Amani imetoweka moyoni mwangu, Co Worker wa kiume na mke wangu wapo karibu sana, nichukue uamuzi gani?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Co-worker ni mtu mnaefanya nae kazi

Ni kwamba nina informer/ mpelelezi ambae ni rafiki yangu wanafanya kazi sehemu moja na wife.

Recently kuna jamaa kaletwa hapo kutoka mkoa mwengine na wamekuwa close sana na mke wangu, details nilizopata ni walisoma chuo kimoja mke wangu akiwa mwaka wa kwanza na huyo mwengine akiwa wa tatu.

tukiwa nyumbani sijawai kuona yupo bizi anachat na huyo jamaa ama simu zinaita anazokata ama kuongelea nje, nadhani bila mpelelezi wangu nisingejua chochote.

Huko kazini wamekuwa team hupenda kuongozana wao wawili kufatilia ishu za benki, manunuzi, kufatilia wateja wa shirikika, kwenda lunch, n.k. huwa wanatumia gari ya jamaa. hili niliwahi kulihakikisha mwenyewe mara mbili.

Kuna siku nilichukua simu yake kimya kimya nikasechi namba ya huyo jamaa niliyopewa na informer, Huwezi amini mara ya mwisho kwenye meseji za kawaida na whatsaoo lakini nilitahamaki chats zao ni chache sana na chats za mwisho zina wiki na ni mambo ya kikazi tu, nikasechi sechi jina la huyo cowrker na message zingine hata alizosevu majina ya ndugu ila sikuambulia kitu, Napata mashaka zaidi maana haiwezekani mtu uwe nae karibu msiwasiliane, Nahisi mke wangu ana simu ya pili ama kanizidi ujanja wa teknolojia kuficha mawasiliano maana anajua naijua password yake,

Najua fika kwa jinsi tulivyo wanaume hapo kuna mambo ya ziada yanaendelea.

Niwe mkimya niendelee kukusanya data nipate ushahidi huku nachohisi kikiendelea kikishamiri ? Nimwambie mke wangu kwamba akae mbali na huyo co worker ? Nimwachishe kazi ? Niende kum confront huyo mwenzake ? Nikubaliane na hali nikaushe ? Niachane na mke ? Niwashirikishe ndugu wa mke wanisaidie,,,,,,,,,,,,,,

NICHUKUE UAMUZI GANI WENYE HEKIMA NA BUSARA?
 
Suluhisho ni kuachana na mwanamke kama una ushahidi wa wazi wa usaliti.

Mwanaume ama huyo co worker huna sababu ya kugombana nae kwa sababu hajambaka mke wako, amemtongoza na mkeo akakubali.

Ukikorofishana na huyo, atakuja co worker mwingine atamtafuna.

Deal with the source.
 
Una uhakika gani huyo "informer" anakuletea taarifa kwa nia njema mpaka utilie maanani taarifa yake??

Mke wako amekupa sababu gani ya kutomuamini mpaka uombe ushauri kuhusu uamuzi unaoweza/paswa kuchukua?? Tukikuambia uachane nae utamuacha??🙄

Huwezi kufanya maamuzi yoyote bila kuwa na sababu ya msingi. Kama una wasiwasi ongea na mkeo, ama mfuatilie (huu ushauri sijatoa mimi 😶‍🌫️, ili uone kama kuna chakutilia maanani au la!
 
Back
Top Bottom