Mama wa watoto wako ameishikilia hatma yako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
MAMA WA WATOTO WAKO AMEISHIKILIA HATMA YAKO!​

Anaandika, Robert Heriel
Shahidi.


Ujumbe huu ni Kwa Watibeli, wanaume na Wanawake wanaohitaji kuishi Kwa furaha katika Ulimwengu huu.

Unapochagua MKE sio tuu unachagua Kiburudisho cha kukupa utamu kila usikiapo hamu ya ngono.
Mke ni zaidi ya Kiburudisho. Mke ndiye atakayeamua HATMA ya Maisha yako, Hii ni Kwa sababu kuwa Jukumu kuu la MKE ni USAIDIZI; sasa anaweza kukusaidia kuangamia na kukuangusha kwenye shimo refu la mateso wewe na kizazi chako chote. Au anaweza kukusaidia kukufanya uwe na future njema wewe na kizazi chako.

Mke ni Mama wa watoto wako. Hivyo Wakati unamchukulia kama MKE wako usisahau kuwa huyo ni Mama wa Watoto wako. Hivyo pamoja na kujifikiria wewe lazima pia uwafikirie Watoto watakaoletwa na huyo Mwanamke.

Je Watoto wako watakushukuru kumchagua huyo Mwanamke kama Mama Yao. Je anavigezo vya ku-rise kizazi Bora?

Elewa kuwa hata mwanaume uwe Bora vipi lakini endapo utachagua MKE au Mama wa watoto asiye na Sifa njema basi future yako Ipo matatani. Hakuna future pasipo uzao, hakuna HATMA njema pasipo kuwa na uzao Mwema. Na uzao lazima uhusishe Mwanamke ambao kazi Yao ni kuzaa na kufanya Malezi.

Elewa kuwa Mkeo au Mama Watoto wako ananguvu katika mambo yafuatayo;

1. Mwalimu
Fikiria Watoto wako wafundishwe na Mwalimu mpumbavu, mwalimu asiye na contents, asiyejua maadili ya ualimu. Unafikiri mtoto wako atakuwaje? Wanasema ukimuona mwanafunzi anafanya vizuri au vibaya basi mtafute mwalimu wake. Mkeo ndiye Mwalimu namba moja Kwa Watoto wako.

Ni lazima uchague Mwanamke mwenye good attitude (mtazamo chanya) mwenye Maadili, anayejua nafasi yake kama Mwanamke, MKE na Mama, Mwanamke mchapakazi na anayejua kufundisha Watoto kazi.
Ukiona Watoto hawamheshimu Baba Yao, tambua kuwa hapo mwenye tatizo sio Watoto Bali ni Mama Yao.

2. Mwombezi

Mwanamke au Mama wa watoto wako lazima awe MTU wa ibada kulingana na Imani na Dini zenu.
Lazima uoe Mwanamke mwenye uwezo wa kukuombea Kwa dhati yote.
Inafahamika kuwa Wanaume ndio wenye Bahati lakini bahati zao mara nyingi zinabustiwa na Maombi ya Wake zao.

Ukipata Mwanamke mwombaji Kwa dhati, tambua huyo anafaa Sana kwenye Future yako. Faida ya kuwa na mwanamke mwenye imani na mwombezi;

I) Sio mlalamishi Bali ni MTU wa kushukuru.
Hii ni Kwa sababu anajua kuwa mtoaji na mpaji ni Mungu mwenyezi. Ni Muelewa pale utakapomuambia hujapata Pesa, na atashukuru hata Kwa kidogo utakachompatia. Mwanamke asiyemlalamishi na mwenye shukrani atakuzalia Watoto wenye shukrani na wasio walalamishi. Kwani atawafundisha kumuomba Mungu na kumshukuru.

Lakini ukioa haya magarasha, tegemea malalamiko yasiyoisha, tegemea mikosi isiyoisha, tegemea kuzaa mitoto isiyo na shukrani, isiyoona jitihada zako. Future yako itakuwa Mbaya kivyovyote tu.

ii) Atakuwa mfariji
Mwanamke mwombaji siku zote ni mfariji, atakutia moyo miaka mia.

iii) Ni mlinzi wa bahati na Nyota yako
Mkeo na Mama wa watoto wako ni mlinzi wa Nyota yako, na hapa nazungumzia Mwanamke mwombaji, mwenye Maadili. Sio hawa vikuranjia, Mwanamke Malaya au Kahaba hajawahi kuleta bahati njema ndani ya nyumba. Na hapa nazungumzia Mwanamke anayelala wanaume zaidi ya mmoja.

Ukitaka kuchafua bahati au riziki yako basi tembea na Malaya. Unaweza ukafanya uchunguzi. Unaweza ukapata Pesa lakini mara Baada ya Kupata tuu unashangaa matatizo yanakujia Kwa kasi ili yamalize hizo Pesa ulizozipata.

3. Maisha Marefu

Mkeo au Mama Watoto wako atachangia Kwa kiasi kikubwa umri utakaoishi Duniani. Ni rahisi kuacha Watoto wako yatima ikiwa hautakuwa Makini kuchagua MKE wa kuoa. Sisi wanaume tunahitaji utulivu wa Akili pamoja na heshima. Endapo utaoa Mwanamke anayekupasua kichwa, ambaye bila Shaka atakuzalia Watoto pasua kichwa basi tambua kuwa uwezekano wa Kufa mapema ni mkubwa Mno. Yaani Watoto wako kubakia yatima ni Jambo la hakika. Ni ngumu kufikisha miaka 60 ikiwa haujachagua MKE sahihi.

Elewa kuwa Wanawake wengi wasio na Sifa za kuwa MKE wanaamini kuwa utakufa mapema Kabla Yao.
Elewa kuwa Mwanamke asiyekuombea au anayekuombea Kwa faida zake(ubinafsi wake) huyo ni mchawi.
Mwanamke anayewaza Mali kuliko kukuwaza wewe mumewe huyo ni mchawi. Na ninahakika hauwezi kutoboa miaka 60.

Wazee wangu waliwahi niambia kuwa Mwanamke mchawi na mshirikina Mpe talaka,

4. Uzee wenye Mateso
Hata uwekeze vipi, hata uwe Tajiri vipi, kama hautokuwa Makini katika kuchagua Mama wa watoto wako, nina kuhakikishia uzee wako utakuwa wa mateso. Asije akakudanganya mtu kuwa Pesa ni kila kitu, sio kweli. Pesa hiyohiyo inayorahisisha mambo inaweza kuwa sumu nyakati ukiwa Mzee.

Mkeo anaweza kuchonga njama na watoto au moja ya Watoto wako ili wakuue. Watoto wenyewe wanaweza kukuletea nginjanginja mpaka ukaita Maji MMA. Mali ulizozitafuta Kwa jasho na damu Kwa miaka mingi sio ajabu ukaziona zikitawanywa na kupotezwa kirahisi bila Watoto kujali.

Hii ni Kwa sababu Watoto hawakufunzwa vyema. Zingatia mwalimu Mkuu wa watoto ni Mama, kisha Baba ni mwalimu Msaidizi.

5. Familia Isiyo na Umoja
Hakuna Jambo linaloumiza wababa wenye umri kuanzia miaka 50 kama kuona Watoto wake Hawana umoja.
Siku zote umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Ni kawaida Baba akishafikisha umri wa miaka 40 kusisitiza suala la umoja ndani ya nyumba, tena kama kuna mtoto wa nje basi miaka ya 50 huweza kumtambulisha huyo mtoto na kuwaomba Watoto wengine wamchukulie huyo mtoto kama Ndugu Yao.

Baba anajua kuwa Ikiwa Watoto wake Hawana umoja basi ni wazi familia yake haina nguvu. Na hiyo inamaanisha ameshashindwa. Na familia isiyo na umoja ni rahisi Sana kuwa Maskini na fukara.

Jambo moja la kujua kuwa, hata Baba alazimishe vipi umoja ndani ya nyumba, kama Mama hatoi ushirikiano basi ni hakika nyumba hiyo haitakuwa na umoja yaani nguvu. Historia inaeleza kuwa Wanawake wengi ndio chanzo cha kuvurugika Kwa UMOJA ndani ya familia nyingi Kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu.

Taikon Acha nipumzike

Ijumaaa Kareem na nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ndo hivyo!

Taikoni keshamaliza kutoa mawaidha na wosia wake kwa Watibeli watukutu.

Mwenye masikio na asikie!

Screenshot_20230324_101052_Chrome.jpg
 
Napenda sana kusoma Nondo zako nzito kwani zinaniongezea maarifa mara kwa mara
 
Nimesoma mwanzo mpaka mwisho,
Npo Kwenye ndoa miaka kadhaa Sasa,
Nilishajisamehe kitambo kwa kutokujua thamani ya mke wangu tangu mwanzo,
Now namshukuru Mungu, Maisha yaendelea vema.
 
Nimesoma mwanzo mpaka mwisho,
Npo Kwenye ndoa miaka kadhaa Sasa,
Nilishajisamehe kitambo kwa kutokujua thamani ya mke wangu tangu mwanzo,
Now namshukuru Mungu, Maisha yaendelea vema.

Barikiwa Sana Mkuu.
Mkeo ni sehemu ya mwili wako, sehemu ya Maisha yako.
Hivyo kama vile unavyoupenda na kuuhwshimu mwili wako ndivyo ambavyo unapaswa kufanya vivyohivyo kwake.

Hatari ni pale unapokosea kuchagua
 
Back
Top Bottom