Mhasibu wa Halmashauri ya Jiji Dar afikishwa Mahakamani kwa kutakatisha Tsh. Bilioni 8.9

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1688128998621.png

Mhasibu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Alinanuswe Mwasasumbe (60) amefikishwa katika Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo ya kughushi nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Sh 8.9bilioni.

Mwasasumbe ambaye ni mkazi wa Mbagala Maji Matitu, amefikishwa mahakamani hapo leo Juni 30, 2023 na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali Mwandamizi Fatuma Waziri akishirikiana na Veronica Chimwanda, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Ferdinand Kihwonde.

Wakili Waziri amedai mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 34/2023 yenye jumla ya mashtaka 13.

Kati ya mashtaka hayo 13; mashtaka 10 ni ya kughushi, moja la kuisababishia Halmashauri ya Jiji hasara, moja la kutakatisha fedha na jingine ni matumizi mabaya ya madaraka.

Awali, kabla ya kusomea mashtaka yake, Hakimu Kihwonde, amesema mshtakiwa hatakiwa kujibu chochote kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu uchumi na mahakaka hiyo haina uwezo wa kusikikiliza shauri hilo hadi kwa kibali Maalumu.

Akimsomea mashtaka yake, Wakili Waziri amedai katika shtaka la matumizi mabaya ya madaraka, mshtakiwa anadaiwa kati ya Julai Mosi 2019 na Juni 30, 2021 katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mtumishi wa umma kwa nafasi ya Mhasibu, alitumia Mamlaka yake vibaya kwa kushindwa kuweka kiasi cha Sh8.9 bilioni kwenye akaunti za jiji hilo zilizopo katika Benki ya NMB, CRDB, NBC, DCB.

Kiasi hicho cha fedha ni mapato yaliyokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya Jiji hilo na hivyo kujipatia manufaa yasiyofaa kiasi cha Sh8.9 bilioni.

Miongoni mwa mashtaka ya kughushi nyaraka, mshtakiwa anadaiwa Februari 28, 2021 katika ofisi hizo, kwa nia ya kudanganya, mshtakiwa alitengeneza nyaraka ya uongo yenye kichwa cha habari 'Kurudishwa fedha iliyotumika kuanzia Februari Mosi Hadi Februari 28, 2021' akionyesha kiasi cha Sh5.9 milioni kimerudishwa kama ilivyoombwa ili kitumike kuwalipa vibarua na matumizi mengine, wakati akijua ni uongo.

Katika shtaka la kutakatisha fedha, mshtakiwa anadaiwa katika kipindi hicho, alijipatia Sh 8.9 bilioni kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wakati akijua kuwa fedha hizo zinatokana na Makosa tangulizi ya kughushi nyaraka.

Katika shtaka la kuisababishia hasara Halmashauri ya Jiji, Dar es Salaam, mshtakiwa anadaiwa kati ya Julai Mosi 2019 na Juni 6, 2021 kwa makusudi na huku akinia kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria, mshtakiwa aliisababishia hasara ya Sh8.931, 589,500.

"Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa shauri hili bado unaendelea hivyo tunaomba terehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amedai Wakili Chimwanda.

Hakimu Kihwendo baada ya kusikiliza shauri hilo, ameahirisha hadi Julai 10, 2023 itakapotajwa.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalowamkabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

MWANANCHI
 
Yaaani ni mwendo wa ma-Biii na ma-Biiii na ma-Biiiiiiiii tu (in M. Kitenge's voice). Kweli Bongo ni nchi tajiri. Ingekuwa maskini ingeshafirisika ile kitambo sana.
 
View attachment 2674219

Halafu hawa ukiwakuta maofisini mwao wanakuwa kama miungu watu na jeuri ya kutisha,huyu atakuwa alikuwa anakula na wakubwa zake, ndio kama akina Mwakibibi, kwa umri wa miaka 60 sijui alikuwa bado anasubiri nini ofisini badala ya kusepa kwenda Afaghanistan.
 
Back
Top Bottom