Mke wangu kaniambia wana ndoa sio lazima waishi pamoja, kahamia Dar lakini sijui anaishi wapi!

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,823
Alipomaliza chuo, nilipomuambia mambo ya kumuoa, akaniambia hapana, subiri mpaka nipate kazi, kuna mambo namalizia, nikajitahidi kuhangaika, kuna mshikaji wangu akamuunganishia, akapata kazi benki. Mshahara laki 6, sijakaa miezi miwili, ananiambia kuwa ananunua gari, nikawaza kwamba maisha gani ananunua gari, akanambia nimechukua mkopo kazini.

Mimi nikatulia, akanunua hiyo gari, nakumbuka kipindi kile IST alinunua milioni 14, nikasema poa, haina shida. Naongelea mambo ya ndoa, ananiambia mimi sina shida kuhusu kunioa, lakini siwezi kuishi huko, nataka kuishi Dar au Morogoro. Nikamuambia mimi niko Dodoma, unafanya kazi Dodoma, kwanini utake kuhama?

Akanambia, ndiyo nimeamua, kama unataka kunioa basi ni kati ya mikoa hiyo. Nikasema isiwe shida, tutahamia huko, basi tukafunga ndoa, mara kanambia anaacha kazi, anahamia Dar kama alivyonambia kwani kapata kazi nyingine huko, nikamuambia mimi uhamisho kuja Dar mgumu, ananiambia kwani nani alikuambia nataka uhamie na mimi.

Mimi sitaki kuishi na wewe, baki Dodoma, mimi nataka kuishi Dar, siwezi kuishi na mwanaume 24/7. Tukagombana, nampigia mama yake, ananiambia kama mwanangu hataki kuishi na wewe kwanini unanilazimisha. Sijakaa sawa, akaacha kazi, nasikia yuko Dar kahamisha kila kitu chake, hivyo ananiambia nitakuwa nakuja kila weekend!

Ni mwaka wa pili sasa, mke wangu namuona kila anapotaka yeye, sijui hata anaishi wapi huko Dar, nikitaka kwenda ananiambia unakuja kwani wewe ndiyo unalipa kodi, hataki hata kunizalia kiasi mimba anatoa, nipo tu hata sijui nafanya nini, nguvu ya kumuacha sina, hata nguvu ya kuchepuka sina!
 
Swahili: Kama sio chai, basi wewe fala.

English: If it's not tea, then you're fala.

Spanish: Si no es té, entonces eres fala.

Nyarwanda: Niba atari icyayi, noneho uri fala.

Hindi: अगर यह चाय नहीं है, तो आप फ़ला हैं।

Dutch: Als het geen thee is, dan ben je fala.
 
Hakuna mwanamume hapo huyo ni binti wa kiume wanaishi kama lesbians

Wanaume huwa tuna muscalinity hakuna mwanamke anaweza kumwendesha a muscaline man
Hakika 100% ndiyomaana Ke wengi sana huongozana kwa kina Sangoma kupewa hirizi na kushinikizwa masharti ya ajabu ajabu ilimradi tu amtawale Me kimahusiano.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Alipomaliza chuo, nilipomuambia mambo ya kumuoa, akaniambia hapana, subiri mpaka nipate kazi, kuna mambo namalizia, nikajitahidi kuhangaika, kuna mshikaji wangu akamuunganishia, akapata kazi benki. Mshahara laki 6, sijakaa miezi miwili, ananiambia kuwa ananunua gari, nikawaza kwamba maisha gani ananunua gari, akanambia nimechukua mkopo kazini.

Mimi nikatulia, akanunua hiyo gari, nakumbuka kipindi kile IST alinunua milioni 14, nikasema poa, haina shida. Naongelea mambo ya ndoa, ananiambia mimi sina shida kuhusu kunioa, lakini siwezi kuishi huko, nataka kuishi Dar au Morogoro. Nikamuambia mimi niko Dodoma, unafanya kazi Dodoma, kwanini utake kuhama?

Akanambia, ndiyo nimeamua, kama unataka kunioa basi ni kati ya mikoa hiyo. Nikasema isiwe shida, tutahamia huko, basi tukafunga ndoa, mara kanambia anaacha kazi, anahamia Dar kama alivyonambia kwani kapata kazi nyingine huko, nikamuambia mimi uhamisho kuja Dar mgumu, ananiambia kwani nani alikuambia nataka uhamie na mimi.

Mimi sitaki kuishi na wewe, baki Dodoma, mimi nataka kuishi Dar, siwezi kuishi na mwanaume 24/7. Tukagombana, nampigia mama yake, ananiambia kama mwanangu hataki kuishi na wewe kwanini unanilazimisha. Sijakaa sawa, akaacha kazi, nasikia yuko Dar kahamisha kila kitu chake, hivyo ananiambia nitakuwa nakuja kila weekend!

Ni mwaka wa pili sasa, mke wangu namuona kila anapotaka yeye, sijui hata anaishi wapi huko Dar, nikitaka kwenda ananiambia unakuja kwani wewe ndiyo unalipa kodi, hataki hata kunizalia kiasi mimba anatoa, nipo tu hata sijui nafanya nini, nguvu ya kumuacha sina, hata nguvu ya kuchepuka sina!
Hizi mada mkipost kuna watu wanaiga wanaenda kuchomwa na magunia ya mkaa, wanaume wengi hatupo hivi.
 
Swahili: Kama sio chai, basi wewe fala.

English: If it's not tea, then you're fala.

Spanish: Si no es té, entonces eres fala.

Nyarwanda: Niba atari icyayi, noneho uri fala.

Hindi: अगर यह चाय नहीं है, तो आप फ़ला हैं।

Dutch: Als het geen thee is, dan ben je fala.
Kihindi pekeyake kimekataa fala
 
Back
Top Bottom