Mtazamo wa CHADEMA juu ya Lema kujiingiza gerezani

kumbe lema aliyaona haya mapema
soma baadhi ya vifungu katika hotuba yake bungeni

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/158997-full-text-hotuba-ya-lema-bungeni.html

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inawataka Askari polisi wote wa nchi hii, wasikubali kutumiwa vibaya kukandamiza demokrasia na haki za wananchi, kwa maslahi ya kukibeba chama fulani cha siasa na badala yake watende haki kwa manufaa ya Watanzania wenzao. Wajue kuwa Watanzania wanaowafyatulia risasi, mabomu ya machozi na kuwapiga virungu, ni Watanzania wenzao. Ni sawa na Baba zao, Mama zao, Kaka zao au wadogo zao, kwa hiyo wasikubali kutumika vibaya kuua au kukandamiza ndugu zao. Badala ya kufanya hivyo, tunawashauri waishinikize serikali hii inayowatumia vibaya, iboreshe mishahara na maslahi yao
 
Alichokifanya Lema ni kutuma ujumbe sehemu husika na nina hamini umeshafika.
God bless u Kamanda mpiganaji.
Suala hapa ni kuwa wakubwa walidhani lema anaogopa jela kwa hiyo wakaamua kimfungulia kesi za ajabuajabu. Hii ni strategy ya magamba na polisi wao kwa miaka mingi ili Mh akose muda wa kushughulikia matatizo ya wananchi waje kichukua jimbo kiulaini.

Tanzania kuna tatizo ambalo wananchi mpaka wasomi hawajaliona, ukisema na kifanya ya ukweli basi wewe ni mbaya..

Ukiwa mdanganyaji basi wewe ni mwema. Ukitaka uwatetee basi unatafuta sifa... Hii nchi ni hatari na itachukua muda kuja kupata demokrasia ya kweli.
 
Mimi nasema LEMA ni shujaa na mpiganaji hasa,Polisi wamekuwa wakitumiwa kisiasa na chama cha wakoloni weusi CCM kukandamiza upinzani,Polisi kimekuwa chombo cha kisiasa,uonevu,dhuruma kwao ndiyo vimejaa.
 
wadau mkumbuke kuwa LEMA hakukamatwa peke yake
walikuwa wengi na dhamana wakapewa baadhi
wengine wakanyimwa ndipo walipoamua kwenda wote magereza

kamanda yuko sahihi kwani yeye ndio chanzo cha kukamatwa wenzake.

sikumbuki kama kuna alie kosa mdhamini vijana wote 19 waliwekewa mdhamana
 
Tarehe 14 Novemba anatajarajiwa kurejea mahakamani tena sijui atakataa tena dhamana
 
Tatizo la Polisi wetu wanashindwa kuelewa kuwa wapo kwa ajili ya wananchi wote wa TANZANIA na sio kwa ajili ya chama CCM. Hawajue weledi wao wa kazi wapo kimaslai ya CCM na si kuwatumilia wananchi kama inavyo wapaswa kufanya.

Kingine huu mtindo wa kumbambika kesi upo sana yaani Tanzania nzima polisi waha haka kamchezo ka kubambika kesi sasa kwa wale mbavu mbili kama mie hatuna uwezo wa kuwahonga kwani imekuwa ndio ratiba yao kuingia bure kutoka kwa hela, na ukifanya uchunguzi kwa undani sio wote waliofungwa ni wakosaji wengi wao 70% wamebambikiwa kesi.

Alichokifanya Lema ni sahihi kwa huyo OCD hajui wajibu wake wa kazi hii nchi tumepewa uhuru na wakoloni takriban miaka 50 hakuna seria inyomkataza mtu kutembea kwa miguu ama kufanya mkutano na wafanyakazi wake akiwa ofisini kwake ni kosa basi mbona maofisi yote tungekamatwa maana hatuombi vibali polisi kufanya vikao ndani ya ofisi tukiwa ofisini.

Najua Lema akiwa ndani atagundua madudu mengi sana ya polisi na serikali yao.

