Morsi killed by El-Sisi Regime

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
"OPERATION SINAI EAGLE" ILIZIMA DEMOKRASIA NCHINI MISRI, NA IMEKATISHA MAISHA YA Dr MOHAMMAD MORSI.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Wednsday-19/6/2019
Moshi, Kilimanjaro - Tanzania.

Demokrasia imepata pigo kubwa kufatia kifo chenye ukakasi na utata mkubwa, juu ya Mohamed Morsi kufariki ghafra jana na kuzikwa kimya kimya leo, hii inadhihirisha wazi kiasi gani utawala wa General Abdel Fattah El-Sisi unavyo pambana kuhakikisha anajiweka mahala salama kupitia mgongo wa masrahi ya Marekani na taifa la Israel, Mohammed Morsi ambae pamoja na kuwa gerazani kabla ya umauti kumkuta aliendelea kusisitiza kuwa yeye ndio raisi halali wa taifa la Misri jambo lilo mpa hasira zaidi General Abdel Fattah El-Sisi.

Mohamed Morsi aliyekuwa rais wa wa awamu ya tano wa taifa la Misri amefariki dunia mapema jana akiwa katika mahakama ya jinai ya Cairo (Cairo Criminal Court), umauti ulimkuta hapo mahakamani baada ya kuzimia ghafra na kukimbizwa hospital ya Umrah iliyopo katikati ya Cairo ambapo hata hivyo walithibitisha kuwa alikuwa ameshakufa mda mrefu Kabla ya kufika katika hospital hiyo. Morsi alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia kabla ya kupinduliwa na jeshi la Misri Julai 3 2013 kupitia ile "Operation Sinai Eagle" iliyoratibiwa na Marekani kupitia vikosi vya Mossad vya Israeli kwa ushirika na maaskali wa ngazi ya juu katika jeshi la Misri.

Operation kama hii iliwahi kuendeshwa nchini Misri mwaka 1956 wakati ule wa mgogoro wa mfereji wa Suez (SUEZ CRISIS 1956) wakati huo operation hiyo ilipewa jina la "Operation Kadesh/Sinai" iliyo ratibiwa na mataifa ya Marekani, Israel, United Kingdom na France operation ambayo ililenga kumuondoa madarakani Abdel Nasser Gamal na kurejesha usimamizi wa mataifa ya magharibi katika mfereji wa Suez (Suez canal) operation ambayo ilishindwa kufanikiwa. Unaweza kutembelea link hiyo kuona namna mikakati ya kuidhibiti Misri haikuanza leo... See link : https://tinyurl.com/yazu87ae

Mohamed Morsi alikuwa mwanasiasa mashuhuri wa Misri na rais wa tano wa taifa hilo kuanzia Juni 30 2012 baada ya Vuguvugu la siku 18 lilopewa jina la "Operation Tahrir square au Mohammed Al-Baradei movement", baada ya kuwa raisi kwa muda wa mwaka mmoja ambao utawala wake ulitamatika Julai 3 2013, alipopinduliwa na mkuu wake wa majeshi Abdel-Fatah El-Sisi, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake yaliyokuwa yamesukwa na Marekani kwa ushirika wa Israeli na vikosi vya jeshi la Misri.

Baada ya kuondolewa madarakani kiongozi wa muda mrefu Hosn Mubarak, Morsi alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia katika historia ya taifa la Misri. Morsi ni msomi aliefikia ngazi ya PhD na alikuwa mwanachama mwandamizi wa kundi la Udugu wa Kiislamu, akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa tawi la kisiasa la kundi la Chama cha Haki na Uhuru FJP, kilichoundwa na Udugu wa Kiislamu baada ya mapinduzi ya mwaka 2012, baada ya Morsi na wengine kutoka gerezani. Mursi aligombea urais na kushinda katika kiti hicho katika duru ya pili iliyompabanisha na Ahmed Shafik, waziri mkuu wa mwisho wa serikali ya rais Hosni Mubarak.

