Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,754
Ndugu zetu Islam na wazee wa Mila wameweza kudumisha ndoa za wenza wengi na kutokana na elimu waliyonayo ni jambo linalowezekana sana na linatibu jamii ambayo infidelity imekuwa order of the day.
Wakristo na Serikali wamejikita kwenye ndoa ya mme mmoja to mke mmoja ambapo ukiangalia ratio ya sensa unaona wazi kabisaa kuna wanawake wanaachwa pembeni kuishi bila ndoa. Jambo hilo hupelekea kuwepo na tatizo la uchepushaji wa mtiririko wa uaminifu wa ndoa.
Mimi nimekuta Babu yangu ambaye alibatizwa Ulutheri akiwa na wake wawili na wote wanatambulika kwenye kanisa hilo na amesalia bibi mmoja anaishi mpaka leo na huduma anapata. Yaani aliyesalia ni bibi mke mdogo. Tukivuta historia ya Baba wa Taifa hakuitwa mtoto haramu ingawa mama yake alikuwa mke wa tisa wa Chifu Burito.
Kipenzi cha Mungu, Mfalme Daudi alikuwa na ndoa zisizoeleweka kabisaa, na yule bwana aliyepewa na Mungu Hekima na Utajiri kuliko wanadamu wote yaani Mfalme Solomon alikuwa na ndoa yenye idadi ya wake pasua kichwa hadi kukinai.
Swali najiuliza; Hii LAZIMA ya mke mmoja ni kitu gani kinasababisha hayo? Hawa wanawake wanaohaha bila ndoa huku wakitamani ndoa wanaionaje pepo ya dunia? Tuchukulie kwamba idadi ya wanaume inapungua kwa kasi kubwa duniani. Je heka heka za kuchepuka zinasuluhishwaje kwa huu utamaduni wa kujifanya tu waaminifu wakati hatuna hata chembe ya kuvumilia ndoa ya mke mmoja?
Tujadili kwa kuelimishana