Mkuu wa Wilaya aliyecharaza Walimu huyu Hapa

Yaani huyu mkuu wa wilaya anafaa sana kuwa waziri mkuu ili awanyoshe wazembe wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Jamaa anafaa sana ingawa aekumbwa na kufukuzwa kazi. Shule za serikali ka sasa zinadorora kwa sababu walimu wako bize na shughuli zao binafsi huku watoto (wanafunzi) wakiambulia kucheza tu na mwisho wa siku wanafeli. Wakati mwingine yahitaji maamuzi mazito kama haya ili kunyoosha mambo
 
Ukweli ni kwamba uamuzi wa mkuu wa nchi kumfukuza kazi Mnali ulikuwa wa jazba, maana mnali aliona ni bora kuwaadhibu kwa viboko kuliko kuwafukuza kazi kwani wangepoteza maslai yao yote na sababu alikuwa nayo maana inaonekana hawa walimu walikuwa hawhudhuri madara sani kwa muda mrefu na uthibitisho anao. Rais angeweza kumuadhibu kwa kumpa adhabu nyingine lakini si kumfukuza kazi.
 
Serikali imemtoa kafara Mnali ili ijiaminishe kwetu kuwa iko makini. Tumeshagundua janja yao.. wangemwajibisha kwanza Pinda kwani kauli yake ilikuwa ni tata na ya gharama kubwa kwa roho za watu kuliko viboko kwa wale walimu wazembe.

Mambo serious ya msingi Serikali inayafumbia macho... Kagoda mwizi wa EPA na Lowassa fisadi wa Richmond walipaswa kuwajibishwa na kuburuzwa mahakamani. Lakini wapi, urafiki huu utaisha lini?
 
Ushauri wangu wa bure ni huu; kule kwao Newala,agombee Ubunge mwakani basi.
 
Back
Top Bottom