Mke Msomi + Mume Msomi = Ndoa nzuri yenye mafanikio?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Tulikuwa tunapiga soga wakati wa kuukaribisha mwaka mpya; moja ya hoja iliyotolewa ilikuwa ni suala la mmoja wetu ambaye alisema kuwa "lazima mke wangu awe msomi bwana, mimi mambo ya kuoa wa darasa la saba simo". Huo ukawa mwanzo wa mjadala mzito wa umuhimu wa usomi (wa elimu ya juu hasa yenye shahada) katika ndoa. Wengine walikuwa wanadai kama wote hamjasoma hamuwezi kuendesha mijadala ya kisomi; na kuwa ndoa haiwezi kudumu au kuwa ya furaha kwani mume anaweza kuwa na dharau fulani hivi kwa mke wake.

Wengine wakasema mwanamke akiwa msomi sana kuliko mwanamme, mwanamme atajiona duni sana na italeta shida kwenye ndoa. Na mmoja akadai wote wakiwa wasomi sana uhusiano wao unaweza kuwa mzuri sana au unaweza kuwa na matatizo kwani itakuwa vigumu sana kumaliza mijadala itakuwa inabakia kuahirishwa na wote wawili wanakuwa very independent minded.

Hadi kengele ya saa sita za usiku inagonga tulikuwa hatujapata jibu muafaka maana tuliona mahali fulani mtu anatangaza anatafuta mchumba na kigezo cha kwanza kabisa kilikuwa "awe na elimu ya chuo kikuu". Mtu mmoja akasema "we unafikiri kwanini baadhi ya wanawake wenye madaraka sana na wasomi wanajikuta hawana waume wa kudumu"?

Hivyo swali linabakia.
 
lakini % kubwa inabakia kuwa mapenzi hayachagui labda kama mpo after kitu fulani
 
(KE)msomi +(ME) msomi = OK OR TROUBLE 50/50
(KE) Msomi + (ME) asiye msomi) = TROUBLE+ TROUBLE mara nyingi
( ME) Msomi +(KE) asiye msomi = POTENTIAL TROUBLE OR HAPPINESS - 50/50
 
Wote mmesoma au hamjasoma muhimu ni maelewano!Kama wote ni wasomi na hamna maelewano mtaishia kubishana kila mmoja akiona yeye ndo mjuaji zaidi!Kwa ambao mmoja ana elimu zaidi ya mwenzake panahitaji uangalifu zaidi maana kama mke std 7 mume PhD itakua ngumu kua kwenye level moja hata kwenye majadiliano ya kawaida tu!Wakiwa na marafiki wa aliyesoma wa std 7 anaweza akabaki anashangaa tu bila kushiriki mazungumzo kwasababu yamekaa kisomi..hiyo itampunguzia kujiamini hata akiwa na mumewe tu!
 
Couples za wasiosoma kabisa huwa zimetulia sana! Refer enzi za ujima na zama za mawe ndoa zilikuwa zinadumu sana.
 
Ole wenu mwanmke aliyesoma hata akawa na Masters, & mumeo Dr, most of time hakuna NDOA hapo, go & search, wanawake wengiiiiiii
wakiwa na high level ya Education say from ka degree, most of them kwenye ndoa are trouble makers, why...!!!? wanachanganya U Beijing (
women rights, gender equality hadi home) & NATURE
that means waliosoma haki degree & above most wanataka KUWA KICHWA NDANI YA NYUMBA, in short mwanmke anataka kuwa dume home, since when..? hamna ndoa hapo, go & do reseach ndogo
 
aaa ah usitudanganye masanilo... Zamani babu zetu walikuwa wakioa wake si chini ya wanne,,,,,, na ukiangalia kitabia hicho alhamdulillah kimetulia sasa hivi,,, yaani ni kumi kwa mmoja wallah...
couples za wasiosoma kabisa huwa zimetulia sana! Refer enzi za ujima na zama za mawe ndoa zilikuwa zinadumu sana.
 
Lakini sisi sote tupo katika mazingira haya je wale waliowasomi wote ndoa zao ni za kheri zaidi - je zina uwezekano wa kupata divorce kwenye mazingira hayo? Inakuwaje kwenye mazingira ambapo mwanamke ndiye msomi zaidi nani anakata mashauri nyumbani? Fikiria mama ni bosi wa wanaume kibao na wanawake kazini halafu anarudi nyumbani mume wake anataka kufanya uamuzi wa mwisho je mwanamke wa namna hiyo kweli akubali au atumie ujiko wake wakiofisi kufanya maamuzi kwa vile anajua sana au yuko katika nafasi ya kujua zaidi?

Inakuwaje kwenye kumsahihisha mtoto? baba akisema hivi na mama akisema vile na wakapingana nani asikilizwe au wamuache tu mtoto aamue mwenyewe?
 
Ubosi unaisha anapotoka tu ofisini...Akifika nyumbani anarudisha upole na unyenyekevu(kwa pande zote!) makali ya ofisini yanabaki huko huko!Newayz elimu sio inayojenga ndoa..yote inategemea wanavyochokuliana!Kama hamna anaetaka kumtawala mwenzake hata kama wamepishana vipi kwa kisomo,amani itakua pale pale!
 
Ndoa ni makubaliano ya wawili japo siku hizi imekaa kibiashara zaidi, ila mke akiwa msomi zaidi ya mume ni fujo fulan hivi!
 
Ndoa ni makubaliano ya wawili japo siku hizi imekaa kibiashara zaidi, ila mke akiwa msomi zaidi ya mume ni fujo fulan hivi!

:A S 41::A S 41::A S 41::A S 8::A S thumbs_up::hug::clap2::clap2::typing:
 
Back
Top Bottom