Morsi aliibuka katika siasa za nchini Misiri na kupata uungwaji mkono mkubwa baada ya ile iliyoitwa "Vuguvugu la Kialabu ambapo kwa nchini Misri ilitafsilika kama Operation Taharir square" ilioanzia nchini Algeria na kutamatisha tawala nyingi za viongozi wa nchi za kiarabu walio kuwa wamekaa madarakani muda mrefu, mara baada ya maanadamano ya umma kutamahalaki jijini Cairo pale katika viwanja vya Tahrir Squre yaliyo tamatisha utawala wa Housen Mubalak tarehe ya 18 Januari mwaka 2011 ulikipa nguvu chama cha undugu wa kiislam na kumuibua Mohamed Morsi.

Uchaguzi wa baadae wa juni 2012 ulikipa ushindi chama cha undugu wa kislamu (Muslim Brotherhood) na kukilejesha tena katika dira za kisiasa hata hivyo Mohammed Morsi alishinda uchaguzi huo kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo mwaka 2012,

Lakini aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wake kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika nchini humo kuupinga utawala wake. Kwa nyakati tofauti Morsi alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ugaidi na mpaka umauti unamkuta alikuwa anakabiliwa na mashitaka mengine katika mahakama za nchini humo huku akiwa kafutiwa adhabu ya kifo katika kesi yake ya awali.

Kuondolewa kwake ilikuwa ni mbinu chafu kupitia mkakati uliipangwa na taifa la Marekani kwa uratibu na Israel mkakati huu uliitwa "Operation Snai Eagle" ambao mpango wa kuidhibiti Misri ilianza toka mwaka 2008 kupitia mpango maalumu kwa kuandaliwa Mohamed El-Baradei (kisa hiki ntakuja kukieleza siku nyingine vizuri kwa kuangazia mkakati huu na namna alivyo andaliwa Mohamed El-Baradei), lakini leo tutaangalia operation hiyo hiyo ya namna na mpango wa Mosri kuondolewa madarakani.

Mpango wa kuondosha kwake unahusianishwa na chama chake cha Undugu wa kiislam (Muslim Brotherhood) kuwa kitovu cha mabadiliko nchini Misri yanayoweza kuhatarisha masrahi ya Marekani na uwepo wa Israel mashariki ya kati, hii ni kwasababu chama hicho nchini Misri kina ushawishi mkubwa hasa katika chuo cha Al-zhar chuo ambacho kimezalisha wasomi wengi ambao wamerudi kua viongozi kwenye nchi zao pamoja na msimamo mkali katika mipango ya kuunda jamuhuri ya kiislam yenye ushawishi nchini Misri.

Lakini pia Ikumbukwe kuwa Al-zhar kina tawi la vijana la Muslim brotherhood lenye nguvu kubwa lenye lengo ya kutaka mataifa ya kiarabu yawe huru yaachane na mfungamano wa nchi za kimagharibi pamoja na kuilinda Palestine dhidi ya Israeli. Hii ni kwakua muanzilishi wa Hamas alikua mwanachama wa Muslim Brotherhood Kwahiyo wayahudi wa Israel wangekubali Muslim Brotherhood ya Morsi itawale Misri, Hamas wangepata support kubwa kutoka kwa serikali ya Misri, jambo ambalo lingewapa wakati mgumu katika adhima yao ya kuikalia Palestine na hilo lingewafanya wayahudi wapate tabu sana kama Mohammed Mosri angesalia madarakani.

Kuna ushahidi wa kutosha kwamba general Sisi raisi wa Misri wa Sasa alidhaminiwa kufanya yale mapinduzi na Israel kupitia mgongo wa Marekani ili kuilinda Israel na hii inathibitika kuwa baada ya Sisi kuingia madarakani amekuwa upande wa Israel kwakua Israel wanapokuwa wanaishambulia Gaza, Misri ya Sisi huwa wanafunga mpaka wa Rafah ili kuwazuia wapalestine wasipate msaada wowote, Ikumbukwe kuwa mpaka huu Rafah ni mpaka ambao unatenganisha baina ya Misri na Palestina katika ukanda Gaza, eneo hili hutumiwa na Hamas katika harakati zake kijeshi Ikiwa kama kuchumba mahandaki ya kupitishia chakula na silaha, mahandaki hayo ambayo huwa yanachimbwa kwa msaada wa Iran.

Hivyo kwa vyovyote vile kwa masrahi ya Marekani na Israeli ilikuwa ni lazima Morsi na chama chake cha Muslim Brotherhood kuondolewa madarakani ili kuifanya Israel kubaki salama, kwaiyo mpango wa kumuondoa Morsi uliipangwa Washington na kupata baraka zote Tel Aviv Israel, mpango wa kwanza ilikuwa ni kuwarudisha wananchi mtaani ili kuwaaminisha kuwa utawala wa Morsi utakiuka haki za wamisri na kugeuka kuwa kaa la moto kwao, mpango huo utakapo kamilika vyema wataihusisha jeshi kwa kuingilia kati kwa kufanya mapinduzi baridi kumuondoa Morsi madarakani.

Baada ya mpango huo wa pili kukamilika itafuatiwa na kukufuta chama cha undugu wa kiislam (Muslim Brotherhood) na kumtia kizuizini Morsi kwa kumpa kesi ili kumdhofisha yeye na wafuasi wake. Kumuua ilikuwa ni mpango mbadala wa kummaliza kabisa Ikiwa itaonekana ushawishi wake kuongezeka, kumdhibiti Morsi kulikwenda sambamba na kuachiwa huru kwa aliyekuwa mtangulizi wake Hosn Mubarak ambae chini ya utawala wake alifunguliwa mashtaka kadhaa ya kuhusika katika mauaji ya waandamanaji wakati wa vuguvugu la Taharir square.

Husni Mubarak ambae alikaa 'kizuizini' kwa takribani miaka 6 alikuwa ni mpango kazi mwingine ambae kupitia yeye ilitakiwa kuwaaminisha watu kuwa utawala wa General Sisi ulikuwa mkombozi kwa Wamisri, uthibitisho wa hili ni juu ya kizuizi cha ajabu alikowekwa Mubarak maana alikuwa chini ya askari wake! Siku zote Mubarak alikuwa anajulikana ni 'mgonjwa' na akifikishwa mahakamani ndani ya machela. Ila baada tu ya kuachiwa huru Mubarak aliweza kusimama na kupungia watu mikono kupitia dirisha la kasri lake pale Heliopolis! yani Mgonjwa kapona kwa furaha! Hii yote ilikuwa mkakati maalumu bila ya wale wote walioendesha mapambano kujua kuwa ile ilikuwa picha la kimarekani lilopangwa Washington na kuratibiwa Tel Aviv

Toka kupinduliwa kwa Morsi Julai 3 2013 alikuwa mtu gerazani na mahakamani mpaka pale mauti yenye utata yalipo mpata mapema jana akiwa katika vyumba vya mahakama jijini Cairo. Na kufanyiwa mazishi ya kimya Mashariki mwa jiji la Cairo yasiyo kuwa na heshima yoyote ile chini ya ulinzi mkali wa askali wa serikali, Wakili wake ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kuwa Morsi alizikwa Mashariki mwa jiji la Cairo asubuhi ya Jumanne bila kuruhusu watu wa nje kuhudhuria isipokuwa familia yake tu ndio ilipewa kibali cha kuwepo.

Mohammed Morsi, aliyekuwa na miaka 67, alikuwa kizuizini tangu alipoondolewa madarakani kiharamia kupitia Operation Sinai Eagle mwaka 2013. Hata hivyo kifo chake chenye utata imesababisha makundi kadhaa ya watetezi wa haki za binaadamu, ambayo yalikosoa mazingira ambayo Morsi aliwekwa,wametoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kifo chake, hayo yamefatia baada ya familia yake na wanaharakati wengi kote duniani wamezungumzia kifo chake na muda ambao aliwekwa katika seli ya peke yake, akizuiwa kutembelewa na wanasheria na familia yake. Mtoto wake Abdullah Mohamed Morsi, ameliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters kuwa siku ya Jumatatu baada ya kifo cha baba yake mamlaka za Misri ziliikatalia familia yake kufanya maziko katika makazi yake.

