Mr Magufuli atua Kivukoni, kuzuia nauli mpya?

Status
Not open for further replies.
Majid, hakuna kuomba radhi!!! Hawa watu walimzomea. Kama hukumzomea basi wewe hauhusiki na kauli hiyo. Walikosa ustaarabu, kuzomea ni udhalilishaji mkubwa, hakuna anayeweza kuuvumilia. Najua utasema kuwa yeye ni kiongozi, lakini equally, nasema pia na waongozwaji wana wajibu kuwa na heshima na adabu.
Kwahiyo wewe unaona hiyo kauli ni sawa kuwajibu watu? Nothing can and will justify such statement like the way you want us to believe....
 
Miafrika ndivyo tulivyo.. watu wakiamua kufanya kazi mnawazomea.. kosa la maghufuli nini hapo? Tuwe wakweli.. pamoja na ulegelege wa kukusanya mapato pale kivukoni kama mbunge na wadau wengine wanavyojaribu kutetea ila sh 100 jamani tangu 1995??!

Nchi hii watu wanapenda kuchekewa chekewa tu.. ndio maaana tupo hapa tulipo naskia na waziri mkuu kasitisha hizo bei mpya.. huu ni uendawazimu na upuuzi kuliko yote! kwa hili Pinda kakosea sana ndio maana watu wamekufa mabondeni kwa ajili ya upuuzi huu huu wa kuchekea na kutaka kumfurahisha kila mtu

samora10
hapa umepotoka ndugu yangu, laiti kama ungejua wajibu wa serikali kuhusu kuweka miundo mbinu imara kwa raia wake usingependekeza huu uzi wako hapa, hiyo tshs.100 unayoona ni ndogo ajabu haifiki yote sehemu husika, naweza sema ni kubwa mno kulingana na mapato yanayopatikana pale kivukoni kwa siku ambapo bahati mbaya sehemu kubwa ya hayo mapato yanaishia kwenye matumbo ya wajanja, sikuungi mkono kwa hili,
 
Nadhani tatizo la Magufuli ni kuwa muwazi zaidi. Anasema kile kilicho moyoni mwake bila chenga! Pengine ajifunze ku-smile wakati anatatukia balaa.

On a serious note - Hivi hiki kivuko kingekuwa chini ya 'mwekezejai' nauli ingekuwa kiasi gani? shs 100/=?
Ushauri wangu kwa watu wanaoishi Kigambo, msihame, huku nauli haikamatiki ndugu zangu! shs 100?
 
Waziri wa ujenzi John Magufuli amekwenda kivukoni kutuliza hali ya hewa baada ya uongozi wa vivuko hivyo kupandisha nauli zaidi ya asilimia miamoja bila sababu za kueleweka!
Nitawajuza habari zaidi baadae!

Updates!

Taarifa iliyotolewa hapa nikuwa Waziri mkuuMh Pinda ni kuwa amesitisha nauli mpya za vivuko!
Hii ni kwa mujibu wa mr Magufuli PM


Ni kwa vivuko vyote nchini au ni hapa Dar es Salaam peke yake? Tunaambiwa hakuna kivuko kinachotoza nauli ya chini kama hapa Dar es Salaam, sasa kwa nini huyu Waziri mkuu hakuwahi kushusha nauli sehemu zingine? Au watu wa Kigamboni ndio wenye maisha magumu kuliko sehemu zingine? yale yale ya kusema tunataka posho kwa sababu gharama za maisha Dodoma zimepanda!
 
Majid, hakuna kuomba radhi!!! Hawa watu walimzomea. Kama hukumzomea basi wewe hauhusiki na kauli hiyo. Walikosa ustaarabu, kuzomea ni udhalilishaji mkubwa, hakuna anayeweza kuuvumilia. Najua utasema kuwa yeye ni kiongozi, lakini equally, nasema pia na waongozwaji wana wajibu kuwa na heshima na adabu.

swali la kujiuliza je ni nani wa kwanza kutoa kauli? Alitoa hiyo kauli ndio akazomewa au alizomewa kwanza ndio akatoa hiyo kauli?
 
Shirika la ndege TZ lilianza na ndege nyingi lakini zimekufa moja baada ya nyingine hadi ikabakia moja ambayo na yenyewe ilikuwa mbovu ndio imeanza kazi hivi karibuni. Ukifuatilia undani wake, utakuta ni matatizo ya kuleanaleana tu na kuogopa kuchukua maamuzi magumu. Ukweli kuna angala zile gharama za uendeshaji zinatakiwa zifahamike ili ilinganishwe na kile kinachopatikana kisha ijulikane kama kuna upungufu nani aubebe.

Kuna mchangiaji amesema TEMESA inapata fedha toka mfuko wa barabara kwa ajili ya kuendeshea vivuko, hili sio kweli hata kidogo!

Endapo TEMESA itakaa kimya bila kupiga kelele sasa wakati vivuko hivi vikiwa vipya, utafika wakati vivuko hivi vitakapoanza kuhitaji matengenezo na yakawa hayapatikani, huduma itakosekana. Ikifikia hatua hiyo, wananchi hao hao akiwemo Mh. Mbunge wao, watakuwa wa kwanza kurusha madongo.

Hii inanikumbusha rafiki yangu aliyeniomba nimwazime gari asafiri nalo umbali wa karibu km 500 kwa kigezo kuwa gari bado ni nzima yeye ataweka mafuta (dizeli) ya kwenda na kurudi. Kwa mtazamo wa watu wengi, kwao gari ni dizeli tu na kusahau kuwa kuna service, tear and wear na kwamba unatakiwa ufike mahali, gari hiyo ikizeeka inunuliwe nyingine.

Vivyo hivyo kwa upande wa vivuko, watu watasema ni vipya na vimenunuliwa na Serikali, sawa. Lakini baada ya kununuliwa vimekabidhiwa kwa TEMESA ili ivihudumia kwa ajili ya kuvusha abiria na mali zao. Vinahitaji kuhudumiwa na muda utafika vitazeeka vitahitajika vingine. Mimi nahisi huo ndio mtazamo wa TEMESA kwamba wana maono ya siku za usoni. Kwa hiyo nauli zimepanda, tuwasubiri watuonyeshe jinsi watakavyoboresha huduma zao.

Na kwa upande wa abiria, badala ya kulilia lia kuwa kuna ufisadi, watueleze nani amewahi kuuona uongozi na kuueleza kuwa fulani anahujumu kivuko hicho kimapato akadharauliwa? Kama kuna biashara mahali basi ujue kuna muuzaji na mnunuzi. Kwa maana hiyo kama kuna wizi kama wa mafuta, wananchi na wenye wanahusika kuhujumu, lasivyo, kama wasingeyataka wangetoa taarifa ili mitego iandaliwe wahusika wakamatwe!

Taarifa zilizopo, wanaokamatwa kwa kuzungusha tiketi au wizi wa dizeli wanakamatwa na viongozi wa TEMESA wakishirikiana na askari na baadhi ya raia wema.

Nafikiri tuache kulalamika, ifike mahali mtu unapotoka nyumbani kwako ama kwa miguu, gari, guta au miguu, ujiulize safari yako ina tija? Isije kuwa safari zinapangwa kwa sababu ya usafiri kuwa wa gharama nafuu!
 
Dr. Magufuli kwa kujua kwamba yeye ndiyo mhusika wa hilo ndo maana kaenda kulitatua. Kwa upande wa kikwete akiwa kama msimamizi mkuu wa maswala ya uchumi wa nchi hatujaona hatua za maana kuchukua zaidi kusingizia uchumi wa dunia. Ameshindwa kuwadhibiti wafanyabiashara, mfn ni aibu bei ya sukari kuwa kubwa mikoa ya viwanda kuliko eneo lingine, kwanin petrol/dizel inakuwa na bei ndogo inakoshukua. Tafakari udhaifu wa kiranja mkuu jk msimamizi mkuu

Mkuu, retail prices za cement ziko juu kwenye viwanda (Tanga, Dar na Mbeya) kuliko Morogoro: TAFAKARI
 
Kwa kwawaida serikali haifanyi biashara.Je kwa nyongeza hizi za gharama za vivuko ni biashara au ni huduma kwa jamii au watanzania wanyonge kama wa kigamboni waliokata tamaa na wasiojua kesho yao iko wapi.

Hiyo sio biashara, basi ni kuchangia huduma kama unavyochangia kwenye huduma za hospitali na shule, maji
 
Kaka hawa jamaa wa vivuko ni kiboko yaani kuanzia tar 1 hadi mtoto mchanga analipa ukiwa hata na kimfuko cha mboga unakilipia huu ni wizi na hata siku moja sijawahi kusikia kwenye bajeti ikisema miongoni mwa vyanzo vyake vya mapato ni vivuko
ukondoo wetu utatufanya ifike mahali tuambiwe tulipie hata nguo na viatu tulivovaa mbona wameshajua watanzania ni kama kondoo tu hata mtoto mdogo anaweza kuwachunga bila tabu, "asiweza kulipa anaweza kupiga mbizi baharini akavukia upande mwingine"
 
Kwa upande wangu naona makufli yuko sahihi sema kauli aliyo tumia ndiyo mbaya sana. Tatizo letu watanzania tumekuwa watu wa kulalamika kwa kila jambo hata kama liko sawa. Mbona uwa hamlalamiki inapofka jioni na makodakta wa daladala wakapandisha nauli badala ya 300 ikawa 500?
Sasa nauli ya kvuko toka mwaka 1995 ni shs 100 leo imepanda ndo basi mmeanza lalamika.

Kinacho nishangazani ile hali ya viongozi wetu kupenda kumfurahisha kila mtu kama pinda na hili suala ndilo limetufikisha hapa tulipo. Huwezi kumfurahisha kila mtu mambo mengine hayanabudi kufanyika hata kama watu flan hawatafurahi.

Najua watu wanaoishi mabondeni wangehamisha kwa kulazimishwa wakati mvua haijaanza kunyesha watanzania mngepiga kelele ooh wanaonewa ooh mara hivi mara vile. Lakini baada ya maafa ndiyo mnaona umuhimu.
BADILIKENI BWANA
 
Mwacheni mkuu awaongezee tu nauli, huku kwetu kuna kivuko cha kutoka Lugezi Ukerewe kwenda Kisorya Bunda, nauli yake kama sikosei ni shs 500 na umbali wake hautofauni sana na wa kigamboni kwenda ng'ambo ya pili ya daresalam. sasa inakuwaje nyie huko iwe 100 na sisi iwe 500? Ila Mheshimiwa Magufuli Pombe ulikosea tu kusema wapige mbizi kama hawana sh 200! Mara mia ungesema waogelee kuliko kuwadhihaki wapige mbizi
 
Mwacheni mkuu awaongezee tu nauli, huku kwetu kuna kivuko cha kutoka Lugezi Ukerewe kwenda Kisorya Bunda, nauli yake kama sikosei ni shs 500 na umbali wake hautofauni sana na wa kigamboni kwenda ng'ambo ya pili ya daresalam. sasa inakuwaje nyie huko iwe 100 na sisi iwe 500? Ila Mheshimiwa Magufuli Pombe ulikosea tu kusema wapige mbizi kama hawana sh 200! Mara mia ungesema waogelee kuliko kuwadhihaki wapige mbizi

Watu wa Dar kwa kulalamika!
 
Ingawa huwa simfagilii Magufuli kwa baadhi ya mambo yake lakini kwa hii nampongeza. Walipe hiyo 200! Tupunguze safari zisizo na tija kama hiyo 200 wanaona ni gharama.
 
Ingawa huwa simfagilii Magufuli kwa baadhi ya mambo yake lakini kwa hii nampongeza. Walipe hiyo 200! Tupunguze safari zisizo na tija kama hiyo 200 wanaona ni gharama.


Fikiria zaidi ya vile unavyoona pua yako
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom