Mrejesho kuhusu kesi yangu na app za mikopo

Hypersonic

JF-Expert Member
Apr 14, 2012
612
1,131
Kama nilivoahidi kuwa leo Jumatatu tarehe 26/02/2024 naanza mchakato wa kuwashitaki hawa watu.

Nimeanzia TCRA ambako nimepeleka malalamiko yangu, Majibu ya TCRA ni kwamba wao hawahusiki kwa sababu hasimamii watu bali wabasimamia makampuni ya mawasiliano. Hii kidogo imeshitua hivo ikabidi niende polisi, Majibu ya polisi ni kwamba nikamshauri mkopaji alipe kwanza alafu yeye ndo afungue mashitaka.

Nimeamua kubadilisha kesi na nimefungua kesi ya kutukwana na kudhalilishwa kwa njia mtandao kwa wale niliofanikiwa kuwarekodi.

Ahadi ya polisi ni kwamba wanatrack namba wakishawapata wahusika watawakamata na baada ya hapo ndo tutaendelea mbele.

Ugumu wa kesi ni kuthibitisha pasipo shaka kuwa kweli ile sauti ni ya mhusika pindi akiwa mahakamani.

Ni nini cha kufanya:- Bado sijakamata tamaa narudisha mpira kwa kipa kwa maana ya kushirikiana na wanasheria ili nishitaki ama TCRA au Kampuni ya mtandao husika kwa kushindwa kulinda faragha yangu nikiwa kama mteja ambaye wanawajibu wa kulinda taarifa zangu.

Safi Sana watu conscience kama wewe wakiongezeka hakika hata ccm itaanga mpambano.
 
Wewe ndio mkopaji na wewe ndio mlalamikaji au ni mimi sijaKulewa? Dawa ya deni ni....
au unataka kutafuta technicality ya kufutiwa deni?
Hajakataa kulipa. Tunaongozwa na sheria na hakuna sheria inayosema kuwa usipolipa utukanwe na uzalilishwe.

Mtoa mada, usikate tamaa, na kwa kushauri inawezekana mmiliki ni mtu fulani mzito usideal na kampuni, deal na aliyetoa matusi ukihitaji kampuni itoe ushirikiano kwa kumtaja.
 
Kama nilivoahidi kuwa leo Jumatatu tarehe 26/02/2024 naanza mchakato wa kuwashitaki hawa watu.
Nimeanzia TCRA ambako nimepeleka malalamiko yangu, Majibu ya TCRA ni kwamba wao hawahusiki kwa sababu hasimamii watu bali wabasimamia makampuni ya mawasiliano. Hii kidogo imeshitua hivo ikabidi niende polisi, Majibu ya polisi ni kwamba nikamshauri mkopaji alipe kwanza alafu yeye ndo afungue mashitaka.

Nimeamua kubadilisha kesi na nimefungua kesi ya kutukwana na kudhalilishwa kwa njia mtandao kwa wale niliofanikiwa kuwarekodi.

Ahadi ya polisi ni kwamba wanatrack namba wakishawapata wahusika watawakamata na baada ya hapo ndo tutaendelea mbele.

Ugumu wa kesi ni kuthibitisha pasipo shaka kuwa kweli ile sauti ni ya mhusika pindi akiwa mahakamani.

Ni nini cha kufanya:- Bado sijakamata tamaa narudisha mpira kwa kipa kwa maana ya kushirikiana na wanasheria ili nishitaki ama TCRA au Kampuni ya mtandao husika kwa kushindwa kulinda faragha yangu nikiwa kama mteja ambaye wanawajibu wa kulinda taarifa zangu.
Nadhani ungeenda na BOT
 
Hii kesi hushindi, na unajipeleka mwenyewe kwenye mdomo wa mamba; utalipia gharama zote za usumbufu, kama watatumia wakili mbobezi.

Ungekuwa umelipa deni kwa wakati ndio ikatokea hiyo songombingo; kesi yako ingekuwa na mashiko.

Kwa kukushauri tu; lipa deni, songa mbele.​
 
Weka hapa RB ya Polisi tuone kama kweli umekwenda. Je, TCRA tutaamini Vipi umeenda? Malalamiko umetuma kwa njia gani? Je, wamekujibu kwa Maandishi?
 
Sheria na sera za mikopo haziruhusu mtu aliyeshindwa kulipa deni kudhalilishwa na kutukanwa.

Na hapo ndio hizo kampuni uchwara hukosea

Leseni huna
Hujasajiliwa
Bado unatukana wateja
 
Unafikiri kwa nini huko alikoanzia wana mpiga dana dana?
 
Wewe ndio mkopaji na wewe ndio mlalamikaji au ni mimi sijaKulewa? Dawa ya deni ni....
au unataka kutafuta technicality ya kufutiwa deni?
Mimi si mkopaji, kuna mtu alikopa lkn hawa watu wa hizi App wanaingia kwenye phone book ya mkopaji kwa kutumia hiyo APP, wanachukuwa taarifa za mkopaji, kwa maana ya contacts list, sms, photos nk. Hivo wakishachukuwa hizo details na ikiwa mkopaji amechelewa kulipa hizo hela wanatuma sms kwa namba zote zilizoko kwenye Simu ya mkopaji.
Kifupi mimi ni Mhanga kutokana na kwamba ni miongoni mwa wale wenye namba ambazo ziko kwenye phone book ya mkopaji. Sijakopa, sijawahi kuulizwa ikiwa namfaham mkopaji, na kama niko tayari kumdhamini. Natumaini nimekujibu.
 
Hii kesi hushindi, na unajipeleka mwenyewe kwenye mdomo wa mamba; utalipia gharama zote za usumbufu, kama watatumia wakili mbobezi.

Ungekuwa umelipa deni kwa wakati ndio ikatokea hiyo songombingo; kesi yako ingekuwa na mashiko.

Kwa kukushauri tu; lipa deni, songa mbele.​
Nitalipaje ili hali sijawahi kopa nadhani hujaelewa soma tena. Na wala sitotishwa na maneno yako. Sizui mtu kukopa wala kufanya biashara ya Loan Sharks, mimi ninapingana na utaratibu wao wao wa kuharass wale tusiokuwa wakopaji. Mimi siwezi kwenda kukopa laki kadhaa kwenye taasisi nitaenda kwenye taasisi kukopa milioni kadhaa, laki kadhaa namalizana na wana kitaa.
 
Weka hapa RB ya Polisi tuone kama kweli umekwenda. Je, TCRA tutaamini Vipi umeenda? Malalamiko umetuma kwa njia gani? Je, wamekujibu kwa Maandishi?
RB nikuwekee wewe kama na nani inatosha kuamini hivo, TCRA nimeenda nimejibiwa kwa mdomo niweke pia mdomo hapa ili uamini nimeende, bado sitotolewa kwenye reli najua wengine ndo wale mnaolipwa na wachina vilaki mbili mbili kutukana watu huku mkisukuma siku. Hata kama sitoshinda naamini kuna kitu kitabadilika hatuwezi kuacha wahuni na wapuuzi wachache waendelee kufanya wanavyotaka, Mahakamani lakini lazima nifike pamoja na kuwashitaki wale walionitolea lugha za matusi wakati na hoji bado nitashitaki App zilizojitambulisha wakati natumiwa sms. Hili ni suala la kushirikiana na wanasheria zaidi.
 
Nadhani ungeenda na BOT
Kwenda BOT ni endapo ningekuwa nahoji uhalali wa leseni zao, ila mimi sitaki kujua chochote kuhusu biashara zao. Mimi nataka kama wanahitaji kukopesha watu, wafuate taratibu wahakikishe wanayemkopesha anakopesheka na anaouwezo wa kulipa. Wadhamini wasainishe mikataba ya makubaliano kama kweli wanahitaji wadhamini.
 
Back
Top Bottom