VIVA LEMA VIVA CDM MAPAMBANO YANAENDELEA!!
 
sikumbuki kama kuna alie kosa mdhamini vijana wote 19 waliwekewa mdhamana

Washtakiwa 7 tu ndio waliweza kukidhi matakwa ya dhamana na kuachia huru.

tarehe 14 sijui atakataa tena dhamana
 
Nimesoma kitabu cha Nelson Mandela cha ‘THE LONG WALK TO FREEDOM – Ni kitabu kikubwa sana. Tukio kubwa ktk kitabu hicho ni Mandela kukamatwa na polisi wa makaburu kwa tuhuma za kuongoza mapambano na maandamano ya kudai haki na usawa dhidi ya makaburu
Mandela anasimulia, baada ya kukamatwa nilipewa chaguo rahisi sana, kati ya kukana na kusitisha harakati za kupinga makaburu kisha niachwe huru au nigome kufanya hivyo nipelekwe jela kabisa. Akaelezwa hayo –na yeye alijua, jela kuna mawili, unaweza kufa kama wenzako (waliomtangulia wakafa) au ukateseka muda mrefu.
Mandela aliwajibu mahakamani bila woga, mkiniachia tu, nikishatoka nje ya kizingiti cha mlango wa mahakama hii, naanza harakati za kudai haki - alichagua chaguo la pili – Kwenda jela bila kujali kama anaenda kufa kama wenzake au ateseke muda mrefu. Kwake hilo lilikuwa chaguo rahisi sana. Mandela kama Lema hakutaka kuwadanganya makaburu wamwachie huru ili aendeleze harakati kwa siri au porini. Alijitoa mhanga hadharani na mahakamani kama Lema. Makaburu wakamsweka jela miaka 27. Aliwaambia, kwangu mimi, heri kufa kuliko kuwa mtumwa wa makaburu ndani ya nchi yangu. Sina sababu ya kuishi kama waafrika wenzangu hawana uhuru na Mateso haya yote yana mwisho, nisipoona mimi mwisho wake watoto au wajukuu zetu wataona. Mandela akaona matunda ya mapmbano yake miaka 27 baada ya kutoka jela.

Lema kama Mandela anasema, na nukuu waraka wake

Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasa bila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.

Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU

Binafsi nimeumizwa sana na tukio la Lema kwenda mahabusu bila kosa, Lema analalamikia jeshi la polisi kutumika kisiasa. Amegomea dhamana ama alikosa kwangu mimi siyo hoja. Hoja ya maana ni uonevu wanaofanyiwa watu wa Arusha.

Komredi Lema anauliza, maandamano yake toka mahakamani yanatofautianaje na yale ya UVCCM Arusha? hakuna jibu, Anahoji yale maandamano ya Ole Sendeka toka mahakamani akisindikizwa na washabiki wake, yanatofautianaje na haya ya Lema? Jibu halipo.

Halafu na sisi wengine tujilize, watu zaidi ya 200 hadi 500 wanaondokaje wote mahakamani kwa pamoja kesi inapoisha halafu usiite hayo ni maandamano? Je, tuwalazimishe waondoke mmoja mmoja ili isionekane ni maandamano? Kuna sheria ya namna hiyo? Kama ipo, ni kwa Chadema tu? Haiwahusu Ole Sendeka na UVCCM?

Mimi kama Lema najiuliza, utawekewa dhamana mpaka lini kwa kesi ambayo unajua haipo? Si afadhali uende huko ambako wanakutishia ili wajue kuwa uvumilivu wako na uvumilivu wa wananchi umefika mwisho? Si inabidi wajue kwamba Jela haiogopwi mbele ya haki?
Hii tishio la kukamata na kuwatoa kwa dhamana viongozi wa Chadema inatofautianaje na tishio la Makaburu kwa Mandela na wenzake? Hivi Lema, Dr Slaa, Mbowe, Ndesamburo nk ambao wamesha lala mahabusu wanakosa gani kama siyo ukaburu wa ccm?
Nini mwisho wa yote haya? Hata hivyo, pamoja na yote haya, Mimi kama Martin Luther King naona mwanga mbele ya Safari. Naona ccm ikifa kifo cha mende kama makaburu wa Mandela. Ninawaombea Lema, Dr Slaa, Mbowe, Ndesamburo nk ambao wamekwisha lala mahabusu bila kosa waone siku hiyo – wasikose kama Martin Luther king ambaye ndoto yake imetimia mpaka mweusi ( obama kuwa Rais) wakati yeye hayupo.

Aluta Continua.
 
  • Thanks
Reactions: Lua
Mh . Lema hajapenda kunyanyaswa ndio maan kila kiongozi anyanganywe gari lake halafu tuone akitembea kwa mguu tu ni maandamano ama kweli falsafa ya mandamano imekwisha SO watanzania wote wanaoenda katika shughuli zake za maisha ni maanadamano hakika Hivi JK yupo hapa nchini na anafurahia hilo BORA LOWASA angesema ujinga huo uishe lakini Mpemba mlietuletea hapa haelewi kitu hata kova mwenyewe anamshinda
 
kumbe lema aliyaona haya mapema
soma baadhi ya vifungu katika hotuba yake bungeni

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/158997-full-text-hotuba-ya-lema-bungeni.html

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inawataka Askari polisi wote wa nchi hii, wasikubali kutumiwa vibaya kukandamiza demokrasia na haki za wananchi, kwa maslahi ya kukibeba chama fulani cha siasa na badala yake watende haki kwa manufaa ya Watanzania wenzao. Wajue kuwa Watanzania wanaowafyatulia risasi, mabomu ya machozi na kuwapiga virungu, ni Watanzania wenzao. Ni sawa na Baba zao, Mama zao, Kaka zao au wadogo zao, kwa hiyo wasikubali kutumika vibaya kuua au kukandamiza ndugu zao. Badala ya kufanya hivyo, tunawashauri waishinikize serikali hii inayowatumia vibaya, iboreshe mishahara na maslahi yao

Police wetu they dont give a Damn about Hotuba ya Lema wao always they do obey Commanding orders from big Boss period
 
wana jf tujue kuwa police wa Arusha ni sehemu ya chama tawala sio kwa manufaa ya wananchi au serikali.
 
Nimesoma kitabu cha Nelson Mandela cha ‘THE LONG WALK TO FREEDOM – Ni kitabu kikubwa sana. Tukio kubwa ktk kitabu hicho ni Mandela kukamatwa na polisi wa makaburu kwa tuhuma za kuongoza mapambano na maandamano ya kudai haki na usawa dhidi ya makaburu
Mandela anasimulia, baada ya kukamatwa nilipewa chaguo rahisi sana, kati ya kukana na kusitisha harakati za kupinga makaburu kisha niachwe huru au nigome kufanya hivyo nipelekwe jela kabisa. Akaelezwa hayo –na yeye alijua, jela kuna mawili, unaweza kufa kama wenzako (waliomtangulia wakafa) au ukateseka muda mrefu.
Mandela aliwajibu mahakamani bila woga, mkiniachia tu, nikishatoka nje ya kizingiti cha mlango wa mahakama hii, naanza harakati za kudai haki - alichagua chaguo la pili – Kwenda jela bila kujali kama anaenda kufa kama wenzake au ateseke muda mrefu. Kwake hilo lilikuwa chaguo rahisi sana. Mandela kama Lema hakutaka kuwadanganya makaburu wamwachie huru ili aendeleze harakati kwa siri au porini. Alijitoa mhanga hadharani na mahakamani kama Lema. Makaburu wakamsweka jela miaka 27. Aliwaambia, kwangu mimi, heri kufa kuliko kuwa mtumwa wa makaburu ndani ya nchi yangu. Sina sababu ya kuishi kama waafrika wenzangu hawana uhuru na Mateso haya yote yana mwisho, nisipoona mimi mwisho wake watoto au wajukuu zetu wataona. Mandela akaona matunda ya mapmbano yake miaka 27 baada ya kutoka jela.

Lema kama Mandela anasema, na nukuu waraka wake

Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasa bila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.

Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ," JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU

Binafsi nimeumizwa sana na tukio la Lema kwenda mahabusu bila kosa, Lema analalamikia jeshi la polisi kutumika kisiasa. Amegomea dhamana ama alikosa kwangu mimi siyo hoja. Hoja ya maana ni uonevu wanaofanyiwa watu wa Arusha.

Komredi Lema anauliza, maandamano yake toka mahakamani yanatofautianaje na yale ya UVCCM Arusha? hakuna jibu, Anahoji yale maandamano ya Ole Sendeka toka mahakamani akisindikizwa na washabiki wake, yanatofautianaje na haya ya Lema? Jibu halipo.

Halafu na sisi wengine tujilize, watu zaidi ya 200 hadi 500 wanaondokaje wote mahakamani kwa pamoja kesi inapoisha halafu usiite hayo ni maandamano? Je, tuwalazimishe waondoke mmoja mmoja ili isionekane ni maandamano? Kuna sheria ya namna hiyo? Kama ipo, ni kwa Chadema tu? Haiwahusu Ole Sendeka na UVCCM?

Mimi kama Lema najiuliza, utawekewa dhamana mpaka lini kwa kesi ambayo unajua haipo? Si afadhali uende huko ambako wanakutishia ili wajue kuwa uvumilivu wako na uvumilivu wa wananchi umefika mwisho? Si inabidi wajue kwamba Jela haiogopwi mbele ya haki?
Hii tishio la kukamata na kuwatoa kwa dhamana viongozi wa Chadema inatofautianaje na tishio la Makaburu kwa Mandela na wenzake? Hivi Lema, Dr Slaa, Mbowe, Ndesamburo nk ambao wamesha lala mahabusu wanakosa gani kama siyo ukaburu wa ccm?
Nini mwisho wa yote haya? Hata hivyo, pamoja na yote haya, Mimi kama Martin Luther King naona mwanga mbele ya Safari. Naona ccm ikifa kifo cha mende kama makaburu wa Mandela. Ninawaombea Lema, Dr Slaa, Mbowe, Ndesamburo nk ambao wamekwisha lala mahabusu bila kosa waone siku hiyo – wasikose kama Martin Luther king ambaye ndoto yake imetimia mpaka mweusi ( obama kuwa Rais) wakati yeye hayupo.

Aluta Continua.

Freedom Is Cuming Tomorrow!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu ulicho kisema ni sawa kabisa me ntabase Upande wa UVCCM arusha ni kama 3 weeks zilizo pita Police wao hao hao walikili kuwa UVCCM kufanya shughuri zao za kuzindua mashina yao hapo arusha mjini kwenye baadhi ya vitongoji walikuwa na escort ya police na wakawa na mikutano yao ya ndani na Police walikuwa mashaahidi, Baada ya siku mbili Mbele Police wakatoa tamko lao kuwa M/Kiti wa UVCCM mkoa alitoa maneno ya kashifa kwa Ridhwan Kikwete na Police wakaongezea kuwa UVCCM waliandaa Mkutano bila Kibari cha Police.

Hili lilipelekea Tafrani katika mji huo wa Arusha kwa walio shuhudia wakajiuliza mbona police walikuwepo iweje leo OCD usema hakukuwa na kibali chochote kuhusu kulinda usalama wa raia wakati UVCCM wakiendelea na shughuri zao za uzinduzi wa mashina?

Police wanakinzana wao kwa wao tunaamini sasa Police ya Arusha ina makundi kuna wanao support upande kuli na wanao supoort upande wa Kushoto.

James Millya alijisalimisha Police na mpaka leo hatuja sikia hiyo kesi na ndivyo ilivyo tokea kwa Lema Police walikwenda mpka office kwa Lema wakamwambia uko chini ya ulinzi na akawasiliana na OCD akaambiwa aende police kujadili na kufika police ndio wakambia uko chini ya ulinzi kwa kuandaa maandamano na kufunguliwa shitaka sasa hapo ukijiuliza hiki kizungu mkuti cha Police kubagua Raia huyu ndie anastahili kosa fulani na huyu astahili kosa fulani linatokea wapi na kwa nguvu ipi? Police ya kwetu na waandiushi wa habari hawajatupa mkanda halisia ya nini kilikuwa chanzo kamili ni fitana na je wao waandishi wa habari wanaona ni HAKI inatendeka au na wao kama watoa taarifa kwa jamiii ni wana fuata order semeni hiki kwa kutishiwa au?

