Salaam,
Mimi ni mjasiriamali mdogo mdogo wa vitenge hasa kutoka Tunduma, katika kuhangaika wa kunifungia mzigo nishajikusanya nikaanza kufanya utafiti nikakutana na sister mmoja anasema yupo Kigoma anaweza kunifungia mzigo Kwa uaminifu mkubwa ila yeye hayuko Tunduma.
Basi, nikaanza mawasiliano nae nikampatia aina ya vitenge ninavyohitaji akasema angeliweza kunifungia mzigo ma kesho autume nilipo.
Nikamtumia Hela, tangu nimemtumia hajaniblock nikimpigia hapokei anafanya kutuma meseji tu, whassap anasoma meseji zangu hajibu, nikajaribisha kumtumia ujumbe na kujifanya Niko nahitaji vitenge kama mteja tofauti nilishangaa ananiambia kwanini namtafuta kwenye Simu nyingine?
Je, inamaana hauzi bidhaa hizo?! Kwa maana kama angelikuwa anauza basi angeligundua ni mteja mpya. Kuna siku alinipigia Simu kuwa mzigo umeshatumwa ila Kuna tatizo nikamuuliza tatizo Gani?
Akadai mzigo huo umefungiwa na mzigo wa mteja wake ambaye hajalipia Kwaiyo nisubilie ampate ili tuchukue mzigo baada ya siku mbili nikamwambia anitumie namba ya mzigo wangu utakaokuwa umeongezeka nitalipia basi alikataa kunitumia akadai nimtumie Hela kwanza Kisha ndio anitumie namba ya mzigo!
Nikakataa, kesho yake ananiambia mzigo utarudishwa Kigoma ili atoe mzigo usiokuwa wangu Kisha autume tena!! Jamani ni wiki mbili Sasa natuma ujumbe kuuliza mzigo wangu ananijibu Kwa ukali kuwa nitulie atanitumia Hadi Sasa hajibu chochote!
Nilimtumia 262,000 naomba msaada kwa namna Gani naweza kupata haki yangu?
Anadai yeye sio tapeli lakini mpaka Sasa hivi nahisi hakuna cha vitenge ila nahitaji nirudishie pesa yangu jamani😭😭😭😭.
Niende wapi nipate msaada ili akamatwe na arudishe Hela yangu maana vielelezo vyote vipo.
Msaada please!