Hofu ya maamuzi inakwamisha maendeleo ya wasomi

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
"Hakuna watu waoga katika kufanya maamuzi kama watu wenye elimu, muda mwingine hujichelewesha wenyewe kwa sababu ya uoga". anasema Ulimbaga Mwalupufu Mwalimu wa sekondari mkoani Mbeya.

Mwalupufu anasema wasomi wengi wamekuwa waoga kufanya maamuzi hutumia muda mrefu kufanya tathmini kwa kila jambo kabla ya kulifanya na muda mwingine hujichelewesha na kudumaza maendeleo yao.

Anachukulia mfano wa vijana wa zamani walivyokuwa na maamuzi ya haraka kama vile maamuzi ya kuoa, tofauti na vijana wa siku hizi ambao wengi wao wana elimu na uelewe mkubwa huanza kupiga hesabu maisha ya ndoa yatakavyokuwa hivyo huogopa na kuchelewa kuoa.

"Mtu asiye na elimu anaweza kufanya jambo kwa haraka pasipo hata kuhitaji muda wa tathmini lakini huwa inatokea bahati jambo hilo likafanikiwa na kumfaidisha hivyo kumpa maendeleo".

Anabainisha kuwa usomi huleta hofu ya kufanya mambo kwa haraka ndio maana ni wasomi wachache walio matajiri lakini asilimia kubwa ya watu wenye utajiri ni wasiosoma.

Kauli hii inaungwa mkono na mtazamo wa jumla wa jamii kuwa wasomi ni watu wenye hofu inayowatenga na fursa za jamii.

Mtazamo huu unabainisha wasomi kama watu wenye kuchagua kazi kwa sababu ya hofu ya kutazamwa na watu juu ya kazi husika na kutojihusiha na baadhi ya kazi kwa hofu ya kupata hasara.

Hofu hiyo hugeuka kikwazo cha mafanikio yao mwisho hupelekea kudumaa kwa maendeleo yao.

Je wewe ni msomi, una mtazamo gani kuhusu mjadala huu?

Peter Mwaihola
Photo_1704990872386.jpg
 
Back
Top Bottom