Mrejesho kuhusu kesi yangu na app za mikopo

Mimi si mkopaji, kuna mtu alikopa lkn hawa watu wa hizi App wanaingia kwenye phone book ya mkopaji kwa kutumia hiyo APP, wanachukuwa taarifa za mkopaji, kwa maana ya contacts list, sms, photos nk. Hivo wakishachukuwa hizo details na ikiwa mkopaji amechelewa kulipa hizo hela wanatuma sms kwa namba zote zilizoko kwenye Simu ya mkopaji.
Kifupi mimi ni Mhanga kutokana na kwamba ni miongoni mwa wale wenye namba ambazo ziko kwenye phone book ya mkopaji. Sijakopa, sijawahi kuulizwa ikiwa namfaham mkopaji, na kama niko tayari kumdhamini. Natumaini nimekujibu.
Nadhani hapo mkopaji anatakiwa asi allow hiyo app husika kuwa na access ya contacts list na device husika hivyo unapo pakua nenda kwenye settings an disallow hapo hautaweza kupata contacts zako
 
Back
Top Bottom