Msaidieni mama huyu

Esperance

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
364
84
Hamjambo wana Jamvi la MMU, nimepotea kidogo afya inasumbua na hii hali yangu. Leo nimepata kisa cha kusikitisha sana. Kuna mama mmoja ameolewa na watoto 2. Sasa wameanza ujenzi na mume wake, katika pitapita mafundi wamemwambia mumewe anaendaga site na binti ana watoto wadogo 2 na wanamwitaga baba. Katika uchunguzi inaonekana mumewe ana nyumba ndgo. Kumuuliza akamjibu lazima wapajue kuna leo na kesho,ndio ni watoto wangu. Mama wa watu keshainvest karibia robo tatu ya nyumba. Na mumewe kila siku analalamika hana pesa mama akipata anatupia mjengoni pamoja na mikopo. Mama keshakuwa frastruted anahama makanisa, keshatishia kujiua mara 2. Msaada wapendwa imeniuma sana.
 
Pole mpendwa ...miezi kadhaa tu utakua unajichekea mwenyewe!!!

Aisee hiyo story ya huyo mama inasikitisha!!Jamani wanaume nyie sijui wanawake wamewakosea nini!!
Huyo mama anahitaji lundo la faraja maana matatizo yote hayo anaweza akajimaliza wakati wowote.
Nashindwa kuendelea ngoja nisome some kwanza.......
 
asante dear we acha hapa nalala na embe tanga, yani huyu mama acha hana tumaini tena,ni Mungu tu atamsaidia.
 
Pole na kuumwa, hapo cha kusaidiwa ni nini? aidha nyeusi au nyeupe, hakuna kijivu hapo. Abaki na mumewe au amuache! kuna jingine?
 
si haende mahakamani aka claim divorce kama ni ndoa ya kikristu, then aende kufile petition mahakamani ya kuomba haki yake katika hiyo nyumba, the court will decide.
 
Aisee hiyo story ya huyo mama inasikitisha!!Jamani wanaume nyie sijui wanawake wamewakosea nini!!

.

And it pains a lot, with lots of attention when a victim is a woman.
But when the reverse is the case its a rightful deed. Too bad that we men we rarely disclose our concerns.
 
Watu waache kulalamika bila kuchukua hatua. Huyu mama hata akisali ndani ya makanisa 100 kwa siku hayawezi kutatua tatizo lake. Kwa hiyo akubali kuchukua maamuzi mazito bila kuangalia makunyanzi. Na awe tayari kwa matokeo yoyote. Kwa hiyo...
1. Akae na mume wake ampe ufafanuzi wa kutosha kuhusu hiyo nyumba yake ndogo (endapo yeye ni mke rasmi wa ndoa) na pia amweleze mipango yake ya muda mfupi na muda mrefu na huyo mzazi mwenzake. Kama atamweleza basi huo utakuwa ni mwanzo mzuri wa kukubaliana kuhusu umiliki wa hiyo nyumba. Kama mwanamume atakataa kuzungumzia haya mambo ya kuendeleza jeuri kama hiyo aliyotumia kumueleza kuwa hao watoto ni wake...achukue hayo ninayoshauri kwenye No.2.
2. Awaone wataalamu wa sheria ili wampatie ushauri wa kisheria. Hapa inawezekana Mume akakubali kuweka mambo kwenye karatasi au akagoma. Na hapo ndipi dada itabidi aamue ama kupoteza nyumba na kubaki na mume au kudai haki yake kwenye hiyo nyumba hata ikibidi kumpoteza mume.

Kwa maoni yangu hakuna short kati...akiendelea kulia lia na kunena kwa lugha ataambulia BP!!

Mzee DC!!
 
And it pains a lot, with lots of attention when a victim is a woman.
But when the reverse is the case its a rightful deed. Too bad that we men we rarely disclose our concerns.
Bana weee....hamna

upendeleo ila hapa namfikiria mama wa watu tu....itakapokuja inayomhusu mwanaume nae atapata haki yake but untill then ntaendelea kujiuliza huyu mama alimkosea nini huyo mwanaume maana alivyomtenda......
 
Lizzy,

Hivyo ni baadhi ya vijimambo vya kwenye ndoa. Kutenda hayo maswahibu, ambayo wewe unasema ni kumetenda huyo dada si lazima akukosee. Tena unaweza kukuta huyo mume anampenda sana mke wake ila kuna kitu huyo nyumba ndogo anacho kinachomzingua.

Mke wa ndoa atafute msaada wa kisheria ili kila kitu kiwekwe wazi..black and white. Ila hata sisi tulioko nje au tunaotazama hiyo movie tujifunze kuishi maisha ya uhalisia..

Nachukia tabia ya kukimbia matatizo ingawa pia nachukia sana kuwatendea wenzangu mambo yanayoumiza mioyo yao beyond repair!

Mzee DC!!
 
Hamjambo wana Jamvi la MMU, nimepotea kidogo afya inasumbua na hii hali yangu. Leo nimepata kisa cha kusikitisha sana. Kuna mama mmoja ameolewa na watoto 2. Sasa wameanza ujenzi na mume wake, katika pitapita mafundi wamemwambia mumewe anaendaga site na binti ana watoto wadogo 2 na wanamwitaga baba. Katika uchunguzi inaonekana mumewe ana nyumba ndgo. Kumuuliza akamjibu lazima wapajue kuna leo na kesho,ndio ni watoto wangu. Mama wa watu keshainvest karibia robo tatu ya nyumba. Na mumewe kila siku analalamika hana pesa mama akipata anatupia mjengoni pamoja na mikopo. Mama keshakuwa frastruted anahama makanisa, keshatishia kujiua mara 2. Msaada wapendwa imeniuma sana.

I feel for the woman i wish i knew her... yuko so frustrated na naamini moyo, akili na mwili woote unamuuma. Akina mama siku zote hata kama ndoa yako ina raha gani haitakiwi kujisahau kabisaa katika ndoa maana ni wazi kua baba zetu hawa hawaridhiki... Huyo mama alifanya haraka sana hatua alizochukua but simlaumu maana mara nyingi mtu waweza kua irrational katika hali hio....

Inabidi kwanza ashinde moyo wake na kutuliza akili yake, kama ameinvest robo tatu katika nyumba na inajulikana kua she is the wife naamini kua nivigumu sana kua hio nyumba ataimiliki tu mwanaume peke yake maana sasa hivi hayo mambo akina mama wanasimamiwa saana akipeleka issue kama hio sehemu husika. Na inasikitisha saizi makanisa yamekua mengi saana mpaka wa kuchakachua waumini wamo humo humo... Na anapotishia kua atajiua ni kazi bure mana itakua furaha kwa mwanaume maana kama kathubutu kumjibu bila aibu ni wazi kua hamjali...

Atahangaika, atachanganyikiwa, ataenda makanisa yoote, atamchukia mumewe, atahaha but ukweli unabaki kua kuweza tatua tatizo lake inabidi atulize akili na apunguze hizo hasira. Huyo mwanamke ina maana tayari ni mke mwenzake, akitaka apate haki yake kwenye hio nyumba akalishe hapo nyumbani - na huyo mwanaume atakua alifanya makusudi kuenda na watoto wa nje ili apate habari na sababu anamfahamu hasira zake, nia yake yaweza kua ili huyo mama aondoke - which akifanya itakua ushindi kwa huyo mwanaume...
 
Atahangaika, atachanganyikiwa, ataenda makanisa yoote, atamchukia mumewe, atahaha but ukweli unabaki kua kuweza tatua tatizo lake inabidi atulize akili na apunguze hizo hasira. Huyo mwanamke ina maana tayari ni mke mwenzake, akitaka apate haki yake kwenye hio nyumba akalishe hapo nyumbani - na huyo mwanaume atakua alifanya makusudi kuenda na watoto wa nje ili apate habari na sababu anamfahamu hasira zake, nia yake yaweza kua ili huyo mama aondoke - which akifanya itakua ushindi kwa huyo mwanaume...[/QUOTE]

Hapana Asha D,

Huyo mwanamume kama anawaza namna hiyo basi anajidanganya. Katika hili hakuna sababu ya kutafuna maneno..Sheria iko wazi. Kama huyo dada ni mke wa ndoa (tena ya mke mmoja au hakuna official report ya mke wa pili) basi anamiliki 50% ya hiyo nyumba. Ni wajibu na haki yake kudai hiyo shea yake na kuhakikisha kwamba kila kitu kinakuwa clarified. Akisubiri kudra za Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu, hatakuwa na mtu wa kulaumu isipokuwa yeye mwenyewe!!
 
DC nakubaliana na wewe but mpaka wafike huko anything can happen.. watu mnapooana siku zinavyozidi kwenda ndo mnazidi kusomana, ndio najua kuwa yawezekana mama anatishia tu kujiua but kwa mtu yeyote anae tamka hivyo possibility ipo... Si wote wanajua haki zao maana kwa jinsi huyo mwana mama alivyoelezewa ni kua anatapatapa mno (ni dalili ya kuonesha hana hope - na kama hana hope ina maana hajui haki yake). Ndo mana nasema inawezekana mume alifanya makusudi kwa kujua mke wake at react vipi....

Ukipitia vizuri post yangu utakuta ulo post hapa nimeliongelea na kuliunga mkono, tatizo hapa nikua huyo mama kachanganikiwa mpaka mwisho na nafikiri hizo frustrations zinakusanya kugundua kuna familia nyingine, kugundua kuna watoto tena wawili, kugundua kua mume anahusisha hio familia from nowhere katika hio nyumba.
Inabidi kwanza ashinde moyo wake na kutuliza akili yake, kama ameinvest robo tatu katika nyumba na inajulikana kua she is the wife naamini kua nivigumu sana kua hio nyumba ataimiliki tu mwanaume peke yake maana sasa hivi hayo mambo akina mama wanasimamiwa saana akipeleka issue kama hio sehemu husika. Na inasikitisha saizi makanisa yamekua mengi saana mpaka wa kuchakachua waumini wamo humo humo... Na anapotishia kua atajiua ni kazi bure mana itakua furaha kwa mwanaume maana kama kathubutu kumjibu bila aibu ni wazi kua hamjali...

Labda kama sijakupata ....
 
Lizzy,

Hivyo ni baadhi ya vijimambo vya kwenye ndoa. Kutenda hayo maswahibu, ambayo wewe unasema ni kumetenda huyo dada si lazima akukosee. Tena unaweza kukuta huyo mume anampenda sana mke wake ila kuna kitu huyo nyumba ndogo anacho kinachomzingua.

Mke wa ndoa atafute msaada wa kisheria ili kila kitu kiwekwe wazi..black and white. Ila hata sisi tulioko nje au tunaotazama hiyo movie tujifunze kuishi maisha ya uhalisia..

Nachukia tabia ya kukimbia matatizo ingawa pia nachukia sana kuwatendea wenzangu mambo yanayoumiza mioyo yao beyond repair!

Mzee DC!!
Mzee DC mapenzi gani hayo yakuletewa watoto wawili kwenye ndoa na kimada kutembelea nyumba anayogharamia mama wa watu???Kwa style hii wengi watakufa kabla ya muda wao...wengine wataingia kwenye ndoa mguu ndani mguu nje wakati wengine tutagoma kabisa!!!
 
Bana weee....hamna

upendeleo ila hapa namfikiria mama wa watu tu....itakapokuja inayomhusu mwanaume nae atapata haki yake but untill then ntaendelea kujiuliza huyu mama alimkosea nini huyo mwanaume maana alivyomtenda......
Jamani wanaume nyie sijui wanawake wamewakosea nini!!
.
.
Niliona uligeneralize ndo mana nikapata mzuka.
Nadhani ilikuwa ni motherly feeling ilikupanda, it can be explained, stori ya mama huyu kama ni kweli inatia huruma
 
Orait....next time ntapunguza munkari kabla sijachangia!!

Yeahhh inasikitisha kweli....hopefully ataweza kukabiliana nayo!!!
 
Mzee DC mapenzi gani hayo yakuletewa watoto wawili kwenye ndoa na kimada kutembelea nyumba anayogharamia mama wa watu???Kwa style hii wengi watakufa kabla ya muda wao...wengine wataingia kwenye ndoa mguu ndani mguu nje wakati wengine tutagoma kabisa!!!

wanaume wa hivi wanawafanya baadh ya wanawake wafanye mambo kimya kimya bila kuwashirikisha aaah, pole mama, naunga mkono hoja ya Mzee DC, Sa ingine maamuzi magumu yanahusu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom