Naomba ushauri: Kuna mtu kamtongoza mke wangu

GeofK

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
837
1,036
Mimi ni mtumishi wa idara X, lakini pia ni mjasiriamali, hapo nyuma mke wangu alikuwa anashinda ktk duka letu dogo lakini kwa sababu za kiafya (anasumbuliwa na maumivu ya Mara kwa Mara ya mgongo) ili tulazimu apumzike nyumbani halafu hapa dukani nitafute mfanyakazi, na pia tuwe na binti wa kazi, huyu binti wa kazi pamoja na majukumu ya nyumbani lakini pia alikuwa anaenda kuuza barafu ktk shule iliyojirani ili tujipatie kipato zaidi, maisha yameendelea.

Katika nyumba ambayo kuna Hilo duka langu walihitaji kufanya marekebisho ya nyumba hivo ilitulazimu kusimama biashara Kama kwa miezi miwili hivi, takribani Kama mwezi 1.5 uliopita binti wa kazi alipata dharura akaenda kwao, na ndio ikawa 1 kwa 1. Hivo kwa vile wife alikuwa tu home basi mwanzoni alianza kwenda kuuza barafu mwenyewe ktk shule ile ya jirani. SHIDA NI KAMA ILIANZIA HAPO. Kwani Mara kadhaa nilisikia akiongea na mwalimu wa hiyo shule kumuuliza Kama wanafunzi wanaenda shule, Kuna wakati pia yule mwalimu alimwambia wife kuwa yeye awe anapeleka tu barafu halafu pesa anafata badae, nikamwambia wife hapana, Sasa juzi kutwa usiku mida ya saa 3 nimerudi home sa wife akasahau simu yake jikoni nikasema nimpelekee, akili ikanituka ktk sms, ktk inbox kukawa na sms za kawaida, ila ktk sent items kukawa na sms zifuatazo:

1. Haunitakii mema, unataka watoto wangu walelewe na mama wa kambo?
2. Hizo ni porojo kama porojo nyingine, ishi na mkeo nami niishi na mume wangu.
3. Haiwezekani kwani utaniharibia ndoa yangu.

Ghafla nikakutana na wife akanipokonya simu Ile kw maneno kuwa mbona nashika simu yake, nikamjibu kuwa mi nilikuwa nakuletea.. Nikaachana naye nikaenda kuoga, badae wakati narudi kulala nikamuhoji akasema ni kweli Kuna mwalimu alimtongoza lakini yeye wife akamkataa, na pia akasema kuwa Kuna siku alimpigia simu huyo dada wa kazi (Maria) kuhusu taarifa za yule mwalimu na akajibiwa kuwa n mtu ambaye Yuko ktk familia, nikajiuliza n kwa nn alimuuliza Maria kuhusu taarifa za yule mwalimu, lengo n kwamba afahamu nn kuhusu huyo mwalimu.

Katika maongezi akasema kuwa yeye wife hakumkubalia yule mwalimu na hata sms zinajieleza, nikahoji suala la kutokukuta inbox za yule mwalimu akasema kuwa simu yake n ndogo hivo hakuona umuhimu wa zile sms hivo akaamuwa kuzifuta, kesho yake asbh nikiwa kazini nikamtumia text kuwa anitumie namba ya simu ya yule mwalimu sa akachelewa kuituma ikabidi nimpigie, akasema kuwa hawezi kuituma kwani hataki matatizo zaidi yahusuyo suala Hilo, na akagoma, jioni nimerudi home nikamwambia tena suala la namba akasema kuwa ameshaifuta na hata sms hazipo Tena, nikakosa jibu. Leo asbh nilimwambia kuwa hataenda tena kuuza barafu ktk Ile shule, mchana Kaja dukani akawa anasema mbona n Mara nyingi tu alikuwa akinkuta mm na sms za wanawake wengine, sikutaka kulijibia hilo,... NIKO STRESSED NA SUALA HILI ninaomba ushauri marafiki

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mambo ya hisia hayanaga ushauri,

Anyway, huyo kamkataa inaonekana kabisa.

Ila mimi siamini majadiliano ya mtu na mke baada ya msimamo.

Majadiliano ni dalili kwamba baada ya mda ataliwa.

Wewe upo na hatari maana hana hofu kwa Sababu na yeye kakushika
 
Back
Top Bottom