Mke wangu ameniomba nimtaftie mwanamume wa kumliwaza

Mkumbavana

Member
Jan 24, 2012
79
22
Asalam aleikum, mimi ni mwanaume rijali mwenye mke 1 na watoto 2,kwa muda mrefu mke wangu amekua haelewani na mama yangu mzazi, na kila ninayeongea naye ili kujua tatizo anamlaumu mwenzie, nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu kama mnavyojua hakuna kama mama,matokeo yake nikiwa kazini nimepokea ujumbe toka kwa wife kuwa nanukuu "nakupenda sana mume wangu,kama umeamua hivyo basi nakuomba unitaftie mtu wa kuniliwaza maana mm sijui pa kuanzia na siwezi kuvumilia upweke tena" nimeshindwa kujua nimzibue au nimfukuze,mpaka sasahivi niko bar nagonga maji na nina mawazo tele,msaada jamani nifanyaje
 
mwanamke ataniambiaje nimtaftie mwanaume,huku si kunidharau kabisa

mkuki kwa nguruwe mchugu

hata we umemdharau sana kwa kutomsikiliza na kuhamisha makazi bar.
yaonekana unependa kukimbia matatizo yako.

halafu unauliza maswali ya kipumbavu sana
eti nimzibue au nimfukuze.. shenzi sana wanaume kama nyie mfie mbali kabisa
bila hata ya aibu umetuma hii thread uko bar.

huyo mama huko nyumbani ndio anaowapikia hao wanao ,
amewalisha na kuwaweka kitandani we uko bar unawaza kumzibua
akili gani hii. huna aibu kabisa.
 
mkuki kwa nguruwe mchugu hata we umemdharau sana kwa kutomsikiliza na kuhamisha makazi bar. yaonekana unependa kukimbia matatizo yako. halafu unauliza maswali ya kipumbavu sana eti nimzibue au nimfukuze.. shenzi sana wanaume kamma nyie mfie mbali kabisa bila hata ya aibu umetuma hii thread uko bar. huyo mama huko nyumbani ndio anaowapikia hao wanao , amewalisha na kuwaweka kitandani we uko bar unawaza kumzibua akili gani hii. huna aibu kabisa.
taratibu! Mbona unahasira sana
 
Dah nimekasirika sana.. Umesema kila mmoja anamrushia mwinzie lawama ulishawakutanisha ukaongea nao au kila mtu na mda wake? Huyo mke kakosea kweli kukwambia umtafitie angetafuta mwenyewe akajiliwaza
 
taratibu! Mbona unahasira sana

inaniudhi sana pale mwanaume bila aibu anapoweka wazi kabisa
yuko tayiri kumpiga mkeo ama kumfukuza kwa kosa ambalo halina miguu.
yeye amekuuliza "umtafutie mtu mwingine" amefanya jambo zuri sana kukuuliza.

umesema mwenyewe " nikaonelea nikate mawasiliano ya chakula cha usiku/ndoa na mke na niwe nachelewa home ili kumshikisha mke adabu " ndio uliyosema hayo..

sasa unategemea mkeo afanye nini???

wanaume wengine bana mtasema hamjaziliwa na wanawake.. aibu sana
 
kumbe.. Mwache basi uoe mwingine lakini hakikisha anamtafuta mama ako ili liwe chaguo lake watapatana usichague wewe mama ako asijegombana nae ukamuacha tena
maneno si ndio haya, na wewe je uko tayari kuwa wangu,nina kila kitu,nyumba nzuri,magari,pesa
 
hivi wewe ni mwanaume kweli??
kama ndio unatakiwa kujua kwamba mama yako ni wa muhimu kwako sawa na mkeo ni wa muhimu pia kwanafasi yake tena kubwa sana!!!
wewe unaposema umfukuze mkeo ukishafanya hivyo utaenda kumwoa mamako au utatafuta mwanamke mwingine???
na je hicho usichokijua ambacho kinamfanya mamako amchukie mkeo utakizuia vipi ukioa mwingine??
uwe na heshima kwa mkeo, yeye ni ubavu wako unatakiwa umpende kama unavyojipenda mwenyewe....
Halafu uwe na msimamo si jibaba zima la watoto wawili kila kitu unaegeemea kwa mamako!!
Hicho ulichokosa kwa mamako hadi ukaamua kuoa hakikisha unampa mkeo na si kumwadhibu kwa kumnyima maana itakula kwako!!

Sijakuambia umchukie mamako ila kamwe asiwe kiongozi au mshauri pale anapotakiwa kufanya mkeo - hao si wake wenza kwa hiyo anatakiwa awe na mipaka
 
tatizo lako unamlinganisha mke na mama...kila mtu ananafasi yake katika maisha yako....na kwanini unaishi na mama na mke the same house...? Angalia familia yako mkuu..mama alishakuwa na familia yake tayari,kaa nao chini kila mmoja na nafasi yake usolve hiyo issue..kumkomoa mke sio issue utaishia kubaya kaka...amka usingizini...
 
Kuna uwezekano mkubwa wa kutotumia busara zako pindi utakaporudi home kutokana na kilaji ukaamsha watoto kwa magomvi yako. Kata maji yako, kisha ukapumzike kimyaa, mpaka utakapokua sober asubuhi. Ni mtizamo tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom