Mke wangu ameniomba nimtaftie mwanamume wa kumliwaza

kumbe.. Mwache basi uoe mwingine lakini hakikisha anamtafuta mama ako ili liwe chaguo lake watapatana usichague wewe mama ako asijegombana nae ukamuacha tena

manake mama yake ndie anaemuoa na kuishi na huyo mwanamke au?jamani tunahitaji kumpa kila mtu nafasi yake,hakuna alie na umuhimu sana kuliko mwingine,mama ataendelea kuwa mama yako na mkeo aliyekuzalia watoto ataendelea kuwa mkeo.kila mmoja ana nafasi yake kulingana na role yake anayoiplay.
 
Asalam aleikum, mimi ni mwanaume rijali mwenye mke 1 na watoto 2,kwa muda mrefu mke wangu amekua haelewani na mama yangu mzazi, na kila ninayeongea naye ili kujua tatizo anamlaumu mwenzie, nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu kama mnavyojua hakuna kama mama,matokeo yake nikiwa kazini nimepokea ujumbe toka kwa wife kuwa nanukuu "nakupenda sana mume wangu,kama umeamua hivyo basi nakuomba unitaftie mtu wa kuniliwaza maana mm sijui pa kuanzia na siwezi kuvumilia upweke tena" nimeshindwa kujua nimzibue au nimfukuze,mpaka sasahivi niko bar nagonga maji na nina mawazo tele,msaada jamani nifanyaje

"Ukweli na Uwazi", mlaumu Nkapa.
 
Wewe ni kichwa cha familia kaka , kwanini usichunguze ukaona tatizo ni nini?? Huyo ni mama yako wewe lazima utakuwa unafahamu mapungufu yake, sasa ndipo mahali pa kumtia moyo mwenzio, Hebu fikiria mkeo mpaka anafikia hatua ya kukwambia umtafutie mtu wa kumliwaza kaka hujisikii vibaya kama una mtesa mwenzio??? Maisha ya ndoa ni kuvumiliana na kuchukuliana mizigo, huenda ikawa mama yako anatatizo, nakwambia hivyo sasabu nina experience na maisha hasa ya ndoa, kina mama wakwe wana matatizo sana kaka,
mfano: Mama amekuja kukutembelea lakini anataka yeye ndio atawale nyumba yako
anataka kila atakachoona mkwewe amevaa na yeye anataka, na ikitokea amepewa kitu ataona kama ni kibaya.

MIMI : nakushauri kaa na mkeo mmalize hilo tatizo siyo vema mnawapa picha gani watoto wenu
 
Mama na mke hawaingilia ktk nafasi zao kimsingi huna uwezo wa kuishi na mama yako na mkeo hivyo fanya utaratibu mama akaishi Ushagoo au kijijini nawe uishi na mkeo mjini, shida yako ni hekima na busara huna kama una rafiki unaeelewana nae vizuri mpe nafasi yako
 
inaniudhi sana pale mwanaume bila aibu anapoweka wazi kabisa
yuko tayiri kumpiga mkeo ama kumfukuza kwa kosa ambalo halina miguu.
yeye amekuuliza "umtafutie mtu mwingine" amefanya jambo zuri sana kukuuliza.

umesema mwenyewe " nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu " ndio uliyosema hayo..

sasa unategemea mkeo afanye nini???

wanaume wengine bana mtasema hamjaziliwa na wanawake.. aibu sana

Umemjibu vizuri sana huyu jamaa....kwakuongezea huko bar anafanya nini. Je yeye chakula anapata...au hapati...isijekua yeye anapata nje ya nyumba chakula halafu mwenzie anamnyima.....DUH....NGOJA NIVUTE SHUKA NILALE MIE
 
au vortex wamemnywesha 'teboksin babebyutenol'?

Inaonekana his mind is being controlled somewhere.
 
Asalam aleikum, mimi ni mwanaume rijali mwenye mke 1 na watoto 2,kwa muda mrefu mke wangu amekua haelewani na mama yangu mzazi, na kila ninayeongea naye ili kujua tatizo anamlaumu mwenzie, nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu kama mnavyojua hakuna kama mama,matokeo yake nikiwa kazini nimepokea ujumbe toka kwa wife kuwa nanukuu "nakupenda sana mume wangu,kama umeamua hivyo basi nakuomba unitaftie mtu wa kuniliwaza maana mm sijui pa kuanzia na siwezi kuvumilia upweke tena" nimeshindwa kujua nimzibue au nimfukuze,mpaka sasahivi niko bar nagonga maji na nina mawazo tele,msaada jamani nifanyaje

Kama hakuna kama mama yako kwa nini hukumuoa yeye?

Haya maisha yenu ya kiswahili yanachekesha sana. Mama yako anaamuaje mambo ya nyumbani kwako? Halafu hata hufichi ujinga wako, eti unaacha kumpa unyumba mkeo umkomoe! Kwanza kafuata nini kwako?

