Dkt. Nchemba aongoza Baraza la Mawaziri wa Fedha na Uchumi Afrika Mashariki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,925
12,208
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) ameongoza Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) na mkutano wa Mashauriano ya Kibajeti wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudani Kusini, Mhandisi Awow Daniel Chuang Deng, ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Baraza hilo, unaofanyika tarehe 17 Mei 2024, jijini Arusha, nchini Tanzania.

Mawaziri hao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo Wasilisho la Nchi Wanachama kuhusu Miongozo ya Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 na Kaulimbiu za bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.

Viongozi wengine walioshiriki Mkutano huo kwa upande wa Tanzania, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, Maafisa na wataalam wengine kutoka Serikalini.
 
Aache kuvaa tu matai awaulize Mawaziri wenzie wanaojielewa wamefanyaje fanyaje pesa yao ikapanda thamani dhidi ya pesa yetu?!.
Kama ni vita ya Ukrain na Russia mbona wao hawajaathirika, pia mbona dola nchi zao hakuna uhaba kama hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom