Masaki
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,463
- 753
Tumeongelea sana elimu, pia kuna vyeo au madaraka hata kama wote ni wasomi. Mke akiwa na madaraka makubwa kumpita mume inaweza kuleta shida fulani aidha kwa mke kujiona yuko juu au mume akawa na complex inferiority!!
Hiyo ya mwanamke kuwa na madaraka makubwa kazini inaweza kuwa tatizo kubwa zaidi kuliko hata kama angekuwa na elimu. Mfano, mwanaume uwe msomi na mwajiriwa wa shirika fulani na una kipato kizuri. Mkeo aingie kwenye siasa, tena siku hizi kama mzaha mzaha tu anaukwaa Ubunge wa viti maalumu halafu Rais anamkandamizia na Unaibu Waziri.....Hapo msipokuwa makini ndoa lazima ilegelege aisee!