Barua kwa atakayekuja kuwa mke wangu

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,272
Natumai u mzima wa afya mke wangu, mimi naendelea vizuri sema niombee sana ukipata muda, haijawahi pita siku sijakuombea, hivi uko wapi?, unafanya nini?, tutaonana lini?, itakuwa wapi?,,mke wangu roho inaniuma kila nikiwaza kuwa kuna uwezekano mkubwa upo namwanaume saizi, mke wangu napata wivu kutokana na ukweli kwamba Kuna mwanaume mwingine unampenda sasa hivi, mke wangu natumia muda,pesa na hisia nyingi kwa wanawake ambao hawastahili hivi vitu vya thamani kutoka kwangu hivi uko wapi nikupe stahiki yako?

Hivi mke wangu umezaa au bado? eti mke wangu una watoto au hujawahi kuzaa? mke wangu ulishawahi kutoa mimba? mke wangu we ni dini gani? ujue nna shauku sana ya kujua hayo yote?, mke wangu unakuja lini sasa? nimechoka kusuburi, nimechoka ubachela mke wangu, nimechoka kula migahawani mke wangu, mke wangu we ni mpishi mzuri eeh??.

Mke wangu utawapenda baba na mama angu?, dada zangu utawezananao kweli mke wangu?, Kuna huyo mmoja anaongeaa sana ila ndo anaongoza kukuulizia mke wangu, ananiuliza Kila siku ntakupeleka lini nyumbani akakuone, mke wangu dada zangu mimi ndio kaka yao pekee si umeona mzigo unaokusubiri?, mke wangu baba na mama ako si bado wanaishi au walitangulia mbele za haki? kama walitangulia pole ila kama wapo natamani kuwaonaa niwashakuru Kwa kunizalia wewe, uje basi mke wangu njoo mda unazidi kwenda mke wangu.

Mke wangu ulevi wangu pekee ni mpira wa miguu napenda kuungalia na napenda kucheza pia, vipi wewe mke wangu kilevi chako Nini?, Kama unapenda mpira pia nitafurahi sanaaa, tutaangalia wote na kubishana sanaaa, ntakasirika timu yangu ikifungwa utanicheka na utafurahi sana, vivyo hivyo timu yako ikifungwa ntakucheka sana, mke wangu we ni simba au yanga?, Ningependa tuwe wapinzani ila sio mbaya tukiwa timu moja pia, ntakuwa naenda kucheza mpira jioni lakini Kwa ruhusa yako si utaniruhusu? Ntakuangalia mpira kibanda umiza na rafiki zangu usiku vipi utaniruhus?

Mke wangu swala la mimi kuchepuka litakuwa mikononi mwako, ukinipenda kunijali na kunisikiliza kwanini nichepuke? kwanini nichepuke wakati wewe upo nyumbani unanisubiri?, kwanini nikalale na mwanamke mwingine wakati mwanamke wangu upo, kwanini nikalale kitandani na mwanamke mwingine wakati kitandani kwangu uko peke ako, kwanini nikupgie mke wangu?? Kwanini nikudhalilishe Kwa majirani mke wangu? Kwanini tusitoke angalau Kila mwisho wa mwezi mke wangu? Kwanini wote tusiende kuabudu angalau mara Moja Kwa wiki mke wangu?

Najua Kuna siku utaniudhi sana mke wangu, ikatokea nimekupiga nisamehe nikikuomba msamaha ni hasira tu ila bado nakupenda, ntakutamkia TUACHANE ni hasira uwezo wa kukuacha sina mke wangu, utapiga simu sitopokea mke wangu ntakuwa busy nielewe, Kuna siku ntakuachia hela ndogo ya kula mke wangu ntakuwa tu nimeyumba kiuchumi tu nielewe ntakaa sawa.

Mke wangu ntakuwa na marafiki wengi husijenge sana mazoea nao, marafiki zako ntakaa nao mbali mke wangu, uwe makini pale mtaani tutapoishi, kuwa makini na aina ya marafiki utaowachagua mke wangu, kuwa makini na malezi ya watoto wetu, kuwa makini na bosi wako, kuwa makini na bosi wangu mke wangu, kuwa makini na ndugu zangu alafu kuwa makini zaidi na ndugu zako, kuwa makini sana na yule kiongozi wa dini, kuwa makini sana na mwalimu wa mwanangu, kuwa makini na yule dereva boda mke wangu, kuwa makini na yule daktari, nakupenda na nakupenda wewe tu.

Mke wangu niambie ukweli, niambie hupendi kuniona nachelewa kurudi nyumbani, hupendi ukaribu wangu na Aisha, hupendezwi na ukaribu wangu na James, hupendi ukaribu wangu na bosi wangu wa kike, nikumbushe mke wangu kwanini muda mrefu sijaenda kusalimia wazazi wako, mke wangu niambie kwamba shemeji yangu anahitaji ada ya shule, niambie kukukalipia Kila siku kunakuudhi, niambie sikupi muda wa kutosha, niambie uwezo wangu kitandani umepungua kwanini alafu wote tutafute suluhu, nikumbushe kwamba sijaenda kusali mda mrefu umepita.

Mke wangu siku nyingine niombee wewe, niombee mchezo, niombee mwichi, niombee muwa, niombee jembe likulime, nipe kwenye kochi mke wangu, nipe jikoni, nipe chooni, we nipe tu popote mpaka nisimuwaze yeyote zaidi yako, nakupenda mke wangu.

Mke wangu najua wewe sio mkamilifu, ukikosea ntakuonya na ntakutaka ujirekebishe, ukijirekebisha tutaishi maisha ya amani na furaha sana, husipojirekebisha mke wangu, husiponisikiliza mke wangu, ukichepuka mke wangu, ukiwa mchoyo mke wangu, husipowapenda ndugu zangu mke wangu, ukinyanyasa wanangu mke wangu, ukiendekeza ushirikina mke wangu, ukiwa mfujaji Mali mke wangu, ukiwa na wivu uliopitiliza mke wangu, ukiwa mpenda hanasa sana mke wangu, ukiwa unapenda kunitushia kifua mke wangu, ukiwa unapenda kutishia kuondoka mara Kwa mara mke wangu na tabia zote zinazofanan na hizo, mke wangu mimi sitosita KUKUACHA mke wangu mpendwaa.

Kwahiyo unakuja lini??


#OneDayYouWillBeGone
Dr criminal
 
Back
Top Bottom