Ni mfumo wa mpinga kristo ndio leo hii umempa mwanamke mamlaka ya kumshika na kumkaripia mume wake akichepuka

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,141
Kwa kasi hii ya Dunia I hope 50 yrs later wanaume ndio watakuwa wanachumbiwa na kuolewa na wanawake.

Ile mamlaka ya Kiungu na kiuongozi ndani ya mwanaume inapotea taratibu.

Inafika wakati sms tu ya kawaida ambayo haina ushahidi wa 100% kuwa mume wake anaishi kimapenzi na mwanamke mwingine mwanamke anapata mamlaka ya kukaripa, kuonya au kumgombeza mume wake.

Haijalishi mwanamke ni mfanyakazi, mfanyabiashara au mama tu wa nyumbani akihisi tu mume wake ana mchepuko mume atanywea na kuomba msamaha.

Wanaume uungu ndani yao wameuvua sasa na kumvalisha Yezebeli.

Ni asili ya mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja. Lakini wanawake hawataki kabisa huo ukweli.

Sheria za ndoa za dini nyingi duniani zinampa ruhusa mume kuwa na wake wawili na kuendelea.

Ila Sheria ya Roman Catholic church ambayo imekopiwa na makanisa mengine imemuondolea mwanaume mamlaka ya kuwa na mke zaidi ya mmoja.

Najua walikuwa na sababu na hoja za kibinadamu tu.

Hoja kuu ni hii kwamba mamlaka ya wanawake kugombana, kutoa amri au kukaripia waume zao kwasababu zozote zile wameitoa wapi?

Lucifer Mpinga Kristo ndiye kiumbe pekee anayeweza kumpa mwanamke nguvu za kutoa amri kwa mume wake au kumkaripia
 
Back
Top Bottom