Mkutano wa CHADEMA viwanja vya NMC Arusha

Jk ameonyesha udhaifu mkubwa sana kumteua mtu asubuh kuwa mb jion waziri jamani hata kama ni mtu mwenye haraka kiasi gani angesubir aapishwe kwanza
 
Wanafiki wanaumbuka kweupeeeee!

Wananchi amkeni, CDM sio chama.

Asante bwana Jackson

CDM inawatumia mbumbumbu,wachumia matumbo na wasiotambua malengo yaliyofichwa ya hiki chama.Hakuna ubishi hiki chama ni cha kikabila! Chacha wangwe alipotaka kugombea uenyekiti,mizengwe kibao iliibuliwa,Zitto naye anang'ang'ana hatafanikiwa kamwe! Uenyekiti ni wa wenye chama tu,wachaga.Bob makan aliukwaa uenyekiti baada ya mtei coz ameoa na kujenga uchagani na alikuwa hana maamuzi(rubber stamp).Inatisha sana.
 
Jk haelewi nini maana ya 'urais' amekuwa kama msukule vile...
 
Mkutana umemalizika salama hakuna hata sisimizi alie umizwa na hakukuwepo na Polisi...

mkuu nashukurusana kwa coverage nzuri Mungu akubariki, tunasubiri hizo movement zienee huko lindi, mtwara.. na kikwengineko walikoahidi MPAKA 2015 CCM KWISHAAAA- SOMO WATAKUWA WAMELIPATA. Weekend Njema

 
Akihutubia utitiri wa wana CDM wa Arushwa Mh. Mbowe alieleza maeneo yafuatayo ambayo KIKWETE amevunja katiba Ya Tanzania.
1. Huwezi kumteua mtu awe mbunge halafu kabla hajakabidhiwa na kuapa kwa kanuni za bunge unamteua kuwa waziri kama alivyofanya jana. Wabunge aliowateua hata kabla hawajaidhinishwa na bunge yeye akawapa madaraka ya kuwa mawaziri na mbaya zaidi kumteua mtu asubuhi mbunge na jioni anakuwa waziri. Mfano mzuri wa mgongano huo ni wakati mbunge wa viti maalum wa chadema alipopeleka maswali bungeni (Akiwa ni mteule baada ya kuchukua nafasi ya Regia Mtema R.I.P) swali lake liliondolewa kwa sababu tu wabunge wa CCM walikataa kwa sababu hajaapishwa. Je? kanuni hiyo inafanya kazi kwa sababu ni mbunge wa chadema tu? CCM na Kikwete wako juu ya sheria?
2. Kuna wizara za Muungano ambazo ni Mambo ya ndani, jeshi na kujenga taifa, fedha, mambo ya nje lakini nyingine ni za Tanzania bara tu! mfano elimu ni bara tu maana zanzibar wana ya kwao au afya ni ya bara tu! Lakini leo Huseein Mwinyi ambaye ni mzanzibar anapewa wizara ya afya ya Tanzania bara! JE? Zanzibar wamewahi kufanya makosa kama hayo? au ni sisi tunajikomba kwao? kwani katiba si inasema wazi?

Naomba kuwasilisha

Looh! Mwenyekiti wa chama anahoji huo utaratibu ambao upo TZ tokea enzi za Nyerere mpaka sasa. Ina maana haelewi au ni siasa tu?

Unaweza usiupende utaratibu fulani lakini kusema amevunja katiba ni tuhuma nzito sana hasa ikitolewa na kiongozi wa upinzani bungeni. Je kweli Mbowe amekaa na wanasheria wake kabla ya kuongea hili?
 
JK anacheza rafu nyingi either kwa makusudi au kwa ufahamu wake mdogo na washauri wake...inasemekena alitaka kumpa uwaziri Mbatia...kajisau kuwa katiba hairuhusu serikali mseto
Hivi nazi ndani huwa kuna nini?
 
Jamii nzima inapaswa kufumbua macho na kutoka ktk usingizi mzito ulio tugubika! Inatupasa tupingane na usingizi huo uliojaa ufisadi na kufungua ukurasa mpya wa mapinduzi kwa vijana,kwani wimbo wa wazee wetu walioimba kuwa vijana taifa lakesho,ndio sisi kwani siku imefika yakuwaonesha kuwa jana imepita na sasa ni leo! Kwamtu mwenye upeo ameishaona kwani dalili ya mvua ni mawingu wameanza na magamba,wataamia kwenye kuvua ngozi! Ilikuwasitili tunawakaribisha kwa gwanda! Peoples...................!
 
