Namkumbuka Baba na Rafiki Yangu Ahmed Rashaad Ali

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
Mwaka wa 1952 Ahmed Rashaad Ali alimwandikia Gamal Abdel Nasser Rais wa Misri barua yenye kurasa sita kuhusu mateso yanayowakabili wananchi wa Zanzibar chini ya usultani.

Rashaad alimuomba Nasser ampe kazi ya utangazaji katika Sauti ya Cairo ili aueleze umma wa dunia madhila ya ukoloni wa Waingereza.

Nasser alikuwa ameongoza mapinduzi yaliyompindua Mfalme Farouk.

Barua hii ya Rashaad ilimuathiri sana Nasser.

Nasser aliwasiliana na Rashad kupitia Ubalozi wa Misri Bombay.

Rashaad alifanya hivi kwa kutambua kuwa mipango yake ya kuondoka Zanzibar lazima ifanywe nje au sivyo haitafainikwa kwa kuwa serikali ilikuwa ikimtazama na angeweza kukamatwa wakati wowote.

Nasser aliafiki na mipango yote iliyopendekezwa na Nasser.

Rashaad alisafiri hadi Bombay na akawasili Bombay mwezi November 1952 na aliondoka Bombay kuelekea Cairo Februari 1953.

Hivi ndivyo Ahmed Rashaad Ali alivyopata kazi Radio ya Cairo (Sauti ya Cairo).

Kituo hiki kikiwa kimeanzishwa na Gamal Abdel Nasser mara tu baada ya mapinduzi ya Misri ya mwaka 1952 yaliyofanywa na kikundi cha wanamapinduzi waliojiita ‘’Free Officers.’’

Madhumuni ya kituo hiki ilikuwa kueneza propaganda kwa niaba ya vyama vya kupigania uhuru vya Afrika.

Baadhi ya wanamapinduzi waliopata kutangaza katika kituo hicho ni Sam Nujoma, ambae baadae alikuja kuwa rais wa Namibia, na Reuben Kamanga, ambae nae alikuja kuwa makamo wa rais wa Zambia.

Kanyama Chiume wa Nyasaland alikuwa vilevile akipewa nafasi kutangaza kwa watu wake kila alipokuwa Cairo.

Kituo hiki kilikuwa Zamalek Street katikati ya jiji la Cairo na serikali ya Misri ilitoa ofisi na huduma za makatibu mukhtasi na wafasiri wa lugha mbalimbali kwa vyama vyote vya wapigania uhuru.

Sauti ya Cairo ilikuchukua msimamo mkali katika matangazo yake na ikaja kupendwa sana Afrika ya Mashariki.

Kulitaja jina la Rashaad ikawa sawa na kutaja Sauti ya Cairo.

Halikadhalika mbali na Sauti ya Cairo, Rashaad alianzisha matangazo mengine kupitia radio ya msituni ikiitwa, ‘’Radio Free Africa’’ (Radio ya Afrika Huru).

Radio hii vilevile ilikuwa ikifadhiliwa na Nasser. Katika Radio ya Afrika Huru kulikuwa hakuna ustaarabu wala staha.

Wakoloni walikuwa wakitukanwa dhahri shahri bila ya kificho.

Katika Sauti ya Cairo Rashaad alipiga muziki wa kawaida wa kuburudisha. Lakini katika Radio ya Afrika Huru alikuwa akipiga nyimbo za kijeshi na za kimapinduzi kutoka Afrika ya Mashariki.

Nyimbo hizi ndizo zilizoongeza utamu katika matangazo ya Rashaad.

Rashad alifanikiwa sana katika matangazo yake kiasi kwamba serikali ya Uingereza ililalamika kwa serikali ya Misri kuwa matangazo hayo yakomeshwe mara moja ama sivyo Uingereza itakata misaada kwa Misri.

Uingereza ilimwita Rashaad ‘’Yule Mkomunisti kutoka Zanzibar.’’

Nasser alipuuza vitisho hivyo na akamuamuru Mohamed Faik, mtu wa karibu sana kwa Nasser na ndiye aliyekuwa waziri wake wa mambo ya Afrika kumuambia Rashaad aendelee na kazi yake nzuri.

Ombi la Nasser kwa Rashaad lilikuwa Malkia pekee yake ndiye astahiwe, waliobaki wote wapigwe vigongo.

Wasikilizaji wa Rashaad wakisikia akisema ‘’Majibwa meupe,’’ hawakupata tabu kumjua hao mbwa walikuwa nani.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1989).

Huu ndiyo uhusiano wa Gamal Abdel Nasser na Afrika ikiwamo Afrika ya Mashariki kuwa alisaidia ukombozi wa nchi za Kiafrika zilizokuwa chini ya ukoloni.

1707112509202.jpeg

Ahmed Rashaad Ali
1707112600227.png

Kushoto, Ahmed Rashaad Ali, Dr. Harith Ghassany na Mwandishi amemshika mjukuu wa Mzee Rashaad Badru Said Badru​
 
View attachment 2894730
Ahmed Rashaad Ali
View attachment 2894734
Kushoto, Ahmed Rashaad Ali, Dr. Harith Ghassany na Mwandishi amemshika mjukuu wa Mzee Rashaad Badru Said Badru​
Maudhui ni Abdul Sykes
 
Maudhui ni Abdul Sykes
Nar...
Hakika...

Si kila siku mtafiti anakutana na mtu mfano wa Abdul Sykes.

Ahmed Rashaad amenipa mengi wakiwa watoto Dar es Salaam 1939 kisha wakiwa Bombay, Kalieni Camp baada ya WWII 1945 Rashaad akiwa mwanafunzi India na Abdul Sykes akiwa katika KAR Burma Infantry askari Waafrika wanasubiri kurudishwa makwao baada ya vita.

Hapa Kalieni Camp ndiko lilipotoka jina la chama cha TANU.

Ahmed Rashaad ananieleza 1950 yuko na Abdul Sykes Nairobi pamoja na Jomo Kenyatta, Peter Mbiu Koinange, Kun'gu Karumba, Bildad Kaggia na Paul Ngei katika mkutano wa siri.

Unawajua hawa historia zao katika kupigania uhuru wa Kenya.

Bildad Kaggia kaandika kitabu, ''Roots of Freedom.''

Kuna mengi ndani ya kitabu hiki kuhusu Mau Mau.

Mzee Rashaad ananieleza aliyoelezwa na Abdul Sykes kuhusu Julius Nyerere wakiwa Cairo 1963.

Historia nzito sana.

Nasikitika sikupata ruksa ya kusoma shajara zake.

Vipi ndugu yangu.
Historia hii inakukera?

Haiongezi maarifa katika historia ya uhuru wa Tanganyika?

Kwingi huulizwa, "Mohamed kweli ukiwajua watu hawa toka utotoni?"

1707144138333.png

Kushoto Abdul Sykes, Cairo 1963

Similar Discussions

Back
Top Bottom