Mke wangu ananiumiza kichwa

That's me
4657f94f34d2a0e66c450429f3668554.jpg
 
Pole ya kawaida hayo, ongea nae delete hiyo account Facebook, jipe muda maumivu yapungue msamehe maisha yaendelee.....
Kumbe it is that easy?
MY dada cheating a man is different from cheating a woman... ***** nasomesha halafu faida ndo hiyo!!
 
Evelyn kinachoniuma ni kwamba before sijakutana nae nilikuwa Malaya mbwa ila nlipokutana nae nikajua roho mtakatifu kanigusa na nikabadilika kabisa, nikiwaza hapa atakuwa ameshanisaliti mara ngapi mpaka hivi leo? Kazi yangu yenyewe ni mikoani mara kwa mara naweza kaa mkoani hadi miezi mitatu kama project ni ndefu kiaina...hapo Kati atakuwa ameshakung'utwa vya kutosha, kama Facebook anajirahisi kiasi hichi vipi vijana wa hapa mtaani? Naweza kuwa nasalimiana na vijana wenzangu mtaani kumbe wananicheka wanavyonimegea mke wangu, sijui naanzia wapi kuongea nae, Nina hasira za karibu na sijawahi mpiga hata siku moja, nahisi Naweza fanya kitu cha ajabu....kichwa kinaniuma vibaya hapa
Formlar ipo hiv,malaya atamuoa malaya mwenzake
 
Mkuu kwenye mtoto sina Shaka mtoto kafanana na mama yangu kila kitu mpaka bimkubwa akamkabidhi jina lake, maana wakubwa zangu walitangulia kuzaa hakuna aliyekabidhi mwanae jina la mama ila alipozaliwa wangu mama akamtazama Akasema iwe isiwe lazima aitwe jina lake na wamefanana kweli...hapo sina Shaka ila kwenye kukung'utwa na watu wengine hapo ndio roho inaniuma maana sina ushahidi wa moja kwa moja ila message zimeniumiza vibaya

Kimbiaaaa
 
Sasa ulimfungulia facebook ya nini. Kama alikuwa haijui facebook ungemwambia asijiunge huko kwani kuna mashetani. Pole.
 
mimi na hii roho yangu Mungu aninusuru maana nikigundua ivo on the spot ataenda kwao,,,,ila ilo kabila m nawafaham vzr ni ikina mama huruma
 
Pole ndugu, ila nliwahi shauriwa kuwa kama huna kifua kaa mbali na simu ya mwenza wako, mi nakuomba fanya yafuatayo, toka naye out siku moja jua wewe na yeye, ikiwezekana hata chukua weekend moja hotelini, wakati mnainjoi embu jaribu kupeleleza kama kuna kitu ana miss kwako, nini anatamani uongeze katika mapenzi yenu, kama vipo hivyo vitu then in a polite way jaribu kumuuliza kama ndo vinafanya anachat ujinga fb, kama havipo jaribu kumuuliza politely why anafanya anayoyafanya?

Ongea naye tatua in a polite way mpe another chance, niliwahi salitiwa na mpenzi wangu niliumwa hadi kulazwa, alikuja akitubu na msamaha analia hadi alizimia ila sikuwa tayari, baadae nilijiuliza hivi ningekuwa ni mimi nimefanya hilo kosa si ningetaka kusamehewa? I believe ingehappen kwako ungetaka na wewe kusamehewa na mwenzako akupe fursa ya kujieleza why ulianguka, kama yeye amechangia au lah, na upewe a chance to make things fresh.

Victor j (MC mtumishi)
Inspirational and motivational speaker/master of ceremony
this is the first time naona comment yako, nimeipenda na ni inspirationalkweli...naomba uwe unapitia nyuzi hapa utupe insiration....salute
 
Mkuu mpaka Sasa nimeshaondoka nyumbani sijamuambia kitu ingawa ananijua vyema ameona imebadilika ghafla, kama nilivyosema najijua Nina hasira za karibu sana hivyo nahisi ningeuliza akanijibu ndivyo sivyo ningesababisha mengine. Nilimpigia Dada yake mkubwa Jana tumepanga kuonana leo, nimueleze ya mdogo wake kisha Dada yake nitamsikiliza ana maoni gani sitaki yafike kwa wazazi maana itakuwa aibu kwake na kwangu pia mambo kama haya
una busara sana...ilabora uanze na dada yakea ila kuwa na evidence....maana ukizingu atafuta af atasema unamsingizia naitaisha kavukavu...umekuwa mstaarabu na mvumilivu...onesha evidence afmay be dada atamuuliza yeye kupitia hiy anaweza kuja omba msamaha haswaaa....atajutia .hapo utaona tu...ila we una hasira bora utulie usije mtoa meno....wanaume kama wew tup wachache
 
TAECOLTD. Wengi wanaokushauri humu hawakuambii/hawakushauri ukweli.

Nakuhakikishia kitu kimoja ambacho wanaume wengi hawafanyi siku hizi". 'Kumpeleka mwanamke shule' kwa asilimia 90 mpaka sasa umebugi
Kwani mlipokutana akiwa std 7 kulikuwa na tatizo gani? mpaka ww uchukue majukumu ya wazazi wake au ndio uoga wa maisha¡
Hapo anasoma anajiachia hivyo ' akianza kuchukua mshahara lazima utajinyonga,

Ushauri
Andaa supa sub kabla hujachelewa.

Ni fundisho kwa wengine wanaofanya mchezo kama wa kwako, hii theory ya kusema tutasaidiana maisha imefeli kwenye ndoa nyingi.
 
Duh! Pole
Mke na Facebook wapi na wapi, hata magroup ya whatsapp pia kagua,
Dawa hapo n kuwa kamanda mwanzo mwisho, hucheki na kima, mpaka anyooke
 
Kwanza nikupe pole sbb ht me ilishanikuta naelewa length of pain u undergoing!
Kisanga chako na changu havijatofautiana sana.
Ila kikubwa cha kukushauri usihukumu kwa hisia kaa ongea nae muonyeshe na huo ushahidi wala usipaniki na kuchukua hatua hatarishi.au anza kumchunguza polepole upate na physical evidence ndo itakuwa vizuri ujue pa kuanzia.
narudia tena kukupa pole maana wanawake wanadanganyika kiwepesi sana siku hizi kwa kujiaminisha lbd upande wanakoenda watapata comfort zone matokeo yake anapewa maradhi aje kukuambukiza na ww
 
Pole sana na inauma kweli. Waswahili wanasema hasira hasara. Katika jambo hili tulia kwanza na ujue wanawake ni viumbe dhaifu, Mkisha kaa na dada yake, mwambie dada yake akamweleze uozo aliokuwa anafanya na hapo utaona kama kweli ameona uovu wake maana kama anajielewa atatubu ki ukweli na utampa second chance. Saa nyingine wanawake wanaweza kufanya hivyo baada ya kupata mwingine na atafanya makusudi hili ndoa ivunjike aende kwa mwingine. Chunguza pia kama kuna jinsi yoyote anafadhiliwa na watu wa nje. Mwisho jipe moyo mkuu ndiyo dunia hii inayoitwa tambara mbovu.
 
Katika kitu ambacho hua sikubaliani na jamii ya leo ni kutokuchunguza simu ya mke/mwenza
yalishanitokea figisu zote nilikua nazipata kupitia simu yake
Nazifanyia uchunguzi nikimueleza anakataa nampa muda baadae namuibukia na data zote anakiri alifanya unamuonya anatulia baada ya muda anarudia tena nikaamua kuachana nae
ninachokushauri ndugu kama bado mkeo unampenda jifanye kama hujaathirika endelea kuchunguza simu yake ili uupate ushahidi wa kutosha baadae kaa nae kitako mueleze kwamba unajua yote anayoyafanya na umkanye aachane nayo
endelea kumchunguza hata baada ya miezi sita au mwaka akiachana nayo utaendelea naye akiendelea kuyafanya ni tabia yake huna namna ya kumzuia asifanye na hapo ndipo utakapo amua kumuachia maisha yake
 
Naona imekuwa wiki ya wake hii, pole sana.

Rudia tu umalaya wako japo haiondoi machungu lakini inakufariji.

Ni ungese kuwa na mwanamke mmoja kisa yeye tu, bora iwe ni kwa utashi wako binafsi na mazingira
 
Nilichojifunza recently ni kwamba wanawake walioshiba ndo hufanya cheating zaidi compared na wenye njaa, kushiba ni kubaya sana!
 
Back
Top Bottom