Mr. Kuku afikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kufanya Biashara Haramu ya Upatu kwa kukusanya bilioni 17

Maana ya upatu ni nini ??

Kesi ya Mrkuku ni yepi hapa

1)kufanya upatu ?

2)kutokuwa na leseni ya Biashara ?

3)kutaperi ?

Maswali ni mengi.

Je ile model ya biashara kwa Tz ni haramu ??
 
Yani watu wamepigwaa parefu mamaee...! Sema jamaa akitafuta wakili imara anaweza chomoa hii kesi alafu akasepa na Mpungaa..
Unamjua 'Diii Piii Piii' wa awamu hii ya mjomba Jiwe?
Huyo mzalendo aliyetufundishia vijana nidhamu ya pesa hachomoi msala wa uhujumu uchumi.
Kutoka hapo akubali kosa alipe mpunga mrefu.
 
Hizo hela kama vile za DECI zilivyopotea kimya kimya na hizi nazo hamtajua zimetoweka vipi.

Hapo hiyo kesi itaoigwa danadana. Jamaa watamkatia mpunga kidogo atakwenda jificha mafichoni... Wakimpatia hata bilioni moja tu inamtosha kuanza maisha mapya..... Wao CCM wanabakia na hizo bil 16 wanapeleka katika kampeni.

Kwa kifupi m'mewachangia pesa za kampeni CCM.....
 
Kijana amebuni njia yake yakujipatia cake ya Taifa, jamaa wa Taifa wameona amezikusanya wameamua kufanya yao.Kwanini wasingemzingua kabla hazijafika kiasi hicho?
Kuna kitu kinaniambia viongozi wa serikali wapo behind these ponzi schemes everytime zinapotokea.

Maana haiwezekani wasubirie hadi zijae zikishakuwa nyingi ndio paaap wanatokea.

Na wakishazichukua hizo hela kesi mtasahau.

Watajifanya muhusika atafungwa kumbe jamaa wanamkatia mpunga wake wao wanabakia na salio.

Sasa bilioni 17 ni hela kidogo..... Wakisema wanampatia hata bilioni 3 tu hapo jamaa si tayari ameshayapatia.

Anakwenda zake huko mkoani anajificha ananendelea na biashara zake..... Akipotea miaka 5 tu tunamsahau hata akija mjini tumeshamsahau.

Serikalini kuna mambo ya kichoko sana.
 
Hahaha watanzania wanapenda sana hizi, waweke pesa mahala wao wakalale wakingoja faida.

Hakuna mtu wa kukufanyia kazi ukiwa umelala nyumbani, ona sasa pesa inaenda kutaifishwa na serikali na hamtalipwa, labda mfungue kesi ya madai.
Huwezi pata hiyo pesa yako hata mia. Ukienda wanakufungulia kesi ya kushiriki upatu ambao ni kinyume na sheria.
 
Ajira hakuna, tukijiajiri mnatukamata kwa makosa ya uhujumu uchumi. Yaani sijui tufanye nini kwenye nchi yetu hii.

Nadhani mpaka mwenzangu amekusanya hela yote hiyo mamlaka zilikuwa wapi kumchunguza toka mwanzoni???

Imagine Mr kuku ni mlipa kodi mzuri. Binafsi naona huku ni kukatishana tamaa...Lakini ipo siku nchi hii itaongozwa na chama kingine ila si CCM!

Mwenye sikiona asikie....
 
Hakuna pesa ya mtindo huo Mkuu, kila siku wanalizwa lakin hayakomi tu tangu lini pesa inatafutwa kwa kutumia vikundi, eti mtu ufanye nae share, vicoba, na sijui jumuiya hapa wajanja ndio watakao kula. Baadae inaanza migogoro na maujinga kibao hata kampuni tu zinaleta shida sembuse hayo ya kumwamini mtu.
Pesa hutafutwa na mtu binafsi na si vinginevyo.
[/QUOTEmjini wajinga hawaishi mkuu
 
Back
Top Bottom