Mohamed Mosri ambae kifo chake kimewasikitisha watetezi wa haki na wapenda mageuzi wengi duniani akiwemo raisi wa Uturuki Edogan Typ pamoja na Mfalme wa Qatar,Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, ambao walikuwa washirika wa karibu na Morsi wameeleza masikitiko yao kutokana na kifo chake kilicho gubikwa na ukakasi mwingi. Pia Mbunge wa nchini Uingereza, anaeitwa Crispin Blunt, aliyeongoza jopo la wanasiasa kutoka umoja wa ulaya katika uchaguzi dhidi ya matendo yasiyo ya haki kwa wafungwa wa kisiasa nchini Misiri, ametoa tahadhari kuhusu kifo cha Morsi kufatia repot ya kutendewa ukatili kwa Morsi mwaka 2018, ametaka ufanyike ''uchunguzi huru wa kimataifa'' dhidi ya kifo hiki.

Huyu Mohammed Mosri ambae mauti yake yamesikitisha wengi duniani alizaliwa katika kijiji cha El-Awwadh katika jimbo lililopo kwenye delta za mto Nile la Sharqiya mwaka 1951. Alisomea Uhandisi katika chuo Kikuu cha Cairo katika miaka ya 70 kabla ya kuhamia nchini Marekani ambapo alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Uhandisi, Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru mwaka 2012 nchini Misri taifa lilopita uhuru mwaka 1922 na kuwa jamuhuri mwaka 1956, akiwa kiongozi mwandamizi wa kundi la kiislamu la Muslim Brotherhood ambalo kwa sasa limepigwa marufuku nchini humo kufatia serikali ya General Abdel Fatah El-Sisi kukiorodhesha chama hicho kama kikundi cha kisasi.

Mohamed Morsi atakubukwa kama raisi ambae utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano ya wanaharakati ambao walimshutumu yeye na kundi la Muslim Brotherhood kujilimbikizia madaraka na kuanzisha dola ya kiislam yenye msimamo mkali nchini Misri, Baada ya maandamano kuwa makubwa, na wafuasi wa Morsi kushambulia wapinzani wake, jeshi likiwa chini ya rais wa sasa Abdel Fattah El-Sisi liliendesha mapinduzi na kumng'oa Morsi madarakani, Juni 2013 mapinduzi ambayo yaliratibiwa na mataifa ya Marekani na mshirika wake mashariki ya Kati Israel.

Baada ya mapinduzi yale ya Juni 2013, Jeshi uliongozwa na Abdel Fattah el-Sisi liliendelea kupambana na wafuasi wa Mohamed Morsi kutoka chama cha Muslim Brotherhood (Undugu wa kiislam) na baada ya mapinduzi zaidi ya wafuasi wake 1,000 waliuawa Agosti 2013. Hata hivyo wafuasi wake kutoka Muslim Brotherhood, na chama chake cha Freedom and Justice, kijacho ishi uhamishoni katika nchi za Iran,Qatar na Turkey kimesema kuwa kifo cha Mohamed Morsi ni '' kitendo cha mauaji kilichotekelezwa na mikono ya General Abdel Fattah El-Sisi".

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copy rights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
FB_IMG_1560948358020.jpeg
IMG_20190619_162701.jpeg
FB_IMG_1560948395206.jpeg
 
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.comView attachment 1131818
Download Image
View attachment 1131819View attachment 1131820
Mtu akiwa na pesa nyingi au madaraka makubwa awe makini na maisha yake asijekufa kifo cha aibu,utata........mara ameuliwa na ndugu maramke mara marafiki maranan nk....
 
