Mke wangu ananiumiza kichwa

Habari za jumatano wanajamvi, bila shaka mmeamka salama kabisa.

Leo nimekuja huku kuomba ushauri maana tangu usiku sijalala kichwa kinawaka moto.Nimeoa miaka minne ilitopita, kabla ya hapo niliambiwa kabila la Mbulu sio la kuoa mie moyo ukawa umenasa hivyo na pete kanisani ikavaliwa. Nimebarikiwa mtoto mmoja wa kike.

Mwaka 2011 nilimfungulia account facebook mchumba kabla sijamuoa na nilikuwa namuamini sana.Tatizo Jana (Jumanne nikiwa kazini akaniambia account yake imesumbua halafu njia ndio mie hivyo nikiwa kazini nikalog in kwenye account yake (ikumbukwe tangu nimuunge sijawahi ingia kwenye inbox wala kugusa simu yake) baada ya kumrekebishia tatizo lake nikaona niingie inbox kwa mara ya kwanza.

Ukweli mie sinywi pombe lakini Jana nilijikuta naondoka kazini mapema na kwenda kuzimua kichwa. Nimekuta message nyingi anachat na vijana za ajabu ajabu mara mume wangu nitamuaga naenda kwa ndugu nitakuja kwako, mara mume wangu hayupo halafu nipo kitandani peke yangu baridi kali, Mara nimetoka kuoga ndio najifuta now, halafu anagawa namba yake ya simu kirahisi kwa kila anayemuomba namba. Yaani nusura nianguke ofisini maana mpaka wenzangu wamejua kuna tatizo ila sijafungua mdomo wangu.

Nimerudi nimemkuta ananichekea yani sijaongea kitu roho inaniuma vibaya, nahangaika kutoa jasho kwaajili ya kumpendezesha na mtoto wetu ila kaniona boya. Wakati naanza uhusiano nae nilikuta akiwa na elimu ya darasa la saba tu, nikamuendeleza QT na kumfundisha mpaka now ana diploma na October anaingia degree, sijui hata nifanye nini haki ya Mungu inanitesa sana.
Huwa najiuliza ishu kama hizi zikinitokea nikija Kuoa nchukue uamuz gan? MaanA najijua huruma kwenye cheating ctakuwa nao
 
Hakunipa password bali account nilimfungulia mie na sikuwahi kufatilia...account yake ikasumbua na akawa hana ujanja kabisa ndio akaniambia nimrekebishie na kumbadilishia password ndio hapo hayo yote yakaibuka Mkuu wangu
Login upya afu badili password bila ye kujua
 
Huwa najiuliza ishu kama hizi zikinitokea nikija Kuoa nchukue uamuz gan? MaanA najijua huruma kwenye cheating ctakuwa nao
Hv kwanini mwanaume akicheat wanawake tunavumilia ila mwanamke akicheat hata kama mwanaume ndo kasababisha kuna zero tolerance??
Naomba kueleweshwa hapa, why can't u forgive a cheating wife akiomba msamaha ili muanze moja
 
Miye naumwa kichwa zaidi yako. Kuna kaswali kananisumbua sana kichwani. Je, haiwezekani kuwa umepunguza mawasiliano na mkeo?? Kama mnawasiliana vizuri kimwili na kiroho huyo mama atakuwa mjinga kiasi gani kukuambia ati umsaidie kutatua account yake ya fb??
Huenda hata haekewi inavyo fanya kazi lakini sasa akuombe kweli huku akijua kuwa kwa utaalam wako waweza pia kuisoma?? Kuna sababu hapo. Labda alitaka tu ufunguke ujue kuwa una mke nyumbani. Wanaume wengi huwa tunasahau wajibu wetu nyumbani. Mke sio wa kununulia unga na mboga tu bali na mawasiliano madogo madogo ni ya muhimu pia.
Swali la kizushi tu;
Mkuu. Umemwambia mkeo huyo;" Nakupenda" mara ya mwisho ni lini? Mwanamke bwana; anahitaji ugali mwingi sana, lakini maneno ya kumbembeleza mawili humshibisha kuliko ugali mwezi mzima.
 
Justifiable u knw,the guy hayupo miezi 3 afu ukute he never calls wala kumuweka mke karibu unategemea nini...baadhi ya waume mnajisahau sanaa
Cheating can never be justified....well at least according to me.
 
Miye naumwa kichwa zaidi yako. Kuna kaswali kananisumbua sana kichwani. Je, haiwezekani kuwa umepunguza mawasiliano na mkeo?? Kama mnawasiliana vizuri kimwili na kiroho huyo mama atakuwa mjinga kiasi gani kukuambia ati umsaidie kutatua account yake ya fb??
Huenda hata haekewi inavyo fanya kazi lakini sasa akuombe kweli huku akijua kuwa kwa utaalam wako waweza pia kuisoma?? Kuna sababu hapo. Labda alitaka tu ufunguke ujue kuwa una mke nyumbani. Wanaume wengi huwa tunasahau wajibu wetu nyumbani. Mke sio wa kununulia unga na mboga tu bali na mawasiliano madogo madogo ni ya muhimu pia.
Swali la kizushi tu;
Mkuu. Umemwambia mkeo huyo;" Nakupenda" mara ya mwisho ni lini? Mwanamke bwana; anahitaji ugali mwingi sana, lakini maneno ya kumbembeleza mawili humshibisha kuliko ugali mwezi mzima.
Mwanaume yuko radhi aseme pembeni nampenda sana LadyRed ila kuniambia mwenyewe live hasemii ng'oo,how can I know u never tell me??
Mwanamke sio mambo ya hela tu sijui vyakula na mavazi,jenga urafiki na mke wako ujue maisha yake yanaendaje hata ukiwa mbali
 
Umenikumbusha mbali sana. Mimi huwa sisemi. Ila niliwahi kuwa na pasua kichwa mmoja yeye always alikuwa ananiambia 'i know u love me even if you dont say it'.....matendo yana maana kuliko maneno, vitu unavyomfanyia mtu ni muhimu kuliko hizo three words I LOVE YOU....
 
Hahaha nna kisiki cha mpingo hiko hadi sangoma kaniambia he's madly in love Ila hajawahi sema,matendo tu yanaongea,..msemage jmn japo once in a year
 
Back
Top Bottom