Utaratibu wa nauli mpya za tarehe 8/12/2023 zinahitaji ufafanuzi zaidi

Southern Giant

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
321
550
Swala la nauli mpya zilizoanza kutumika tarehe 8/12/2023 bado linatia wasiwasi, LATRA wanadai wametoa elimu ya kutosha kabla ya kuzifanyia mabdiliko nauli lakini ajabu walengwa wengi ambao ni abiria wa hivyo vyombo vya usafiri(daladala) nami nikiwemo sikusikia hiyo elimu iliyotolewa na mamlaka.

Hapo ilibidi nitafute ukweli wa hili jambo ili namimi niondokane na mkanganyiko huu, kwa kutumia simu yangu niliwapigia LATRA wanaodai wametoa elimu ya mabdiliko haya ya nauli bahati nzuri ililia miito miwili na kupokelewa, mara baada ya kutambuana kwa majina maongezi yalianza mara moja.

MIMI: Je kuna mabadiliko yeyote ya nauli za daladala?

LATRA: Ndio kuna mabadiliko na yameanza kutumika tangu tarehe 8/12/2023.

MIMI: Hayo mabadiliko ya nauli, nauli zimeongezeka au zimepungua?

LATRA: Hazijapungua ila zimeongezeka.

MIMI: Zimeongezeka kwa kiasi gani?

LATRA: Zimeongezeka kulingana na Kilomita za sehemu husika mfano kwa mkoa wa DSM kutoka Magomeni kwenda Manzese ni shilingi 6000, hapo mwanzo ilikua 500 lakini hivi sasa ni 600 kwasababu magomeni kwenda kinondoni ni ndani ya kilomita 10 kwa kupitia morogoro road.

Ilinipa shauku zaidi ya kuhitaji kufaham mtu anayetoka Gerezani kwenda Vikindu kupitia kilwa road anapaswa kutoa kiasi gani cha nauli kwasababu hii safari ni Kilomita 19.9 ni sawa na Kilomita 20 kwa mujibu wa google map.

LATRA: Kwa safari ya gerezani kwenda vikindu nauli yake ni 1100 ambapo kabla ya madiliko ilikua 850.

MIMI: Chati yenu iliyopo katika website yenu inamtaka abiria alipie 800 kwasababu yupo ndani ya kilomita 20 je hapa hamuoni kunasintofahamu na wizi wanaibiwa abiria.

LATRA: Hiyo ndio nauli halali kutokea gerezani kwenda vikindu 1100, je unachangamoto nyengine nikusaidie?

MIMI: Hapana sina.

LATRA: Tukutakie siku njema.

Maongezi yetu yaliishia hapo.

Tukirudi katika chati yao ya nauli mpya kwa daladala ni kama ifuatavyo;-

Umbali wa Njia:
1. Usiozidi Kilomita 10 - SH600
2. Kuanzia Kilomita 11 hadi 15 - SH700
3. Kuanzia Kilomita 16 hadi 20 - SH800
4. Kuanzia Kilomita 21 hadi 25 - SH900
5. Kuanzia Kilomita 26 hadi 30 - SH1,100
6. Kuanzia Kilomita 31 hadi 35 - SH1,300
7. Kuanzia Kilomita 36 hadi 40 - SH1,400

Nakumbuka kipindi cha nyuma LATRA walikua wakiongeza 100 au 50 kwa njia zote lakini iweje hivi sasa kunaongezeko la hadi 250 kwa baadhi ya njia.

Haya majibu ya LATRA bado hayajaniridhisha nimeona niliwasilishe humu ndani kwa ajili ya ufafanuzi zaidi kwa wajuzi wa mambo, Asanteni.
 
Back
Top Bottom