Mke wangu ameniomba nimtaftie mwanamume wa kumliwaza

wewe ndio una matatizo makubwa kuliko huyo mkeo.... umeonekana kupoteza heshima ya kuwa mume ndio maana unafanya vitu vya ajabu na mkeo yuko sahihi kabisa kusema kuwa umtafutie mwanamume mwingine kwa kuwa wewe umeshindwa kusimama katika nafasi yako.... think twicw bro kama kweli ulistahili kuoa ama la
 
we unaonekana bado una mambo ya kijijini wewe,huna chochote.yaani unashindwa kukaa chini na mkeo ujue tatizo lake unakimbilia kutafuta solution bar???piga mkeo mboko za kueleweka usiku then mbembeleze atakuambia.vinginevyo we sio mwanaume kamili
 
nipe namba yake kama hatakwambia ili nikusaidie,ataniambia halafu ntakwambia wewe.pole sana
 
duniani kuna mambo kiukweli eti kisa mkeo hawaelewani na mama yako ndo eti unamkomoa kumnyima tendo la ndoa lol
 
Mkuu hapo baa hakikisha round za menu nazo zinaendana na biere "pig uipana kwa kuanza wikend mapema"
Kwenye hili suala lako nakushauri usinywe pombe kwa stress matokeo yake huwa mabaya sana kunywa kwa
starehe tu.
rudi home utatue tatizo na wife kaka ucje kukuta mtu ameanza kumliwaza wife ikawa shida
 
Nionavyo mimi tayari una nyumba ndogo unataka kuhalalisha, huku unatafuta sababu tu. Angalia sana mambo ya kuwa na mama mzazi nyumbani kwa muda mrefu. Huyo mama yako kwa nini hayupo na mumewe (baba yako)?, huenda ameshaharibu huko. Tunza ndoa yako, lea watoto wako. This is my take.
 
Asalam aleikum, mimi ni mwanaume rijali mwenye mke 1 na watoto 2,kwa muda mrefu mke wangu amekua haelewani na mama yangu mzazi, na kila ninayeongea naye ili kujua tatizo anamlaumu mwenzie, nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu kama mnavyojua hakuna kama mama,matokeo yake nikiwa kazini nimepokea ujumbe toka kwa wife kuwa nanukuu "nakupenda sana mume wangu,kama umeamua hivyo basi nakuomba unitaftie mtu wa kuniliwaza maana mm sijui pa kuanzia na siwezi kuvumilia upweke tena" nimeshindwa kujua nimzibue au nimfukuze,mpaka sasahivi niko bar nagonga maji na nina mawazo tele,msaada jamani nifanyaje

Hamjoana nyie, walioona wanaambiana kila kitu. Mke wako angekuambia kama kweli mnapendana na mama yako kama anamapenzi ya kweli angekuambia kila kitu. Hapo wanakuona wewe huna msimamo ndo maana kila mmoja anasita kukueleza ukweli.
 
Asalam aleikum, mimi ni mwanaume rijali mwenye mke 1 na watoto 2,kwa muda mrefu mke wangu amekua haelewani na mama yangu mzazi, na kila ninayeongea naye ili kujua tatizo anamlaumu mwenzie, nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu kama mnavyojua hakuna kama mama,matokeo yake nikiwa kazini nimepokea ujumbe toka kwa wife kuwa nanukuu "nakupenda sana mume wangu,kama umeamua hivyo basi nakuomba unitaftie mtu wa kuniliwaza maana mm sijui pa kuanzia na siwezi kuvumilia upweke tena" nimeshindwa kujua nimzibue au nimfukuze,mpaka sasahivi niko bar nagonga maji na nina mawazo tele,msaada jamani nifanyaje

Yaani wewe unaleta habari za ndugu, or mama kwenye ndoa yako? kwa mtindo huu ndoa yako itakuwa soon!!! Na kwa hakika kama mke umemuoa halafu humpi haki yake je akienda kuitafuta nje utamlaumu? Tena namsifu sana huyu aliyekuomba eti umtafutie!!! Sasa usipomtafutia mashoga au yeye atatafuta mwenyewe na akipata wa kumfikisha sawasawa basi sahau tena mke huna.
 
Yaani nimeamini kuwa wanaume wanawaza kwa kutumia pua na sio akili, siku zote ukitaka ndoa yako iwe salama, kaa mbali na wazazi wako wewe mwanaume na hata wazazi wa mke. Wazazi waishi kwao na wewe ishi na mkeo na watoto wako tu, hata biblia imeandika, 'mwanaume atamwacha baba na mama yake ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja', sasa wewe unaambatana na mama yako kivipi? Unasema umfukuze mkeo umwache mama yako, je atakupa akupacho mkeo? Hata kama utaoa mwanamke mwingine hataweza kuwa kama yule wa kwanza, je na wanao je? Walelewe na mama kambo kisa mama yako mzazi? Na kama mama yako ameshindwa kuishi na huyo mkeo, ukileta wa pili ndo ataweza kuishi naye? Think twice ndugu yangu, tumia ubongo na akili kwa kufikiria na sio pua au mdomo, in short unakera.

kama hajaelewa hataelewa kamwe!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom