Kwanini Mawakili wengi binafsi wanashangilia na kukimbilia kusimamia kesi za wanaodaiwa kutukana au kuikosoa Serikali?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Leo tumeona Polisi wamedai kumkamata mmiliki wa akaunti ya X inayotambulika kwa JINA la Sukunuku; mara tu polisi walipotaka hayo mawakili binafsi wengi wameonyesha nia ya kusimamia kesi hiyo huku baadhi wakiweka wazi kwamba watashinda kesi husika mapema kabisa.

Mmoja wa mawakili ndugu Madeleka ameeleza ugumu wa kesi ya mtandao kwamba ili uthibitishe upotoshaji lazima uonyeshe ukweli jambo ambalo kwenye kesi ambazo uandaliwa kwa hisia za mpelelezi nivigumu kupata ushahidi wa kuishawishi mahakama.

Upande mwingine wanaharakati wanaeleza kwamba pamoja na sheria ya cyber kuwepo ni vigumu kuthibitisha makosa yaliyoainishwa katika sheria hiyo na hivyo kushindwa kesi kwa Jamuhuri ni jambo la kawaida.

Wapo wengine wanaodai kwamba sheria hii ni ngumu kutekelezeka hasa ikizingatiwa kwamba mwana CCM akitoa lugha fulani hazitafsiriwi na jeshi la polisi kama matusi. Mfano anatajwa Nape Nauye kwamba mara kadhaa ametukana mtandaoni lakini hakuna aliyewahi kumkamata. Viongozi waandamizi wa serikali pia utukana lakini hakuna aliyewahi kukamatwa jambo linaloleta tafsiri kwamba sheria hizi zimeundwa kwaajili ya wapinzani na siyo watu wote.

kulingana na mitizamo hii naamini imewafanya mawakili wengi kuona wanaokamatwa wanaonewa na hivyo kujitolea kuwasimamia lakini pia jeshi la Polisi limekuwa halichukulii serious kesi hizi hasa wakitambua kwamba hawatendi haki kwa watu wote bali wanakandamiza kundi flani

Kwa upande wangu naamini hali hii imepelekea wavunjaji wa sheria kuwa na watetezi wengi hasa sheria zinazolinda maslahi ya wanasiasa watawala. Hakuna mwananchi anayechukizwa na watoe matusi kwa sababu wameona watoa matusi nao wana hoja isipokuwa katika kuwasilisha malalamiko yao wanaweka na maeneo ya udhalilishaji na yanayotweza utu.

Way foward: Tukamate kwanza watawala na kuwafungia ili walio nje ya utawala wajifunze. Nazungumza haya nikikumbuka alivyofanyiwa NONDO wa ACT......akahesabika kama gaidi leo anakula meza moja na watawala
 
Anko nikueleze tu. Twitter inaongoza kwa watu wanaoichukia serikali. Watu wanaopata habari nusu nusu. Wao kila kitu wanakishadadia. Good enough wanaenda na upepo. Anakamatwa kijana, deus wakili kamuombea dhamana katoka. Wao wanatembea na. Upepo kesi hakuna walimkamata tu, ona sasa wamemuachia wanasahau ni dhamana ndio imemtoa.

Something else nikazie, Polisi Tanzania huwa hawafatilii mwenendo wa kesi zao. Zinaenda kirafiki sana. Ndio maana wenye makosa wakiwa na connection huachiwa na wanaopotea ni watu hoe hae.

Ambao hawafatiliwi.

Sijui ntakua nimejibu vzuri. Ila nahisi kuna part siijaizungumza kama sitoeleweka
 
Leo tumeona Polisi wamedai kumkamata mmiliki wa akaunti ya X inayotambulika kwa JINA la Sukunuku; mara tu polisi walipotaka hayo mawakili binafsi wengi wameonyesha nia ya kusimamia kesi hiyo huku baadhi wakiweka wazi kwamba watashinda kesi husika mapema kabisa...
Talking about Sukununu yule jamaa yuko vizuri sana kwenye critics na sio kwa Gvt tu bali hata kwa tweeps wengine.

Mbaya zaidi anafanyia bullying watu wa X(formerly Twitter) kiasi wanamchoka hasa sana wanawake, wanaume(few of them especially those seeing themselves as superior than others) na watu wa Gvt.

The issue of Sukununu ilichukua sura mpya baada ya kuibuka pande mbili
1. Upande wa sukununu (utetezi)
2. Upande usio wa sukununu (washtaki)

Hata baada ya kuzagaa taarifa kua Sukununu amekamatwa ilizua gumzo why & how mbona wako wengi tu ambao wanatukana tena sana ila hawajawahi kamatwa so why him?

Nape aliwahi sema (yashakum si matusi) m*e**e ila hakuwahi kuchukuliwa hatua hata pia bungeni kuna mbunge aliwahi kusema live sasa kwanini Sukununu tu.

Nadhani hiyo ndo imeleta picha tofauti kwa Advocates kukivalia njuga ili kuepusha uonevu kwa raia wa kawaida.

NO ONE IS ABOVE THE LAW
 
Leo tumeona Polisi wamedai kumkamata mmiliki wa akaunti ya X inayotambulika kwa JINA la Sukunuku; mara tu polisi walipotaka hayo mawakili binafsi wengi wameonyesha nia ya kusimamia kesi hiyo huku baadhi wakiweka wazi kwamba watashinda kesi husika mapema kabisa...
Sasa Mtu kaandika "Samia zaidi ya kuwa Rais, wewe pia ni mke wa mtu". Hapo kapotosha nini?
 
Tanzania mtu akiwa anatukana na kudhalilisha watu,anaonekana shujaa kwa baadhi ya wajinga wanaenda mbali zaidi na kusema ni Uhuru, tunatengeneza kizazi cha ovyo sana kwa kisingizio cha Uhuru. Yaani utukane matusi usingizie uhuru?
 
Talking about Sukununu yule jamaa yuko vizuri sana kwenye critics na sio kwa Gvt tu bali hata kwa tweeps wengine.

Mbaya zaidi anafanyia bullying watu wa X(formerly Twitter) kiasi wanamchoka hasa sana wanawake, wanaume(few of them especially those seeing themselves as superior than others) na watu wa Gvt....
Dogo anazingua yule, mi nilimtia block kitambo sana pamoja na chawa wapush hashtag wale. Ana lugha chafu sana
 
Tanzania mtu akiwa anatukana na kudhalilisha watu,anaonekana shujaa kwa baadhi ya wajinga wanaenda mbali zaidi na kusema ni Uhuru,.......tunatengeneza kizazi cha ovyo sana kwa kisingizio cha Uhuru.....yaani utukane matusi usingizie uhuru?
Shida nchi yenyewe inaendeshwa kitapeli, ni kweli ana makosa ila sio makubwa kiasi hicho, na nchi yenyewe ipo kiholela, mfano mdogo waziri wa michezo anasema atakaye enda kuwapokea wapinzani (al ahly na mamelodi) watashughulikiwa kwa kosa lipi? Na kanuni ipi?
 
Anko nikueleze tu. Twitter inaongoza kwa watu wanaoichukia serikali. Watu wanaopata habari nusu nusu. Wao kila kitu wanakishadadia. Good enough wanaenda na upepo...
Kwanini tweeter iwe na watu wanaopinga Serikali? Hawa watu hawana akaunti kwenye mitandao mingine?

Wewe unaamini kwamba watu wanakamatwa kwa kupinga serikali au kwa kukiuka sheria?
 
Tanzania mtu akiwa anatukana na kudhalilisha watu,anaonekana shujaa kwa baadhi ya wajinga wanaenda mbali zaidi na kusema ni Uhuru,.......tunatengeneza kizazi cha ovyo sana kwa kisingizio cha Uhuru.....yaani utukane matusi usingizie uhuru?
Je nani anasema ili ni tusi na siyo tusi? Kwanini kesi nyingi za aina hii tunashindwa kuthibitisha mahakamani?

Nini serikali iboreshwe kuepuka kumkamata kiumbe ambaye jamii inaona ametukana lakini kwenye uso wa sheria siyo tusi?
 
Kwanini tweeter iwe na watu wanaopinga Serikali? Hawa watu hawana akaunti kwenye mitandao mingine?

Wewe unaamini kwamba watu wanakamatwa kwa kupinga serikali au kwa kukiuka sheria?
Kuna kundi la vijana wachache wanaosapotia a(wapwa)
Mengine hayo uliyoandika yako nje ya mada yangu, hizo hisia achana nazo ndugu.
 
Shida nchi yenyewe inaendeshwa kitapeli, ni kweli ana makosa ila sio makubwa kiasi hicho, na nchi yenyewe ipo kiholela, mfano mdogo waziri wa michezo anasema atakaye enda kuwapokea wapinzani (al ahly na mamelodi) watashughulikiwa kwa kosa lipi? Na kanuni ipi?
Nikweli mambo mengi hayako sawa,ila haihalalishi kutukana watu,Ndumbaro anataka kutrend tu..... ndiyo viongozi wa kizazi hiki
 
Je nani anasema ili ni tusi na siyo tusi? Kwanini kesi nyingi za aina hii tunashindwa kuthibitisha mahakamani?

Nini serikali iboreshwe kuepuka kumkamata kiumbe ambaye jamii inaona ametukana lakini kwenye uso wa sheria siyo tusi?
Ila mzee ungeelewa mfumo wa ukamataji na ufunguaji au uendeshaji kesi hapa ungepata jibu la swali lako.
 
Je nani anasema ili ni tusi na siyo tusi? Kwanini kesi nyingi za aina hii tunashindwa kuthibitisha mahakamani?

Nini serikali iboreshwe kuepuka kumkamata kiumbe ambaye jamii inaona ametukana lakini kwenye uso wa sheria siyo tusi?
Malezi yanaanza ndani ya familia,huyu dogo upuuzi alikuwa anaandika amekosa adabu
Screenshot_20240314-233100.png
 
Leo tumeona Polisi wamedai kumkamata mmiliki wa akaunti ya X inayotambulika kwa JINA la Sukunuku; mara tu polisi walipotaka hayo mawakili binafsi wengi wameonyesha nia ya kusimamia kesi hiyo huku baadhi wakiweka wazi kwamba watashinda kesi husika mapema kabisa...
BIG FACT
 
Nikweli mambo mengi hayako sawa,ila haihalalishi kutukana watu,Ndumbaro anataka kutrend tu..... ndiyo viongozi wa kizazi hiki
kwenye kutukana watu binafsi nilimtia block mapema sana alianza kukashifu tweeps, hii alivopotea ndo ikatrend nikafahamu anatukana mpaka viongozi acha dawa ikolee kwanza
 
Back
Top Bottom