Mama kama alikuja kuwasalimia na aende arudi alikotoka. Kama hakuna mtu mwingine wa kumuangalia basi angalia namna ya kumuhifadhi. Maisha ni wewe na mkeo na sio ndugu zako.

Suala la wewe kuwa rijali halituhusu mkuu. Umeanza na asalam aleikhum na hii ni salamu ya jamii fulani, at the same time unasema upo bar unakunywa, je wewe ni kafiri au halal? Tutakapoweka kipengele cha dini kwenye sensa ya 2022 wewe tukuhesabu upande gani?

Ningekuwa jirani yako ningekufunza adabu ukamheshimu mkeo. Shida ni kwamba hapo mtaani kwenu wanaume wachache ndio maana unajishaua
 
Kulinganisha mke na mama yako, kumbe wana mahitaji sawa? Na sie wamama tunatakiwa tujipange kuacha watoto wetu wa kiume wakikua waanze maisha na familia zao mpya. Lazima mama mzazi ujifunze kunyamaza. Lazima mume uwe hodari wa kuwaunganisha hawa wanawake wawili kwa busara, si nguvu, kama bado hujaweza kubalansisha, mtoto wa mama, huwezi kusimamia familia yako?
 
Umemjibu vizuri sana huyu jamaa....kwakuongezea huko bar anafanya nini. Je yeye chakula anapata...au hapati...isijekua yeye anapata nje ya nyumba chakula halafu mwenzie anamnyima.....DUH....NGOJA NIVUTE SHUKA NILALE MIE
mi nina kademu kangu ka zamani sana,huwa mke akinitibua naenda kuliwazwa
 
mwanamke ataniambiaje nimtaftie mwanaume,huku si kunidharau kabisa

Sio kukudharau, kwani amefuata nini kwako kama kitanda kwao kipo, kama msosi upo na kama nyumba ipo alikuwa halali nje kwao hivyo jiulize kwanini mtu anaolewa, hiyo ni njia nzuri tu ya kutaka mzungumze, wanaoogopa wataonekana wanadharau huwa wanachukua maamuzi ya kucheza mechi za mchangani
 
Ndio, mtafutie mtu wa kumliwaza. Kama una akili lazima ujue kama huna huyo mtu jipeleke mwenyewe.

Skia my dear asikuumize kichwa...mjibu tu kama umeshindwa mwenyeo kutafuta me ntawezaje?...nae utakua ushampa adabu yake

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 
Mh ...wengine tunatafuta wa kuoa wengine wanafikiria kuwapiga na kufukuza.
Life aint fair aisee...
 
Man hear this, the One who is wise is cautious and turns away from evil, but a fool is reckless and careless.
 
Asalam aleikum, mimi ni mwanaume rijali mwenye mke 1 na watoto 2,kwa muda mrefu mke wangu amekua haelewani na mama yangu mzazi, na kila ninayeongea naye ili kujua tatizo anamlaumu mwenzie, nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu kama mnavyojua hakuna kama mama,matokeo yake nikiwa kazini nimepokea ujumbe toka kwa wife kuwa nanukuu "nakupenda sana mume wangu,kama umeamua hivyo basi nakuomba unitaftie mtu wa kuniliwaza maana mm sijui pa kuanzia na siwezi kuvumilia upweke tena" nimeshindwa kujua nimzibue au nimfukuze,mpaka sasahivi niko bar nagonga maji na nina mawazo tele,msaada jamani nifanyaje

Ni kweli hakuna kama mama lakini pia hakuna kama mke, mpaka unazaliwa na kuoa maana yake ulikuwa una kwenu ambapo ulitoka na kuenda kujenga maisha mapya na mkeo hivyo mama yako kama yupo hapo ni kama mgeni hivyo busara inatakiwa ku-handle hiyo issue na wakati mwingine wewe ndio inaweza kuwa chanzo kwa kutokuwa na msimamo kwa pande zote mbili kwani kwa kauli yako ya utangulizi kwamba wewe ni mwanaume rijali inaonyesha ni mtu unaependa kuabudiwa flani kwani ungeleta bado bila kujitambulisha hivyo kulikuwa kuna shida gani. Maamuzi uliyochukua sio kwani mara nyingi watu huwa wanawaona wazazi wao kuwa sahihi wakati mwingine sio kweli, kama umeshindwa kuelewa nani mwenye makosa si haki kumnyima haki yake ya msingi mkeo pia hiyo si adhabu bali ni kukuza tatizo kwani tafsiri yake hata wewe unatoka na ndio maana ukabadilisha hata mfumo wako wa maisha kwa kuchelewa kurudi hivyo na yeye anaweza akaamua kuchukua kitu kipya hivyo wajanja wakakusaidia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom