Msaada Rice cooker ipi nzuri yenye uwezo wa kupika mchele kilo moja na nusu?

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Dec 7, 2018
733
1,677
Wadau kwema? Aisee hii wiki ya pili sasa kila nikijaribu kupika wali nachemka. Mara siku nyingine napatia mara siku nyingine kinatoka kiini.

Leo kimetoka kiini nimekumbuka nilipokuwa chuo pale udsm niliwahi kuwa natumia rice cooker kwenye umeme wa bure wa mabibo hostel.

Nahitaji rice cooker yenye uwezo wa kupika wali kilo moja na nusu.

Brand ipi ni nzuri na bei yake?

Vipi kuhusu bajeti ya umeme. Rice cooker inakula sana umeme ? Nijiandae kwa bajeti ya umeme kiasi gani kwa mwezi maana almost kwa wiki nitakuwa napika wali kwa rice cooker.

Kingine vipi rice cooker inatoa wali ambao unakuwa umekwiva vizuri ? Au na yenyewe kuilia timing kama unapikia kwenye gesi au mkaa? With much thanks in advance
 
Weka maji kwenye cooker yenye mchele!

Kiasi cha maji pima kupitia kidole chako cha kati ambapo maji yafikie katikati ya mistari miwili ya kidole chako cha kati!

Likijifyatua tulia for a while then bofya tena kitufe.

Likijifyatua tena na kubaki rangi ya machungwa liache kwa dk 10 hivi hapo Kibeche kitakuwa kipo poa.

MIMI NATUMIA LA E-HOUSE MWAKA WA TISA SASA.
 
Mimi natumia West Point niliinunua 2020 kwa 120,000/= Game iliyokuwa Mlimani City mpaka leo iko poa inapiga kazi.

Yani kwa jinsi nilivyoizoea ni bora nikose vifaa vyote vya umeme jikoni sio rice cooker. Ni mara chache kupika wali nje ya rice cooker na ni ikiwa ni wali nazi pekee.
 
Mkuu mambo yasiwe mengi,

Kama una uchumi mkubwa nunua hayo wanayoshauri,

Ila mm langu nililinunua Ailyons 2020, kwa 50k tu pale tukaanza kutumia UDOM mwaka mzima, humo tumepikia kila kitu unachojua, nyama, njegere, dagaa, hapo unachemsha na kuunga 😂😂😂 + kuchemsha maji, after that nikaenda nalo geto kila siku napikia wali au maharage au kuchemshia nyama,

Sema mtaani huku siungii nyama,

Kuhusu umeme lina 700W, wali kg 1 na robo inatumia nusu saa so kama 0.35 unit,
 
Mimi natumia West Point niliinunua 2020 kwa 120,000/= Game iliyokuwa Mlimani City mpaka leo iko poa inapiga kazi.

Yani kwa jinsi nilivyoizoea ni bora nikose vifaa vyote vya umeme jikoni sio rice cooker. Ni mara chache kupika wali nje ya rice cooker na ni ikiwa ni wali nazi pekee.
Asante sana dada ake. Vipi kuhusu umeme? Elfu kumi kwa mwezi itatosha?
 
Kabisa. Umeme sio wa kuhofia kwenye rice cooker, ni kidogo mno!

Ungemuambia ina Watts ngapi tungempa hesabu ya matumizi ya umeme
Kimsingi hivi vitu vya umeme/Petrol nk vinahitaji data; kwani watu wanatofautiana mtazamo na uwezo; Mfano; kwa mtu mwingine unit 15 za umeme ni nyingi sana , mwingine ni za kawaida na mwingine ni kidogo sana
Ushauri wangu anunue Multicooker (ile ambayo unachagua unachopika, Nyama, mahage nk) pia iwe na watts kati ya 700 na 1200 tu; hizo kiasi zinatumia umeme wa watu wa kawaida
 
Nahitaji rice cooker yenye uwezo wa kupika wali kilo moja na nusu.
  • Usinunue Rice cooker.
  • Bali nunua Pressure cooker
Kwanini ununue pressure cooker?
  • Utaweza kupika wali kama kawaida
  • Utaweza kupigia Nyama
  • Utaweza kupikia Maharage
  • Kwa ujumla chochote kile waweza kupikia.
Utapika Kwa muda kidogo zadi hivyo kubana matumizi ya umeme.

Bei : Haizidi 120,000
Brand: Ailyons ( na ndugu zake), Wapi: Karikoo ziko kwa wingi
 
Good mimi kutokana na experience yangu ya kutumia hizo brand mbili ulizoziponda, nimepata hivyo vyote je ni vibaya kuzisifia, au nilitakiwa nisemee kutokana na experiences za watu wengine mkuu
Kwa aboder hapo utapata performance, applicability na technology lakin huwezi kupata durability ,quality,na efficiency.
 
Back
Top Bottom