Mwanza: Salma Abdallah afikishwa Mahakamani kwa kujihusisha na matumizi ya bangi

Abby Uladu

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
2,031
4,236
IMG_0755.png

Mkazi wa Lumala wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Salma Abdallah (37), amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo na kusomewa shtaka la kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.

Salma amesomewa shtaka hilo, katika kesi ya jinai namba 152/2023 ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 17 (1) (b) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya sura ya 95 toleo la mwaka 2019.

Akimsomea shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Amani Sumari, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Monica Mweli amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Oktoba 1, 2023 na Oktoba 27 eneo la Lumala wilaya ya Ilemela.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa amekana na kurejeshwa rumande kutokana na kutokidhi masharti ya dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kusaini bondi ya maneno ya shilingi milioni mbili kwa kila mmoja, kitambulisho pamoja na barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa ambapo mshtakiwa alijibu hana wadhamini hao.

EATV
 
Huyu kuna jambo lingine tu linamsumbua. Kesi za vijiti tena unavuta mwenyewe polisi hawana muda wa kukushikilia muda wote huo na kupelekana mahakamani.

Labda kama ni pusha ana kg za kutosha, ila kuvuta tu tena Mwanamke, lazima kuna jambo jingine sio bure.
Lipo nje ya panzia hili huyu itakuwa kuna kitu wamepishana au anasingiziwa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo anakwenda kuongeza idadi ya mahabusu unnecessary. Kweli sheria ipo ila issue nyingine zingetakiwa ziishie kwa muendasha mashitaka. Uncle Magu haku deal kabisa na watumiaji wadogowadogo wa madawa bali yeye alikomaa na importers na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Serikali inakwenda ingia gharama ya kumuhudumia kwa issue ndogo. Nahisi kwenye haki jinai kutakuwa na amendments na baadhi ya vifungu vya sheria
 
Huyu kama hukumu itatoka anaweza Kula mingapi? Mkuu

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Kivip tusema hajafanya au?

Au itakuwa wamemsingizia?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Yote mawili. Wapo watu wanahittilafiana au wana bifu kidogo tu kinatengenezwa kisa ili kukomoana.
Kama amejihusisha i.e. ameuza, amevuta au amesafirisha au amewezesha matumizi ya bangi.
Kusingiziwa inafanyika sana kwani kama utaratibu wa upekuzi haukuzingatiwa, majamaa hukuwekea bangi na kudai eti wamekukuta nayo.
 
Hizo nguvu kazi tungeziwekeza kuwashika walamba asali huenda huyu Salma au wale ambao wanao-abuse drugs kwa kukosa muelekeo wangekuwa na muelekeo.....

Kama mlipa Kodi nasema bora kina Salma kumi waachiwe na Mlamba asali mmoja Ashikwe Hususan wale aliotuonya Ndugai (Wauzaji wa Mali za Umma)
 
View attachment 2800141

Mkazi wa Lumala wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Salma Abdallah (37), amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo na kusomewa shtaka la kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.

Salma amesomewa shtaka hilo, katika kesi ya jinai namba 152/2023 ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 17 (1) (b) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya sura ya 95 toleo la mwaka 2019.

Akimsomea shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Amani Sumari, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Monica Mweli amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Oktoba 1, 2023 na Oktoba 27 eneo la Lumala wilaya ya Ilemela.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa amekana na kurejeshwa rumande kutokana na kutokidhi masharti ya dhamana ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kusaini bondi ya maneno ya shilingi milioni mbili kwa kila mmoja, kitambulisho pamoja na barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa ambapo mshtakiwa alijibu hana wadhamini hao.

EATV

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Marekani na baadhi ya mataifa Bangi inauzwa Pharmacy, hapa kwetu ni biashara haramu!!!
 
Back
Top Bottom