Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,913
Ikhwanul Muslimiin ni harakati kongwe sana nchini Misri ambayo hatimae iliweza kupenya mataifa kadhaa ya kiislamu.
Upeo wa mafanikio wa Ikhwaan au muslim brotherhood ni pale chama hicho kilipoweza kupanda madarakani mwaka 2012 chini ya raisi Mohammed Morsi.Hiyo ni baada ya vuguvugu lililomuodoa madarakani raisi Hosni Mubarak.
Kiongozi huyo ambaye alikuwa injinia kielimu na aliyesomea na kufundisha nchini Marekani alionekana ni tishio kubwa kwa nchi za magharibi na nchi jirani ya Israel.Baada ya mwaka mmoja tu harakati pinzani dhidi yake zilifanywa na hatimae kupinduliwa na jeshi na kupelekea Elsisi kushika madaraka huku Mohammed Morsi akiwekwa ndani kwa tuhuma kadhaa za kuzushiwa.
Kumpindua Morsi na kukaa madarakani kwa Elsisi kulikuja kwa gharama kubwa sana ya mauwaji ya kikatili kuliko hata yale yaliyofanywa na China kule Tianmen square.
Pamoja na kuendelea kukaa madarakani serikali ya Elsisi imekuwa na hofu kubwa ya kupinduliwa tena na harakati za muslim brotherhood.
Nchini Misri kuna wafuasi wengi sana wa harakati hizo za ikhwaanil muslimiin na wamekuwa wakiwaunga mkono Hamas wakona ni kama muendelezo wa serikali yao iliyopinduliwa Misri.Nguvu kubwa waliyopata Hamas imetokana na kuungwa mkono na watu waliopo Misri ambao baadhi wana nafasi serikalini.
Kwa ujumla viongozi wakuu wa serikali ya Misri wameshindwa kuiunga mkono wazi wazi Hamas wakati huu wa vita kwa vle wanaiona ni muendelezo wa harakati za Ikhawaanul muslimiin.
Kwa upande mwengine serikali hiyo haiwezi kuwakana moja kwa moja kwani kufanya hivyo kutaleta msuguano mkubwa wa waungaji mkono wake ambao ni wengi nchini Misri.
Hiyo ni sababu mojawapo ambayo serikali ya Misri imeweka nia ya kuzuia Israel kudhibiti mpaka wa Rafaha kama ambavyo wametangaza kwani kufanya hivyo kutapelekea machafuko makubwa ndani ya Misri.