Lalo Salamanca
JF-Expert Member
- Dec 9, 2012
- 1,527
- 1,098
Kuna mshkaji niliwahi fanya nae kazi sehem flani kabla sijaacha pale na kuhamia kwingine, sasa akawa ananisumbua na mameseji mara kuna opportunity sijui e-Commerce nataka tufanye itatutoa kimaisha, ukimuuliza ni nini hasa mnafanya? Hasemi ye anataka tuonane anieleze vizuri hiyo fursa, ukiangalia Status zake za Whatsapp asubuhi mpaka jioni ni Motivational Quotes tu za Financial freedom na zinazodharau waajiriwa, Mara mapicha ya Safari n.k, siku naonana nae nikamkuta na jamaa flani sura yake anaonekana hana furaha halafu kachoka, wote wamenyonga tai nikajua tu hawa ndio yaleyale ya network marketing ila nikajifanya sijui kitu, yule jamaa mwingine ndio kaanza kunipa somo na likitabu lao issue za QNet, nimewasikiliza bila kuwa-interupt for 2hrs, walivomaliza wakasema tutapanga session ya pili nikasema poa, nilivoondoka kesho yake nikamwambia yule mshkaji siwezi kufanya hiyo biashara yenu wala usihangaike kunitafuta tena, nimeblock na namba zake nadhani na urafiki mdogo uliokuepo umeisha rasmi. Nafikiri aliona mimi ni easy target.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app