Looh! Mwenyekiti wa chama anahoji huo utaratibu ambao upo TZ tokea enzi za Nyerere mpaka sasa. Ina maana haelewi au ni siasa tu?

Unaweza usiupende utaratibu fulani lakini kusema amevunja katiba ni tuhuma nzito sana hasa ikitolewa na kiongozi wa upinzani bungeni. Je kweli Mbowe amekaa na wanasheria wake kabla ya kuongea hili?
Ama kweli JF imevamiwa..maneno aliyoyasema Mbowe huhitaji elimuhata lasaba kugundua hilo...kwa hiyo kama kuna makosa yalifanyika zamani basi yaendelee, je unaweza kutoa mfano ni waziri gani kutoka Zanzibar ambae alisha wahi kupewa wizara inayo husu Tanganyika...
 
Looh! Mwenyekiti wa chama anahoji huo utaratibu ambao upo TZ tokea enzi za Nyerere mpaka sasa. Ina maana haelewi au ni siasa tu?

Unaweza usiupende utaratibu fulani lakini kusema amevunja katiba ni tuhuma nzito sana hasa ikitolewa na kiongozi wa upinzani bungeni. Je kweli Mbowe amekaa na wanasheria wake kabla ya kuongea hili?
Mkuu ebu rudia kusoma hicho kifungu cha kwanza,kama sheria hiyo ilitumika kumzuia mbunge wa CDM bungeni kwa sababu hajaapishwa inakwaje ifanye kazi upande wa CCM?think twine bhana
 
Ama kweli JF imevamiwa..maneno aliyoyasema Mbowe huhitaji elimuhata lasaba kugundua hilo...kwa hiyo kama kuna makosa yalifanyika zamani basi yaendelee, je unaweza kutoa mfano ni waziri gani kutoka Zanzibar ambae alisha wahi kupewa wizara inayo husu Tanganyika...

Ali Hassan Mwinyi - Wizara ya Afya Tanzania 1972 mpaka 1975
Ali Hassan Mwinyi - Wizara ya Mali asili na utalii Tanzania 1982 mpaka 1983.

Ahmed Hassan Diria - Wizara ya habari na Utangazaji Tanzania - 1989 mpaka 1990.

Unataka niendelee!!!!
 
Jk haelewi nini maana ya 'urais' amekuwa kama msukule vile...
Atasema alishauliwa na CC ya CCM.....mimi nilishangaa wakati analitangaza baraza la mawaziri alikuwa anaongea huku akitetemeka kumbe alikuwa anajua anatenda dhambi kubwa kwa watanganyika....
 
Mzee Mwanakijiji ukisikiliza kauli nzima ya dogo janja haikuwa na madhara,ila watu wanasimamia kwenye kipengele kidogo ambacho wao ndo walikuwa wanaitaka ili kuonyesha weakness ya CDM,mbona Mbowe kaelezea tu vizuri pale kuwa hiyo siyo kauli ya chama

Hapa kidogoo nimekuwa shocked.......picha ninayopata kumbe ni kweli mwanachama maarufu wa CDM alitamka kauli hiyo mbele ya kadamnasi, hata hivyo mwenyekiti wa chama akakanusha na kutamka wazi kwamba hiyo si kauli ya CDM bali ni ya Mwanachama wake!!

Iwavyo vyovyote, ni pale atakapotokea mwenyekiti mwendawazimu tu ndipo angeweza kukiri kwamba kauli hiyo ni ya chama!! Hivyo basi, sishangai kusikia Mbowe akikanusha!

Picha nyingine ninayopata hapa ni kwamba, hiyo inaweza isiwe kauli ya chama lakini haimaanishi kwamba sio agenda ya chama! Kauli na agenda ni vitu viwili tofauti. Panaweza kuwa na agenda lakini kauli rasmi kuhusu agenda husika ikawa haijatolewa....je, Dogo Janja aliropoka kabla ya wakati muafaka?!

Kuna hii picha nyingine! Inawezekana kabisa kwamba hiyo isiwe kauli wala agenda ya chama....lakini kumbe kuna "wanachama maarufu" wenye agenda ama mawazo kama hayo kwenye mitazamo yao...hili si jambo jema hata kidogo!!

Wengi wanaituhumu CDM na Ukaskazini.....!!! Sina hakika katika hili ingawaje jambo lililo wazi ni kwamba matendo ya CDM yana-reflect tuhuma zinazotolewa dhidi yake!! Kuna harakati za kufa mtu za kuijenga CDM kanda ya Kaskazini lakini harakati hizo hazionekani kwenye maeneo mengine ya nchi hususani pwani na kusini!! Baada ya uchaguzi mkuu 2010, CDM walitangaza kufanya uamsho nchi nzima....inakaribia miaka miwili hivi sasa lakini maeneo wanayozungukia ni yaleyale....!!! Wenyewe wanaita hizo ni strategic areas huku wakitarajia kuchukua nchi kupitia wapiga kura wa ukanda mmoja tu!!!

Mimi ni mtu wa Kusini...CCM imetusaliti na CDM siiamini japo kwa punje ya uwele!! Huwa najiuliza, ikiwa CDM inatutupa mkono wakati wa kuitafuta keki ya taifa, je watatukumbuka wakati imeshapatikana!!!? napata shaka hasa nikikumbuka jinsi ambavyo Dr. Slaa alienda kusini kuomba kura! In few hourz, akapiga kampeni kwenye mikoa miwili....lakini bado wanatushawishi kwamba waliibiwa kura! Kama kuna mtu ninayemuona mjinga kuishabikia CDM basi ni mtu wa kusini unless kama ana nasaba na kaskazini!! Mtanzania mwingine yeyote labda anaweza kuishabikia CDM lakini sio mtu wa kusini!

Kutokana na mwenendo huu wa CDM ndio maana naiangalia kauli ya Dogo Janja kwa jicho la pili...!!
 
Mkuu ebu rudia kusoma hicho kifungu cha kwanza,kama sheria hiyo ilitumika kumzuia mbunge wa CDM bungeni kwa sababu hajaapishwa inakwaje ifanye kazi upande wa CCM?think twine bhana

Mkuu Excellent,
Huruhusiwi kushiriki shughuli za bunge kule bungeni mpaka uwe umeapshwa na spika. Hivyo kanuni ilikuwa sawa kumzuia huyo mama kuuliza swali bungeni kabla ya kuapishwa.

Lakini huzuiwi kufanya shughuli zingine zozote za kibunge kwa mfano jimboni kwako unaweza kuendesha mikutano kama mbunge hata kama hujaapishwa.

Hao mawaziri hawawezi kwenda bungeni kujibu maswali au kuwasilisha budget mpaka waapishwe kwanza lakini kama watendaji wa serikali wanaruhusiwa kufanya shughuli zao za uwaziri kama kawaida.
 
Msaada pliz hivi Rais akivunja katiba, adhabu yake nini?...Mwananchi wa kawaida akivunja katiba hiyo inakuwaje wapendwa?...Ngoja kidogo niongee nimeshapandwa na hasira hapa, mikutano ya halali ya CDM kwanini ipigwe mabomu, au ipingwe? Siku ile baada ya Lema kuvuliwa ubunge polisi nasikia hawakukanyaga pale "CHADEMA SQUARE", je kulikuwa na uvunjifu wowote wa amani?


Kwa kufanya hivyo MTUKUFU ALIYETUKUKA KATIKA KITI CHA ENZI PALE WHITEHOUSE yetu atatujibu nini? Ok mimi sikuwa kwenye mkutano wa leo Arusha, lakini niulize RPC alileta vijana wake? CDM walifanya fujo?

Haya sasa MSAHAFU WA UMMA unaowangoza wana wa nchi umedhalilishwa,umekanyagwa, umesiginwa,...Kwani "Mwenyekiti ye ndio pekee msomi katika nchi hii, au katiba anayo yeye peke yake?

Sihami nchi hata iweje na ninamuomba "Muumba aniweke hai hadi nitakapouona UKOMBOZI wa kweli.
Inauma sana kuona WENYE NCHI WAKIFEDHEHESHWA. Linaweza onekana ni jambo dogo hili lakini madhara yake yakawa makubwa.

Na hao wabunge CCM itawajutia kwa sababu wapo CCM kimaslahi ila na wao wana uchungu kwani wanajua vile KEKI ya Taifa inavyoliwa.
 
Mi naunga mkono hoja ya mh sana NASSARI kama vp tujitenge na dar es saalam plus pwan na uko ukwereni na kwingne kokote wanapowaza maendeleo yataletwa na ccm baada ya miaka 50 sasa
 
Masikini Tanganyika yangu Chadema wanataka kuigawa vipande.
 
Back
Top Bottom