Ili tuendelee, tunatakiwa kwenda hivi

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Ili kuleta maendeleo ya kweli,napendekeza yafuatayo:-

1.Tubadilishe mfumo wa ajira ili watu wengi wavutiwe na ajira za kwenye sekta za kilimo,afya na elimu.

Ifike mahala mtu aone kuwa mwanasiasa hailipi kama kuwa mkulima au mwalimu tofauti na sasa ambapo watu,pamoja na taaluma walizonazo, wanaona kuwa Mbunge ni dili.

Ili mpango huu ufanikiwe,ni lazima Serikali ije na sera ya kuifanya siasa ionekane ni ajira ya watu waliokosa ajira zingine.

Kwa mfano,hivi inashindikana vipi kutengeneza mfumo wetu wa bunge tukaachana na mifumo ya Magharibi?

Kwa nini wabunge wasiajiriwe kupitia usaili unaozingatia taaluma na kuajiriwa mojakwa moja kwa kulipwa mshahara ili Bunge liwepo muda wote kwa kupishana sekta kwa sekta kulingana na mpangilio wa hoja zinazotakiwa kujadiliwa kwa wakati husika?

Hapa nina maana kuwa,kama hoja iliyopo ni kutunga sheria,basi wabunge wa sekta ya sheria tu ndio wakutane na wawe na Spika wao na wote wawe Wanasheria.

Vivyo hivyo kwa sekta zingine.
Kwa mantiki hii, kwanza tutaweza kufyonza wasomi wengi wanaozagaa mitaani bila ajira.

Pili,maamuzi yatakayotokana na wataalamu hawa yatakuwa na tija zaidi tofauti na sasa ambapo hata yule aliyeandika matusi kwenye mtihani ana nafasi ya kwenda kututungia sheria,achilia mbali kutumbua mamilioni ya pesa zetu.

Najua wengine hawatapendezwa na mawazo kama haya,lakini hata kama utekelezaji wake utachukua miongo kadhaa, bado haiondoi ukweli kwamba mfumo wetu wa ajira inaua taaluma zingine kwa kutoziwekea mazingira mazuri ya kuvutia ikiwemo maslahi bora.
Au mliosoma Cuba mnasemaje?
 
Upo sahihi Sana.
 
Mkuu bila kujikita kwenye maeneo mengine ya hoja zako. Ukweli ni kuwa hakuna Sheria yoyote inatungwa na bunge, hilo bunge ni rubber stamp wa Sheria zinazotungwa na serekali. Ukiona Kuna mabadiliko kwenye mswaada uliopelekwa na serekali bungeni, basi ujue ni Yale yaliyosahauliwa na serekali hivyo yanajaziwa tu. Hakuna kinachotakiwa na serekali bunge hili likapinga.
 
Back
Top Bottom