'Atakaye kubariki nitambariki na atakaye kulaani nitamlaani'
Hii kauli ni nzito sana...
Kazi nzuri mkuu.
 
Hivi unajua makabila mawili ya Israel kibiblia yametokea Misri yaani Manasseh na Ephraim kupitia Mwanamke wa Kimisri Asenath!!

By the way hii kauli ilikua kuhusu Abraham na uzao wake ambao kuna mataifa mengi tu sio Israel pekee kama wanavyotaka kutuaminisha.
 
Comred Mbwana Allyamtu nashukuru kwa uzi wako wa kiuchunguzi unaotufikirisha upande wa pili wa hili suala ila ningeomba utuweke sawa kidogo hapa.

1. Unasema El Baradei ni pandikizi la wazungu kuitawala misri. Nachojiuliza Mubarak alikuwa mtiifu wa marekani na hakuwa hostile kwa Israel pia Je nini kifanye wayahudi/marekani waandae pandikizi wa kuchukua serikali ilihali tayari walikuwa na mshirika wao yaani Mubarak kama Rais?

2. Kama El Baradei alikua pandikizi kwanini alijiuzuru baada ya Majeshi ya serikali kuua waandamanaji wa Muslim Brotherhood wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya Misri?? Yaani sielewi kivipi aandiliwe miaka zaidi ya 10 alafu wakati sahihi unapofika wa kumtoa Morsi ndio asalimu amri?

3. Mara baada ya Morsi kuchukua serikali kuna wakati alienda kusuluhisha mgogoro kati ya Israel na Hamas kinyume kabisa na msimamo wa Islamic Brotherhood chini ya Mohammed Badie wakati ule..... Je kivipi mtu aliyekua tayari kwa diplomasia kutawala kwenye mgogoro wa Mashariki ya kati apinduliwe!!

4. Wote tunakubali kuwa changamoto za uchumi zilikuepo na Morsi alifeli kushughulikia hivyo ikapelekea maandamano sasa unavyosema wayahudi ndio walihusika kuandaa maandamano kwa obvious reasons huoni kuwa ni kutafuta mchawi wa kumtupia lawama!! Yaani sielewi kwanini kupinduliwa kwa Mubarak kusiwe na mkono wa wayahudi ila Morsi kuwepo na mkono wakati changamoto zilizopelekea kumng'oa Mubarak ndio zilichangia kumng'oa na Morsi sababu hakuzishughulikia zote!!

Embu tusaidie hapa tuwekane sawa

Cc Malcom Lumumba
 
Hivi unajua makabila mawili ya Israel kibiblia yametokea Misri yaani Manasseh na Ephraim kupitia Mwanamke wa Kimisri Asenath!!

By the way hii kauli ilikua kuhusu Abraham na uzao wake ambao kuna mataifa mengi tu sio Israel pekee kama wanavyotaka kutuaminisha.
Hii kauli ilirudiwa kwa Yakobo wakati akiwa amelala kule bethel
 
Pia baraka hiz za Abrahamu Mungu aliendelea kuzirudia kwa mzaliwa wa kwanza wa uzao wa Abrahamu.
 
Lakini haimaanishi iliishia kwa Yakobo peke yake mkuu, ndio maana hata wagalatia inatambua waaminio wote kurithi baraka za Abraham. Ila Wayahudi wamejimilikisha baraka za Abraham kua zao tu ambao ni upotoshaji mkubwa sana.
 
Pia baraka hiz za Abrahamu Mungu aliendelea kuzirudia kwa mzaliwa wa kwanza wa uzao wa Abrahamu.
Mkuu ina maana ikirudiwa kwa Yakobo ndio imefutika kwa Abraham?? Nachojua ilianzia kwa Abraham hivyo imacover mataifa mengi sana soma 1 Peter na wagalatia sura ya 3 ile nzima utaona watoto wa Abraham wenye hizo baraka wamekuwa extended. Sababu Kibiblia Abraham ni baba wa mataifa mengi sio Israel tu.
 
Back
Top Bottom