Esperance
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 364
- 84
Hamjambo wana Jamvi la MMU, nimepotea kidogo afya inasumbua na hii hali yangu. Leo nimepata kisa cha kusikitisha sana. Kuna mama mmoja ameolewa na watoto 2. Sasa wameanza ujenzi na mume wake, katika pitapita mafundi wamemwambia mumewe anaendaga site na binti ana watoto wadogo 2 na wanamwitaga baba. Katika uchunguzi inaonekana mumewe ana nyumba ndgo. Kumuuliza akamjibu lazima wapajue kuna leo na kesho,ndio ni watoto wangu. Mama wa watu keshainvest karibia robo tatu ya nyumba. Na mumewe kila siku analalamika hana pesa mama akipata anatupia mjengoni pamoja na mikopo. Mama keshakuwa frastruted anahama makanisa, keshatishia kujiua mara 2. Msaada wapendwa imeniuma sana.