Mr Magufuli atua Kivukoni, kuzuia nauli mpya?

Status
Not open for further replies.
sina tatizo na nauli ya abiria ila nauli za bajaji, magari , guta, na baiskeli mmmmmmh zimezidi!!

lakini kilichozidi zaidi ni kauli ya "watu wapige mbizi" hivi unaweza kweli kuwaambia wananchi maneno hayo au waandishi wa habari wamem-quote vibaya?

haina tofauti na yule aliyesema hata mkila majani ndege itanunuliwa...........

hawa ndo viongozi wetu, na watapata kura za kishindo..... Kweli Bongo ni zaidi ya uijuavyo.................

anyway naenda kununua life jacket mie kuogelea si mchezo, kwikwikwi
 
Kwanini waziri asizomewa kama alichoongea ni zaidi ya uhuni na kutojali kwa kuwa tu anaishi kwenye nyumba ya vioo. Hebu tizama hili!

Ongezeko za uendashaji wa vivuko nani anazisababisha? upande wa ulinzi, pana askari jeshi (navy) na polisi huku upande wa kigamboni wako jeshi wawili na polisi wawili hawa kila mmoja kwa siku anakula 15,000/= nje ya mshahara wake. Askari hugombania kupewa lindo hapa (binafsi sielewi wanalinda nini- hasa Navy.

Wapo Suma JKT kama walinzi wa vivuko,.

Gharama za vivuko (vinasimamiwa na temesa) hupata ruzuku ya serikali nadhani ni kupitia mfuko wa barabara. Kwa hiyo ninapopita daraja la sarrender napaswa nitozwe pesa? Ujinga mwingine, sio tu wa waziri na watendaji wake bali wa wananchi wote wasiojua kuwa serikali inapaswa kutoa huduma ambazo hatuzilipii moja kwa moja bali kupitia manunuzi tunayofanya kila siku.

Mapato ya kvuko hayajabadilika kulingana na hali halisi ya kupanuka kwa kigamboni(ongezeko la 4mil linahitaji mjadala pia),

Pantoni la mv magogoni linaweza kuwa linaongoza kwa kuibwa mafuta, hili limejengwa mahsusi kuendeshwa na mashine nne, muda mwingi linaendeshwa na injini mbili tu, na kwa sasa limekuwa ni kinyonga badala ya samaki. kama una haraka ya kuvuka bora kupanda mv Alina kuliko hili na hii ni kwa kuwa magogoni linapigwa nyoka sana (kuibiwa mafuta)

Kama ni kufidia gharama hizi basi wafuatao watozwe ada za kuvuka, moja, wanajeshi, hawa ni wengi huku kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine wa serikali wa kada tofauti. Inachekesha kumuona ofisa wa jeshi,mwenye kipato cha zaidi ya 1.4mil kwa mwezi anapita bure 'mimi afisa' pumbavu sana,
Polisi wote (hawa hata wawe hawakuvaa sare) wanapita bure, ujinga mtupu

Kwa kulinganisha: Tunajua na sasa tunajua sana, kivuko ni kama daraja, kwa kuwa tumekosa madaraja yanayofunguka basi kivuko ni daraja linalotembea, kwanini nitozwe pesa kupita darajani. Mbona kwenye daraja la mkapa ninapita bila malipo, kbala hakujajengwa daraja tulikuwa tukilipa kivuko cha ndundu.

Jirani zetu kenya, upande wa mombasa, abiria wanapita bila kulipa na ni magari na vyombo vya moto vinapilipa. Iliwahi kutokea kenya walitaka kutozwa shilingi moja (shilingi kumi 15 ya tanzania), wananchi waligoma na serikali ikaendelea kutimza wajibu wake wa kutoa huduma.

Waziri Magufuri, unaweza kuwa na misimamo na wengi tunadhani unafaa kuwa kiongozi, kauli yako hii ni kutaka kutuonesha tumbo lako kwa kuwa tu umeshiba nasi tunavuka kwenda kutafuta chakula. Kumbuka wewe kuvuka hulipi.

Wakzi wa kigamboni wanaweza kukaa kimya 'hasa baada ya kuona makomanboo wakivunja matofari kwa mawe' lakini haimaanishi hatuwezi kusema na kusimulia vijana wetu ambao kwa hakika hawatakuwa na akili kama zetu za kukaa kimya bila kuhoji kwa kusimama mbele

Heri ya mwaka Mpya mhe. Magufuri na ninafikiri huu mwaka 2012 utakuwa MPUMBAVU sana kwako

Kwa sasa, niko hapa kivukoni ninasubiri magogoni ije nielekee k'koo
 
...Haya siyo mambo ya kutupotezea muda kuendelea kulumbana nayo humu ndani. Yapo mambo ambayo nadhani ni ya Msingi kuyajadili lakini siyo hili.
Suala la waziri kuzomewa na wananchi sio dogo ndugu yangu. Na waziri kuwaambia wananchi kama hawamudu kulipa sh 200 wapige mbizi nalo sio dogo!

- Waziri alienda kufanya nini kivukoni? Kutangaza nauli mpya kwenye gazeti la serikali si ingelitosha tu ....maana ni 'suala dogo'!?
- Kwa maoni yako ni kwa nini unadhani waziri amezomewa wakati hakuwa na wajibu wa kuwashirikisha wananchi?
- Kwa nini wananchi wa kigamboni wananung'unika?
- Umesema mbunge wao ana hoja kuhusu bajaji, baiskeli....hoja gani hiyo?
 
Hapa magufuli hapa umechemsha kwelikweli,Unapandisha nauli bila kuangalia maisha ya watu,kwani hicho kivuko kimeingiza ngapi na wewe umefaidika na nini ndo maana umeona biashara inalipa so unaichangamukia.
Mwisho wa umarufu wako ,ukiona watu wanakuzomea ujuwe ndo kushineya mzee,anyway ulishasema unaacha siasa ili upumuzike,nakumbuka Igunga ulivyonyea kambi ,as if kama ujaenda shule kutoa ahadi amabayo watanzania wote waliguna mtindo uliotumia ,wewe ulifikiri unawamaliza wapinzani eti utapata sifa kuchukua jimbo kwa sifa hiyo wakati amsikini wameguna.
mimi nasema watu hasa wahali ya chini wakiguna tu ujuwe umechemsha.Jifunze hilo litakusaidia,sana.
Usilewe na sifa mpaka ukawa unafanya mambo ya ajabu.......Mgema akisifiwa............................
 
Utakubali kiaina utakubali kiaina¿Baba usilie kama vp tuanzishe chuo cha wapiga mbizi cha kujitolea.hakuna kuwa lipisha ada wanachuo wetu.tuwafundishe kuogelea bure kwani mia ya panton mtu hana ataweza kulipa ada ya chuo chetu cha wapiga mbizi?Ila anaakili anafaa kuwa rais.wakazi wa kigamboni wote watakua mabaharia.si wanawake si wanaume.utakubali kiaina,Utakubali kiaina.
 
Huyo magufuli,ndo wadau weng walikua wakimpigia chapuo,sasa ona suala dogo tu la nauli anajibu kwa kebeh,je masuala ya kitaifa?mungu anatuonesha mapemaaaaa
 
Mimi nashangaa na hii serikali sababu wanaoishi upande wa Kigamboni ni haki yao kuja mjini kupitia hivi vivuko na iwe bure kabisa. Hivyo daraja likijengwa wataambiwa walipie daraja? Mtu anasafiri Dar hadi Sumbawanga haulizwi kodi ya kujengewa barabara lakini hapahapa Dar intampasa alipe kodi ya kuvukishwa pantoni. Huu ni uonevu wa hali ya juu. Magufuli ni bepari na mnyanyasaji tu. Inabidi serikali ya Kikwete ichukuwe hatua kwani kosa ni lao miaka yote kwanini wasijenge daraja.
 
Utakubali kiaina utakubali kiaina¿Baba usilie kama vp tuanzishe chuo cha wapiga mbizi cha kujitolea.hakuna kuwa lipisha ada wanachuo wetu.tuwafundishe kuogelea bure kwani mia ya panton mtu hana ataweza kulipa ada ya chuo chetu cha wapiga mbizi?Ila anaakili anafaa kuwa rais.wakazi wa kigamboni wote watakua mabaharia.si wanawake si wanaume.utakubali kiaina,Utakubali kiaina.

hata kupata kiwanja itakua ni urasim
 
huyo ana sifa za kijinga

kama haka ka utaratibu ka ban kageenda likizo japo saa mbili na kasikumuke yaliyofanywa nyuma, magufuri ningejipoza kauli yako na bonge la tusi mmaanaina, waziri gani anavyaa kofia kama anatoka kutoa mbwaa wa kizungu nje
 
Suala la waziri kuzomewa na wananchi sio dogo ndugu yangu. Na waziri kuwaambia wananchi kama hawamudu kulipa sh 200 wapige mbizi nalo sio dogo!

- Waziri alienda kufanya nini kivukoni? Kutangaza nauli mpya kwenye gazeti la serikali si ingelitosha tu ....maana ni 'suala dogo'!?
- Kwa maoni yako ni kwa nini unadhani waziri amezomewa wakati hakuwa na wajibu wa kuwashirikisha wananchi?
- Kwa nini wananchi wa kigamboni wananung'unika?
- Umesema mbunge wao ana hoja kuhusu bajaji, baiskeli....hoja gani hiyo?

tuendako,kuingia kigamboni itakuwa ni lazima uwe na viza
 
Inawezekana wengi tukachangia NEGATIVELY dhidi ya Dr. Magufuli kwa jazba bila kuangalia ukweli wa mambo na kuhitimisha kuwa Dr. Magufuli hafai. Mie ninadhani Magufuli yuko sahihi. Inawezekana approach aliyotumia ndiyo mbaya lakini ukweli unabakia pale pale kuwa nauli ya kivuko Kigamboni inabidi ipande kulingana na hali halisi ya uchumi. Nauli hiyo ya Ths.100 imekuwa ikilipwa kwa muda wa miaka 14 sasa.Mtu anaweza kujenga hoja kuwa suala siyo sh. 100 kulipwa kwa muda mrefu suala ni je, inaleta tija kwa ajili ya kuendesha meli hiyo?

Bado hoja zote zitakubaliana tu kuwa sh.100 haiwezi kuendesha meli na kuwalipa wafanyakazi kwa maana kuanzia miaka hiyo 14 iliyopita kila kitukinachotumika kuendeshaKivuko hicho kimepanda kuanzia - mishahara ya watumishi, diseli, vipuri, gharama za ulinzi na matengenezo. Sasa, kama vyote hivyo vikipanda na tukiwa na kiwango kile kile cha mapato tutaweza kuendesha Kivuko?

Maoni yangu ni kuwa Magufuli yuko sahihi kupandisha gharama na kuwa Tanzania tunahitaji Viongozi wa aina hiyo wenye msimamo na wa kusimamia kauli zao. Siyo viongozi ambao leo anasema hivi kesho anageuka kuwa hakusema hivyo na kuwa alieleweka vibaya katika vyombo vya habari. Huo ndiyo msimamo wa serikali na ndivyotunavyotaka watendaji wa serikali kuwa hivyo.

Hatuhitaji kauli za kigeugeu kama za CCM za KUJIVUA GAMBA ambazo baadaye wakageuka na kusema kuwa hawakumaanisha walichotuambia wananchi awali katika mikutano na vyombo vya habari.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!!!!!. Mbunge wa Kigamboni anaweza kuwa na hoja katika gharama za kuvushia maghari na Bajaji na baiskeli lakini siyo gharama za kuvusha Watu.

Naombeni tumwelewe Dr. Magufuli na tumpe ushirikiano.

nakubaliana na wewe....kwa kiasi.

kuna watu wawili wanasimulia tukio la aina moja kama ifuatavyo:

mtu wa kwanza: juma alifumaniwa akimfira mkewe
mtu wa pili: juma alifumaniwa akimwingilia mkewe kinyume cha maumbile

ni rahisi kumtambua yupi mwenye hekima kati ya hawa wawili.

kuhusu hili la magufuli, acha nikuachie wewe umfananishe na nani kati ya hawa wawili!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom