hadi akiwa ofisini.
 
akitaka anaweza kukaa huko miaisha yake yote..mbona jela nafasi ipo tu...amwombe hakimu amfunge tu

hataki dhamana naona anafurahia maisha ya jela
 
Mimi ni mwanachadema tangu 2005 na ninakipenda sana chama chetu makini chadema.kama wadau na wenye chama tunachukuliaje jambo alilofanya mh.lema kwa kukataa dhamana na kukubali kuingia gerezani?

Amekwenda kufanya revolution kisha anatoka acha magamba wafurahie ujinga wao watajuta
 
Kama mtu anatembea kuelekea ofisini na watu wanaamua kumfuata bila yeye kuwaita wala nini, utamlaumu vipi kwamba amefanya maandamano bila kibali? Bora afanye kazi nyingine akiwa huko mahabusu, maana atakuwa na muda wa kufanya utafiti kuhusu mbalimbali yahusuyo mahabusu, wafungwa na haki za binadamu magerezani.
 
Mimi ni mwanachadema tangu 2005 na ninakipenda sana chama chetu makini chadema.kama wadau na wenye chama tunachukuliaje jambo alilofanya mh.lema kwa kukataa dhamana na kukubali kuingia gerezani?

Anataka aone hali ya gerezani ikoje.
Mpigania haki lazima ulale jela
 
Unajua hii issue inachekesha sana, watu wakiuliza kaenda jela kwa kosa gani hakuna kosa yeye mwenyewe ndio kajipeleka kakataa dhamana..

Inabidi wakampime akili siku akitoka jela.

Lema sio mtu wa kwanza kushitakiwa muacheni akae jela hata miaka 10 manyampara watamtunza tu.

Watampa anachotaka

Kama Lema alijipeleka jela na amekataa dhamana Kama ulivyoandika hapa,hivi umeshajiuliza sababu ya yeye kukataa kuwekewa dhamana!!?.
 
wadau mkumbuke kuwa LEMA hakukamatwa peke yake
walikuwa wengi na dhamana wakapewa baadhi
wengine wakanyimwa ndipo walipoamua kwenda wote magereza

kamanda yuko sahihi kwani yeye ndio chanzo cha kukamatwa wenzake.
 
Mimi ni mwanachadema tangu 2005 na ninakipenda sana chama chetu makini CHADEMA. Kama wadau na wenye chama tunachukuliaje jambo alilofanya Mh. Lema kwa kukataa dhamana na kukubali kuingia gerezani?

Alichokifanya Lema ni kutuma ujumbe sehemu husika na nina hamini umeshafika.
God bless u Kamanda mpiganaji.

http://e
 
wadau mkumbuke kuwa LEMA hakukamatwa peke yake
walikuwa wengi na dhamana wakapewa baadhi
wengine wakanyimwa ndipo walipoamua kwenda wote magereza

kamanda yuko sahihi kwani yeye ndio chanzo cha kukamatwa wenzake.
sasa kama katoa uamuzi wa kwenda nao hao walionyimwa mdhamana ni wakati gani aliandika huo waraka?
 
Mimi ni mwanachadema tangu 2005 na ninakipenda sana chama chetu makini CHADEMA. Kama wadau na wenye chama tunachukuliaje jambo alilofanya Mh. Lema kwa kukataa dhamana na kukubali kuingia gerezani?

Hilo ni fundisho kwa Police wa Arusha maana wao huko wamezoe kupigana na wapinzani katika siasa wakasahau wananchi kuwa wana hitaji usalama wameshindwa mktamata Salim Ally anaye nyanyasa vibarua wake walio fanya kazi kwake zaidi ya miaka 5 bila kuajiri wana mkamata Lema kisa katoka mahakama akiongozana na wafuasi wa CDM na Police kumzushia maandamano hivi hii ni Police au ni kichaka cha watu kuvunja na kutishi rai amani na kuwa nyima haki au uhuru wa kujieleza au kutembea?

Jana nilikuwa napata news za UBS TV from Uganda ndicho kilicho mtokea Kiza Bhesije nae alikuwa anatoka kwake kwa miguu anakwenda mjini Police wakamwambia huruhusiwi kutembea kwa miguu ni bora atumia gari lake kisa ati atasababisha maandamano na vurugu sasa mtu anajitembelea watu wakimfuata nalo ni kosa kwani hawa Police wasijiulize wananchi wanancho kitaka ni kitu gani kwa Mtu kama Bhesije na Lema?

My Take;


Police wa Arusha ni shinikizo la kisiasa kutaka kuonyeshana ubabe na wana Arusha huku wakijua fika wananchi wa jimbo hilo wana support Mbunge wao katika kudai haki sasa sielewi Police na viongozi wa juu serikalini wao lao wanataka nini wananchi wawe mabubu katika kudai haki zao?

Police Uganda wao hawa ni vibaraka kabisa wa Museveni bila hata ya kujiuliza mara mbili hivi wana kampala wakitaka kumfua Bhesije kwa gari akiwa amepanda wananshindwaa hapana sasa ni nini shida hapo kwani Police mwatumiwa vibaya na Viongozi wa Juu serikalini kwa faida zao na sio za wananchiii wanan hawa hawa baadhi yao ndio walio wachagua kuiongoza serikali
 
Back
Top Bottom