Msomi anapokuwa mwanasiasa

Mkuu hapo nakubaliana nawe.Tunao wasomi kibao ambao ni "watukuka" katika taaluma zao lakini toka waingie ndani ya siasa(si-hasa) wamekuwa ndivyo sivyo!Kwa maoni yangu watu wangejikita katika taaluma zao hata kama hazilipi haraka kama siasa ambayo baadaye huwadhalilisha sana.
Mfano Prof.Sarungi kafikia hatua ya kudhalilishana na wapinzani wake kule Rorya,aibu iliyoje!

Mkuu,
Kumbe SIASA inamaanisha SI-HASA?
Kazi kweli kweli.
 
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?


Kwa mwendo huo hatutafanikiwa kwa sababu wanasiasa nao wameanza kuwa wasomi. Angalia mama Nagu, Mzindakaya, Nchimbi na risti inaendelea.
 
Back
Top Bottom