Mfano mzuri ni Media ya Uganda jana iliweka wazi Police alimwambia Kiza Bhesije kuwa hurusiwi kutembea kwa miguu kutoka kwako kwani kutembea kwake kungeweza sababisha machafuko njiani ya kuwa watu watamfuata na Bhesije akawelwa ndani kizuizini kwa takribani masaa yasiyo pungua masaa 24 na akaachiliwa huru hakuhukumiwa kwa kesi yoyote bali aliambiwa akirudia tukio hilo tena basi atafunguliwa mashitaka sasa hapo nashindwa tambua hawa police wao ni vibaraka wa viongozi ndio wao wanao lipa kodi ya nchi hii pekeyao au ni raia?
Nac
hosema hapo no kuwa media ya uganda at least ilionyesha kitu ila hapa Media zetu hazikufafanua wala kuonyesha chochote cha Lema kilicho jili huko Arusha.

My Take;
Police kwa hali hii mwaandika historia mbaya ya kidemokrasia katika uso wa Dunia kuhusu siasa za vyama vingi Tanzania
 
Yale yale ya Byesige na Museveni. Sasa kama kutembea kwa miguu ni kosa la jinai naona sis wote tutaishia jela na watabakia tu wezi wetu walio na mashangingi. Kosa namba (1) njama za kutenda kosa. Kosa (ii) kusanyiko lisilo halali. Naona wangaliongezea kosa (iii) kupumua bila ruhusa ya polisi. Hivi CCM wanatupeleka wapi kutumia vyombo vya dola kama mali ya chama? Tunajua wanaendelea kuumbuka kisiasa kila kukicha lakini wasituleteee frustration zao kunajisi demokrasia. Kama hawaamini ya Musa (Libya) wasubiri ya Firauni (?)
 
Polisi wa Arusha wako wako tu.Wakiambiwa lamba boot wanalamba bila kujua wajibu wao kwa raia na viongozi ni nini. Inabidi polisi waelimishwe maana ya maanadamno na mkutano ni nini. Shule hakuna , wanajifanyia hovyo hovyo tu kama serikali yao ilivyo hovyo hovyo.
 
Anatafuta sifa, we si unajua tena magwanda, wakianza kupwaya basi lazima waje na mpya, au ndio mlishasahau ya Mbowe kuletwa na ndege, wenje kutolewa bungeni, zitto kukataa posho. haya yote yametokea hivi karibuni.

Tunamsubiri sugu aka mr 2 aka muheshimiwa aka 2 proud na yeye aje na lake maana naona watu wake pia wameshaanza kugundua kuwa ni mzigo.
Mkuu ina maana Sugu sio moto chini tena? Nalog off
 
tusujidanganye kuwa nchi yetu ni ya utulivu na amani hilihali wananchi wake wamejawa na hasira mioyoni mwao. tafsiri ya amani si kwa kumwangalia mtu usoni ila moyoni mwake anafikiria nini. matendo kama haya yanayofanywa na jeshi la polisi hususani wa arusha mpaka kufikia kuita raia panya, maneno aliyoyatumia Ghadafi kwa wananchi wake na akaishia kukumbilia kwenye calvat na kukamatwa kama MBwa. wanayatenda haya kwa amri za wakubwa wao lakini wajue ya kwamba bomu wanalotengeneza siku linalipuka hakutakalika. wanaounga mkono hali kama hii ya uonevu na ukandamizaji ndani ya nchi yao hakika si wazalendo wala si sio wapigania haki ya kweli. Ni wanafiki na vibaraka ndani ya nchi yao. Ukiona kijana anashabikia na kuunga mkono hali kama hii hafai kusikilizwa. WAJUE YA KWAMBA THERE IS NO SITUATION WHICH IS PARMANENT iko siku na wao watakua upande wetu. Kila kitu kina mwisho. hali hii isitukoseshe nguvu wala isitufunge midomo Lema kaonyesha njia na sisi wapenda haki tummunge mkono.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom